Sunday, June 9, 2013

LADY JAYDEE AMTUKANA MWANA FA KWA KUMUITA " MWANA FAtuma" HUKU AKIMTANDIKA VIJEMBE KWA KUUZA SURA JUZI


Lady Jaydee amemshambulia vibaya MwanaFA. Chanzo cha kuanza kumpa makavu Live ni pale MwanaFA alipo-Retweet post ya shabiki yake mmoja ambaye aliikejeli Show ya Jide kuwa ni Fundraising, ambapo MwanaFA aliongezea neno ‘Daaaamnnn’ kwenye Post hiyo.
 
Mambo yalizidi kuwa mabaya baada ya MwanaFA ku-Retweet post ya shabiki wake mwingine aliyedai kwamba Lady Jaydee anawalipa watu buku buku ili wamponde MwanaFA.

 Hapo ndipo mwanadada Lady Jaydee uzalendo ukamshinda baada ya kutoa warning iliyopuuziwa, akaanza kumchana MwanaFA bila woga lakini MwanaFA hakuweza kujibu kitu zaidi ya ku-Retweet posts za mashabiki wake wanaomponda Lady Jaydee na team yake. 
ILI  kuepuka kusumbuliwa na mahakama , Jide alitumia ‘MwanaFAtuma’ akimlenga MwanaFA.
















Saturday, June 8, 2013

NAIBU WAZIRI WA JINSIA NA WATOTO AIBUA KASHIFA YA RUSHWA YA NGONO KATIKA CHUO KIKUU CHA DODOMA


Suala la uwepo wa rushwa ya ngono kwenye Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) limetinga bungeni.

Suala  hilo Lilijitokeza jana wakati Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu (CCM), alipomaliza kujieleza bungeni akiomba kura kwa wabunge wamchague awe mjumbe kwenye taasisi hiyo.


Baada ya Mbunge huyo kumaliza kujieleza, alisimama Mbunge wa Viti Maalumu, Naibu Waziri wa Jinsia na Watoto, Ummy Ally Mwalimu aliyemhoji atatoa mchango gani katika kupambana na changamoto kwenye chuo hicho, ikiwamo rushwa ya ngono na ukatili wa kijinsia, ili kusaidia watoto wa kike wasome vizuri.


Kabla ya Mangungu kujibu swali hilo, Mbunge wa Chakechake, Mussa Haji Kombo (CUF), aliomba Mwongozo wa Spika kutaka muuliza swali afute kauli yake kwani ni ya udhalilishaji na inaweza kuleta matatizo.


 Hata hivyo, Spika Anne Makinda aliingilia kati na kusema hakuna haja ya kufuta kauli hiyo kwa vile ndiyo hali halisi iliyopo.

Akijibu swali hilo, Mangungu alisema atasaidiana na wenzake kuhakikisha wanakomesha suala hilo.

Katika uchaguzi huo, Mbunge wa Kisarawe, Suleiman Jaffo (CCM) alichaguliwa kuwa mjumbe kwenye Jukwaa la Kibunge la Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC-PF) katika uchaguzi uliofanyika bungeni.

Akitangaza matokeo, Spika Makinda alisema Jaffo aliibuka kidedea baada ya kupata kura 74 na kuwashinda wapinzani wake, Mbunge wa Viti Maalumu, Leticia Nyerere (Chadema) aliyepata kura 56 na Mbunge wa Busanda, Lorensia Bukwimba (CCM) aliyepata kura 51.  Kura 182 zilipigwa na moja kuharibika.
 

Pia Spika Makinda alimtangaza Mangungu mshindi na kuwa mjumbe wa Baraza la Udom kwa kupata kura 137 dhidi ya 38 za mpinzani wake, Mbunge wa Viti Maalumu, Pudenciana Kikwembe (CCM). Kura 177 zilipigwa na mbili kuharibika.
 

Upande wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) aliyeibuka mshindi ni Mbunge wa Babati Vijijini, Jitu Soni (CCM) ambaye hakuwa na mpinzani baada ya Mbunge wa Igunga, Dk Dalaly Kafumu (CCM) kujitoa.
 


Pia Mbunge wa Viti Maalumu, Pindi Chana (CCM) aliibuka kidedea kwa ujumbe wa Baraza la Chuo  Kikuu cha Sayansi na Teknolojia, Mbeya, baada ya kukosa mpinzani.

