Thursday, March 21, 2013

MSANII MATUMAINI ANAOMBA ASAIDIWE....KWA SIKU ANAMEZA VIDONGE 39





Mchekeshaji na muigizaji wa Tanzania Tumaini Martin ‘Matumaini’ amevunja ukimya kuelezea maendeleo ya afya yake akidai kusumbuliwa na maumivu makali ya miguu kwasasa.

Akiongea na BK Cop leo Matumaini amesema kuwa anaendelea kutumia dozi ingawa hali ya afya yake bado si shwari kutokana na kugulia maumivu makali ya miguu hali inayomfanya ashindwe kutembea.

Msanii huyo ameeleza kuwa kwa siku moja huwa anameza vidonge zaidi ya 39 lakini hapati lishe nzuri kwababu ya kutokuwa na pesa na kujinunulia chakula. 

Aidha amedai kuwa wakati alipokuwa msumbiji alipata misaada ya kifedha kutoka kwa wasanii mbalimbali lakini hasaidiwi tena tangu alipofika Tanzania.
‘Niliomba msaada kwenye magazeti ambapo niliacha namba zangu za tigo pesa lakini meseji nyingi nazopokea ni za pole; hata hivyo kuna watu wanadai wametuma kwa namba ya Michael Sangu (Mkt Chama cha waigizaji) ambayo alitoa gazetini lakini mimi sikuwahi kuonana tena na Michael tangu aliponililipia matibabu wakati natoka hospitali’.Alisema Matumaini

Mnamo Februari 9 mwaka huu Matumaini aliruhusiwa kutoka hospitali ya Amana jijini Dar es salaam alipokuwa amelazwa kwa siku tatu tatizo kubwa likiwa ni miguu na alitakiwa kurudi tena hospitali baada ya kumaliza dozi aliyoandikiwa na daktari.

Awali Matumaini alikwenda kuishi nchini msumbiji na kuripotiwa kusumbuliwa na maradhi, lakini alishindwa kutibiwa akiwa huko ambako Naibu Waziri wa Habari vijana na utamaduni na michezo Bw Amos Makalla akishirikiana na baadhi ya wasanii alichukua jukumu la kutoa nauli ya kumrudisha nchini.

No comments:

Post a Comment