Friday, April 5, 2013

"NATONGOZWA SANA FACEBOOK" ...CHUCHU HANS




Msanii wa filamu Bongo ambaye ni mke wa mtu, Chuchu Hans amefunguka kuwa  anatongozwa sana na wanaume kupitia Mtandao wa Kijamii wa Facebook, kitendo kinachomkosesha amani.

Akizungumza na mwandishi wetu, Chuchu alisema kuwa, anachojua yeye mtandao huo ni sehemu ya kukutana na marafiki na kubadilisha mawazo lakini cha ajabu kila akiingia, wanaume kibao wamekuwa wakimtaka.

“Mimi kwa kweli kila nikiingia Facebook nakutana na wanaume ambao wananitongoza, mtu anajua kabisa una mtu wako lakini bila haya anatangaza dau na kueleza kuwa, anakutaka, mijitu hii naichukia kweli,” 
alisema Chuchu

No comments:

Post a Comment