SAKATA LA HOUSE GIRL ALIYEJINYONGA KISA PENZI LA CHRISTOPHER


 





Mfanyakazi wa ndani aliyejiua kisa mapenzi aitwaye Devotha Sanga leo ameagwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam. 

Marehemu Devotha alijinyonga Juni 4 mwaka huu akiwa nyumbani kwa bosi wake eneo la Kitunda jijini Dar kwa wivu wa mapenzi. 


Devotha alikuwa katika penzi na kijana mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Christopher anayedaiwa kuwa na wapenzi wengi kiasi cha kusababisha marehemu kuchukua uamuzi huo. 

Baada ya kuagwa mwili wa Devotha umesafirishwa kuelekea Njombe kwa mazishi.

MFULULIZO WA VIFO VYA WASANII WAMFANYA DOKII AFUNGUKE KUWA NI MUNGU ANAWAADHIBU


MWIGIZAJI Bongo, Ummy Wenslaus ‘Dokii’ ameibuka na kusema kuwa vifo vya wasanii vimetokea kutokana na kujisahau hivyo Mungu ameamua kuwaadhibu. 

Akiongea na mwandishi wetu katika Viwanja vya Leaders Club, Juni 5, mwaka huu ambapo mwili wa Mangwea ulikuwa ukiagwa, Dokii alisema matukio ya vifo vya wasanii mbalimbali yaliyotokea miaka miwili mfululizo ni pigo kubwa kwani wengi ni vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa kitu ambacho anakiona ni ishara kuwa Mungu anataka kujidhihirisha kwa wasanii.
“Wasanii tulijisahau sana na kuona Mungu hayupo kwani kipindi bado hatujatoka na tunatafuta kutoka kisanaa, tulikuwa tunamuomba kila wakati lakini baada ya kutoka na kuwa mastaa tumemsahau kabisa.

“Hatukumbuki kwenda ibadani tunabaki kuendekeza starehe za dunia tu, hivyo tubadilike kwani Mungu ameanza kujionesha kwetu kwamba yupo,” alisema Dokii.

Tizama Picha ya Diamond enzi hizo kabla hajawa star.

Maisha siku zote nikupambana na mpambanaji hodari siku zote lazima shinde unaweza jua ulipotoka ila usijue uendako. Hivi ndivyoilivyokuwa kwa msanii Diamon.Nani alijua leo Diamond atakuwa hivi.
TIZAMA PICHA HII..hapani Diamond kabla hajawa supasta



SASA TIZAMA PICHA ZA DIAMOND BAADA YA KUWA SUPASTAA 


Kweli pesa sabuni ya roho..all da best Diamond

MTAMBUE KIJANA HANDSOME ZAIDI DUNIANI NA BINTI MZURI ZAIDI DUNIANI.

naitwa Queen Fatima Zohar-Godabari wa Saudi Arabia inasemekana yeye ndiye mwanamke mzuri zaidi duniani kwa mwaka huu wa 2013. Fatima Zohar-Godabari ambaye kwasasa ni malkia wa Saudi Arabia alikuwa akivaa hijabu muda wote kama wafanyavyo wanawake wakiislamu kiasi cha kufunika uso wake masaa yote lakini siku moja alipigwa picha akiwa hajajifunikana usoni napicha hiyo ilipostiwa katika mitandao na magazeti ndipo watu walipodai hakika ni mwanamke mzuri zaidi na kumpelekeakuwahuru kupiga picha pasipo kujifunika usoni.
 Tizama picha zake hapa












Upande mwingine inasemekana kwamba kijana Omar Borkan Al Gala ndiye kijana handsome zaidi kuliko wote duniani kwa mwaka huu wa 2013..Omar Borkan Al Gala ambaye ni mwigizaji napi ni mwanamitindo alifukuzwa huko Saudi Arabia kutokana na mvuto aliokuwa nao.
Tizama Picha zake hapa.






Je Unadhani watu hawa wawili wanastahili sifa hizo???

Friday, June 7, 2013

PICHA ZA MAANDALIZI YA JUKWAA LA KILL MUSIC AWARDS......TUKIO LITARUSHWA LIVE MTANDAONI



Kesho ndio siku yenyewe ambayo wasanii waliotajwa kuwania tuzo za mwaka huu za muziki wa Tanzania, Kilimanjaro Tanzania Music Awards, KTMA watajua hatma yao.

 Tuzo za Kili zitatolewa kesho June 8 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. 

