Msanii anayechipukia kwenye soko la filamu na muziki, Naomi Mbaga ameibuka na kumuonya Husna Idd ‘Sajent’ amuachie bwana wake, January.
Akizungumza na mwandishi wetu, Naomi aliweka bayana kuwa January ambaye ni Mwanamuziki wa Bendi ya Victoria ni mpenzi wake wa muda mrefu hivyo alishangazwa kuona habari mitandaoni kuwa Sajent amejituliza kwa mpenzi wake huyo baada ya kumwagana na mzazi mwenzake, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’.
“Aniachie bwana wangu, kama ameachika kwa huyo Chaz Baba atafute bwana mwingine na siyo wa kwangu. Ole wake nimkute naye siku, atanitambua,” alisema Naomi.
No comments:
Post a Comment