Kundi la wasanii machachali la muziki wa kizazi kipya TMK Wanaume Halisi linaloongozwa na Juma Nature lenye maskani yake Temeke Jijini Dar es Salaam limeibuka kidedea na kuwa mfalme wa Temeke baada ya kulibwaga kundi la Tmk Wanaume Famili katika mpambano wa kumtafuta mfalme wa Tmk lililofanyika jana katika ukumbi wa Dar live Mbagara jijini Dar es Salaam
Juma Nature ambaye ndiye kiongozi wa kundi hilo aliibua hisia za mashabiki wake baada ya kupanda raundi ya kwanza na ngoma aina ya mchiriku huku akisindikizwa na baadhi ya wasanii wanaounda kundi hilo
Akizungumza katika shoo hiyo Nature alisema kuwa aliamini kundi la Tmk wanaume hawataweza kufika round ya pili katika mpambano huo kutokana na uzoefu aliokuwa nao katika fani hiyo
"Aibu yao aibu yao, wamekuja wenyewe hapa ni tatu bila hawafiki round ya pili hao sasa hivi watatoka wenyewe sisi ndio baba zao" alisema Nature
Kundi la Tmk wanaume halisi wakiwa nyuma ya stage teyari kwa kupanda jukwaani kuanza round ya kwanza ya mpambano wao waliingia jukwaani kwa mtindo wa mchiriku |
Dogo Lina akiwasalimia mashabiki waliohudhuria pambano hilo yeye aliongoza mpambano wa round ya kwanza na kusababisha kujizolea mashabiki |
No comments:
Post a Comment