Hizi ni picha za jinsi maandalizi ya jukwaa na ukumbi yalipofikia.
IMG_0728
Mafundi wa TV itakayorusha matangazo live wakiweka sawa mitambo yao
IMG_0730
Sound check
IMG_0734
Hivi ndivyo maandalizi yanavyoendelea
IMG_0739
IMG_0750
Muonekano wa nje ya ukumbi
IMG_0718
Mafundi wakiziweka sawa cranes za camera

MPENZI WA ALBERT NGWEA AKILIA KWA UCHUNGU WAKATI WA MAZISHI



MAJONZI na vilio vilitawala juzi katika zoezi la kuuaga mwili wa marehemu Albert Mangweha ‘Ngwea’ kwenye Viwanja vya Leaders lakini mmoja wa waliotia fora katika kuangua kilio alikuwa dada mmoja mzungu anayedaiwa kuwa alikuwa Mpenzi wa Ngwea aitwaye Misheily. 


Mzungu huyo alionekana akilia kwa uchungu huku akitoa maneno yaliyoashiria kuwa ameumia sana kuondokewa na ‘mtu’ wake huyo ambaye huenda walikuwa na malengo mazuri ya baadaye.

Aidha, kilio alichokuwa akiporomosha binti huyo kiliwafanya watu waliokuwa karibu naye kumsikitikia na kuzidishiwa majonzi kwani ilifika wakati akaishiwa nguvu.


Mwandishi wetu alijaribu kumfuata na kumuomba kuzungumzia juu ya kifo cha Ngwea lakini alikataa na kusema asingeweza kufanya hivyo kufuatia majonzi aliyokuwanayo huku akionekana kutoamini kama jamaa yake huyo ametutoka

MTANGAZAJI WA TIMES FM ( KHADIJA SHAIBU) AJIANIKA "AKIKATA GOGO " CHOONI



MTANGAZAJI wa Kituo cha Redio cha Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ amewashangaza watu baada ya kutundika mtandaoni picha zinazomuonesha akioga bafuni huku nyingine akiwa chooni  akikata  gogo. 


Picha hizo zinapatikana kwenye mtandao wake na hakueleza ilikuwa wapi ila akasema ilikuwa ni siku alipoamua kuitumia wikiendi yake ipasavyo katika hoteli ambayo hakuitaja jina.
 
Baadhi ya watu waliyoziona picha hizo walimponda wakidai eti ni ulimbukeni lakini wapo waliomtetea kwa kusema, ni staili tu ya maisha aliyoamua kuishi.



“Ushamba tu, ndo nini sasa?  alisema mmoja wa wadau huku mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Dick akisema: “Msimuonee wivu mwenzenu, anakula bata zake na nyie hamjakatazwa.”
 
Dida alipoulizwa kuhusu kujianika hivyo alisema, hizo ni ishu zake binafsi na wapenzi wake wanapenda kuona kila anachokifanya, ndiyo maana anawawekea kwenye blogu yake.

BAADHI  YA  MAONI  YA  WATU  KATIKA  BLOG  YAKE 

BABA YAKE DIAMOND YUPO HOI ANAUMWA......DIAMOND HAJAWAHI KANYAGA KUMJULIA HALI


BABA wa msanii Nasibu Abdul ‘Diamond’, Abdul Juma yupo hoi akisumbuliwa na ugonjwa wa miguu.

Kwa mujibu wa chanzo makini, Baba Diamond anasumbuliwa na tatizo la miguu kuvimba hali ambayo imemfanya ashindwe kutembea lakini cha kushangaza mwanaye, Diamond hajaenda kumjulia hali.

“Baba Diamond ni mgonjwa kwa muda mrefu sana lakini Diamond hajawahi kuja kumuona hata siku moja,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kuzinyaka habari hizo, waandishi  wetu walifunga safari mpaka nyumbani kwa mzee huyo, Magomeni-Kagera, jijini Dar ambapo alikiri kuugua kwa muda mrefu na kukosa msaada kutoka kwa Diamond.

“Nasumbuliwa na miguu kwa muda mrefu sana na ninatibiwa katika Hospitali ya Saint Monica, Manzese-Darajani. Diamond ana taarifa za kuumwa kwangu lakini hajawahi kuja kuniona.

“Namshukuru mwanangu Queen Doreen kwa kunijali kwa kila kitu,” alisema baba Diamond.

