Ijumaa, Septemba 13, 2013
shadrack masatu
MWENYEKITI wa Kamati ya Umoja wa Mashirikisho ya Sanaa Tanzania, Kimela Billa, ameutaka uongozi wa Shirikisho la Muziki Tanzania, kumchukulia hatua ya kinidhamu, msanii wa muziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kwa kosa la kukiuka maadili ya Tanzania katika tamasha la Serengeti Fiesta, mkoani Iringa.
Shilole alipanda jukwaani akiwa anacheza wimbo wake wa ‘Nakomaa na jiji’ huku akiwa amevaa nguo ambazo zinaonesha maumbile yake yote ya mwili.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Billa alisema Shirikisho la muziki chini ya rais wake, Addo Novemba wanatakiwa kuchukua hatua zaidi juu ya shilole kwa kosa la kuwadhalilisha wanawake ikiwa ni pamoja na kukiuka maadili ya Tanzania.
“Hatukatai hayo mambo yapo lakini kwa staili ile sisi kama viongozi wa sanaa hatutaweza kuvumilia, shirikisho la muziki wakishindwa kutekeleza hili lazima kamati ilivalie njuga swala hilo, kiukweli wanalidhalilisha taifa hawa wasanii, mbona wanaume hafanyi shoo zao uchi,? Alihoji Billa.
Alisema shirikisho la muziki liige mfano wa shirikisho la filamu kama lilivowaonya Wema Sepetu na Aunt Ezekiel kwa makosa kama hayo, ambapo anamini kwaasilimia kubwa kunachangia kuwa na nidhamu wanapopanda jukwaani.
“Angekua ameenda kwa shughuli za filamu wangelifanya wao lakini hili shirikisho la muziki wanatakiwa wakae meza moja na Shilole kulizungumzia hilo, wao wanakua wazito kuwachukulia hatua wasanii wa muziki kuliko filamu lakini kwa hili haitawezekana, ,” alisema.
No comments:
Post a Comment