Rufaa ya kesi ya Mbunge wa Arusha mjini kwa tiketi ya Chadema, Godbless Lema imetupiliwa mbali na mahakama kumtangaza mbunge huyo kuwa ni halali.
Rufaa hiyo ilisikilizwa na majaji watatu wa Mahakama Rufaa Tanzania ambao ni Engili Kileo, Salum Massati na Benard Luanda kwa pamoja wametupilia madai ya rufaa hiyo.
Mahakama hiyo imewaamuru tena wakata rufaa walipe gharama zote za kesi.
No comments:
Post a Comment