Thursday, June 6, 2013

KHADIJA KOPA AKIELEKEA UWANJA WA NDEGE JANA KWA AJILI YA MSIBA WA MUMEWE JAFFARI ALLY


Khadija Kopa akilia kwa uchungu mara baada ya kupata taarifa za mumewe kufariki.
Akipewa sapoti wakati akielekea uwanja wa ndege.
Baadhi ya viongozi na wananchi wa mkoa wa Rukwa na Mpanda wakimsindikiza kupanda ndege msanii wa taarab na malkia wa mipasho Tanzania Khadija Omar Kopa kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya kupewa taarifa ya kufiwa na mumewe Jaffari Ally Yussuf aliyefariki dunia jana alfajiri. Bi Khadija Kopa alikuwa akitokea kwenye maadhimnisho ya siku ya Mazingira Duniani kitaifa yaliyoadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa juzi.

TUSIPOCHUKUA HATUA, DAWA ZA KULEVYA ZITAWAMALIZA WANAMICHEZO NA WANAMUZIKI WA TANZANIA

WANAMICHEZO NA WANAMUZIKI WA TANZANIA



DAWA za kulevya ni hatari, ni hatari sana. Maisha ya baadhi ya wasanii na wachezaji yamepotea kutokana na matumizi ya dawa hizo.

Aidha, dawa za kulevya husababisha baadhi ya wasanii na wachezaji kushindwa kuendelea na fani zao.
Orodha ya wasanii waliopoteza maisha kutokana na matumizi ya dawa za kulevya ni ndefu lakini baadhi yao ni Elvis Presley, Whitney Houston, Brenda Fassie wa Afrika Kusini.

Tanzania imepata mshtuko kwamba kimeripotiwa kifo cha msanii kutokana na matumizi ya dawa za kulevya. Tukiwa tunangoja ripoti kamili ya daktari juu ya kifo chake, msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya ‘Bongo Fleva’, Albert Mangwea ‘Mangwair au Ngwea’ anadaiwa kufariki kutokana na dawa za kulevya nchini Afrika Kusini mapema wiki iliyopita.

Habari hizo ziwe kweli au la, Mangwair amefariki na mwili wake ulirejeshwa nchini juzi kwa mazishi yaliyofanyika jana huko Morogoro. Hata hivyo kifo chake, kitoe changamoto kwa wasanii wengine  
akiwemo Ray C aliyeko kwenye kituo cha kujirekebisha kutokana na matumizi ya dawa za kulevya.



DAWA ZA KULEVYA
Hizi ni dawa ambazo zimepigwa marufuku kutumiwa na jamii kutokana na kiwango chake cha athari kwa binadamu. Dawa hizi ambazo miongoni mwake ni bangi, heroin na cocaine, zina athari zaidi katika mwili wa binadamu kuliko faida.

Wasanii wanaotumia dawa za kulevya husukumwa zaidi na tabia ya kuiga ili waweze kufanya maonyesho jukwaani kwa ukakamavu mkubwa.

Wasanii hawa wanaamini wanapotumia dawa hizo zinawasisimua mwili ili wapate uwezo wa kutumbuiza jukwaani kwa muda mrefu bila kuchoka tena bila aibu.

Upande wa wanamichezo hasa soka na riadha, msukumo mkubwa upo katika kuwa na pumzi ya kuweza kucheza soka kwa dakika 90 bila kuchoka na moyo wa ujasiri hata kwenye riadha hali ni hivyo hivyo.

ATHARI ZA DAWA ZA KULEVYA MICHEZONI

Serikali duniani kote zinapiga marufuku matumizi ya dawa za kulevya. Kwa bahati mbaya, dawa hizi hutengenezwa, husafirishwa na hutumiwa kwa kificho japokuwa madhara hujionyesha wazi.

Kwa mujibu wa wataalam, mtu anapotumia dawa za kulevya, moja kwa moja huathiri baadhi ya viungo vya mwili kinyume cha imani ya watumiaji.

Mtumiaji hupata ganzi na kutoka katika hali ya kawaida. Kutokana na ganzi hiyo taarifa hutumwa katika ubongo na ubongo nao hutuma vichocheo katika kiungo hicho na hufanya kazi maradufu.

Jinsi dawa inavyotumiwa kwa wingi ili kurekebisha hali ya ganzi ndivyo nguvu inavyozidi kutengenezwa na hivyo ndivyo vinavyowamaliza wasanii na wanamichezo.

Wataalam wanasema matumizi haya ya dawa za kulevya huufanya mwili wa mtumiaji kuchoka na kukosa hamu ya kula kutokana na seli nyingi mwilini kushindwa kufanya kazi.

