Wednesday, May 22, 2013

KUNDI LA CAMP MULLA LAZIDI KUPASUKA....



Hivi karibuni tuliandika habari kuhusu kundi linaloundwa na vijana wanne wenye vipaji kutoka Kenya linalofahamika kama Camp Mulla kumpoteza member mmoja ambaye ndio aliyekuwa msichana pekee katika kundi aitwaye Miss Karun.


Mwanzo ulianza kama uvumi kuwa Miss Karun amepigwa chini na kundi hilo na nafasi yake kuchukuliwa na msichana mwingine aitwaye Tiri, lakini habari mpya habari zilizothibitishwa Kupitia mtandao wa kituo kikubwa Africa Kusini Channel O, zinasema Miss Karun ameamua kujiondoa kwenye kundi kwaajili ya maandalizi ya kujiunga na chuo. 
  

Miss Karun anategemewa kwenda masomoni nchini Marekani mwezi August mwaka huu, lakini ataendelea kufanya muziki kama solo.

camp m

Kama vile haitoshi, kwa mujibu wa mtandao huo member mwingine aitwaye Thee Mc Africa zamani alifahamika kama Taio Tripper naye amejitoa katika kundi hilo na ataendelea kufanya muziki kama solo. 
  

Kundi hilo lilianzishwa mwaka 2009 likiwa na members wanne, Kwa sasa limebaki na members wawili wa mwanzo pamoja na msanii mpya wa kike aitwaye Tiri.

No comments:

Post a Comment