ELIZABETH Bureko (26), mkazi wa Kata ya Nyamatare, Manispaa ya Musoma, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Musoma, kwa tuhuma za kumchoma na moto sehemu za siri mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minane.
Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Baraka Maganga, ilidaiwa na Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Sajini Stephano Mgaya, kuwa mwanamke huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 24 mwaka huu, saa 3 asubuhi.
Kwa mujibu wa mwendesha mashitaka huyo, mshitakiwa alikiuka kifungu cha sheria namba 169 cha mwenendo wa makosa ya jinai kama sheria hiyo ilivyofanyiwa marekebisho na kuwa namba 16, mwaka 2002.
Alidai kwamba, mshitakiwa huyo alimchoma katika sehemu zake za siri na mdomoni baada ya kumtuhumu mtoto huyo wa wifi yake, kwamba alikuwa akinywa uji wa mtoto aliyekuwa akimnywesha.
Mshitakiwa alikana shitaka na kurudishwa mahabusu hadi Mei 25 mwaka huu, kesi yake itakapotajwa tena
No comments:
Post a Comment