Matokeo yake, mwili wa mtu huyo hudhoofu kwa kukosa chakula na hata uwezo wa kutengeneza chembechembe hai za kuulinda mwili na kujikinga dhidi ya magonjwa hupungua, hivyo mwili huruhusu magonjwa ya mara kwa mara.

Hali hii inapotokea uwezo wa msanii au mwanamichezo huonekana umepungua na muda wowote mahala popote anaweza kuchukua maamuzi anayoyajua yeye.

KITU CHA KUFANYA

Masomo ya dini za Kikristo na Kiislamu na elimu maalum ya dawa za kulevya yatumike ili kuwaweka vijana katika misingi mizuri ya maadili na athari za dawa za kulevya.

Hii itasaidia vijana kufahamu kwa undani faida za dawa zilizoidhinishwa na Serikali na athari za dawa zilizopigwa marufuku zikiwemo za kulevya ili kupunguza kwa wimbi la vijana kutumbukia katika matumizi ya dawa za kulevya.

MAKALA HII IMETOLEWA KATIKA GAZETI LA MAWIO NA IMEANDIKWA NA ELIUS KAMBILI

HUU NDO UTENGENEZAJI WA BIKRA FEKI....WANAUME MSIKUBALI KUIBIWA



WANAUME,kuweni makini na Bikra feki...Wanawake wana mbinu nyingi sana za kukuingiza kingi,ndoa imekuwa mtihani kwao,wanafanya kila balaa ili wakuchote akili uingie kingi.

Ukiacha hawa wengne ambao wameamua kuwa Washirikina kwa kwenda kwa Waganga na kupewa dawa za kukukamata,kuna hawa wanawake ambao wametumika kama Bajaj ,wakikuona umekaa dizaini ya muoaji halafu una hela,utapigwa tukio mpaka ushangae.

Atajifanya descent na hajui kitu,atasingizia yeye bikira au amefanya mara moja tu.

Siku ya kufanya Mapenzi kila ukimshika anapiga kelele za kuzuga anaumia,ukishika nywele analia...ukimgusa kifua anapiga yowe kama anakeketwa,ukianza kuzama ndo kabisa,unaweza kudhani uko kwenye Msiba wa Kinyakyusa....

Utasikia taratibu,utafinywa,utapushiwa kama vile ndo unaitoa,kumbe wala.!!!

Mtu mzima unachotwa akili kumbe mwenzio kabla hajajaamekamulia Ndimu,mchanganyiko wa parachichi na tikiti maji,Sabuni ya Kaisiki na Vim ya kuondolea harufu chooni...Ukigusa unahisi bikira kumbe wala,umetegwa...

Hawaruhusu uingize kidole kwenye maandalizi hata kwa dawa utagundua... Dawa yao unakaa na beseni,akizuga unamwagia maji pale juu,litatoka vumbi hujawahi kuona hata kwenye stoo yenu ya kuku wa mayai...

JIHADHARI  na hizi bikira za makuti!

SETH  

DIVA WA CLOUDS FM NAYE ATOA PICHA YA NUSU UCHI ILI KUMTEKA PREZZO ANAYEONEKANA KUHAMISHIA PENZI KWA HUDDAH



Baada ya huddah kuweka picha yake akiwa na prezzo na kuzua gumzo mitandaoni, Diva  wa  clouds  fm ameamua kuweka picha yake yaNUSU UCHI   ili kupotezea  Aibu  hiyo..

"Love at the first sight  imekwishaimekwisha."....
Ulimpiga  KIBUTI   mbunge  mh. JEPESI , tena   kwa  mbwembwe, vijembe  na  kejeli  kibao  mtandaoni......

Leo  hii  jamii  inashuhudia  unavyoumbuka.Penzi  la  Huddah  na  Prezzo  lilikuwa  wazi  na  la  vitendo.....

Siku  moja  kabla  ya  kutolewa  katika  jumba  la  big brother, Huudah  aliweka  wazi  juu  ya  uhusiano  wake  na  Prezzo  huku akielezea  jinsi  alivyo  miss  kushikwa  shikwa...!!
Prezzo  na  mpenzi  wake....


Nani  alikurupuka  kati  yake  na  wewe???
Si  mbaya  sana, ENDELEA  KUWEKA  PICHA  ZA  UCHI, PENGINE  ATAHAMISHIA  PENZI  KWAKO