Thursday, March 21, 2013

Much Better - Leo Leo (Official Video) HD

Much Better - Leo Leo (Official Video) HD

THE DREAM VIDEOZ



D.O.P Raymond Kasoga from The Dream Videoz making Final Touch on the BSS 2012 MENINA the music Called Dream Tonight soon on ur wall. — 

WANIGERIA HATARI, UNAAMBIWA HAYA NI SEHEMU YA MAGARI YA KIFAHARI YA DUNIA YALIYOONEKANA ABUJA


.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

KWA NINI MAMISS WA TANZANIA HAWAOLEWI NA BADALA YAKE HUTUMIWA NA KUACHWA



WAKATI mashindano ya u-miss yanaanzishwa Bongo, wazazi wengi walikuwa wazito kuwaruhusu watoto wao kushiriki wakiamini kwamba ni uhuni. Kadiri miaka ilivyozidi kusonga mbele, taratibu walianza kuelewa kuwa siyo uhuni na wakawaruhusu watoto wao kwa kuyaona yana tija.

Matunda ya warembo yalionekana, lakini kumekuwa na dosari kwao, licha ya mafanikio makubwa wanayoyapata, asilimia kubwa hawaolewi. Swali la kujiuliza hapa ni kwa nini hawaoleki, why?


Mwanasaikolojia mmoja aliwahi kusema, sababu inayosababisha  warembo hawa wasiolewe au hata wakiolewa wasidumu kwenye ndoa ni jinsi wenyewe walivyojijenga akilini kuwa ni watu maarufu, wazuri hivyo wamekuwa wakichagua wanaume na kuishia kutumiwa, wakija kushtuka umri unakuwa umewatupa.

LWAKATARE ATUPWA GEREZANI HADI APRIL 3 BAADA YA KUFUNGULIWA MASHITAKA UPYA


LWAKATARE ATUPWA GEREZANI HADI APRIL 3 BAADA YA KUFUNGULIWA MASHITAKA UPYA



MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam imewafutia kesi ya makosa ya ugaidi  Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare  na Ludovick Joseph baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka( DPP), Dk Eliezer Feleshi kuwasilisha hati ya kuwafutia kesi hiyo washitakiwa kwa sababu hana haja ya kuendelea nayo.

Sambamba na hilo, DPP ilimfungulia kesi ya makosa ya ugaidi  upya Lwakatare na Ludovick ambapo kesi hiyo mpya namba  Na.6/2013 ambapo imepangiwa kwa hakimu mpya Aloyce Katemana.

Katika kesi ya ugaidi Na.37/2013 iliyofunguliwa na Jamhuri dhidi ya Lwakatare na wenzake Machi 18 mwaka huu, ambayo ilifutwa saa tatu asubuhi na ambayo ilikuwa imekuja kwa ajili ya Hakimu Mkazi, Emilius Mchauru kuitolea uamuzi wa ama wa kuwapatia dhamana washitakiwa au la, hakimu Mchauru alijikuta akishindwa kutoa uamuzi wake kwa sababu  mawakili viongozi wa serikali Ponsian Lukosi, Prudence Rweyongeza na Peter Mahugo waliwasilisha  hati hiyo ya DPP chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002, ambapo kifungu hicho kina mpa mamlaka DPP, kuifuta kesi yoyote ya jinai muda wowote kabla ya haijatolewa hukumu na uamuzi huo wa DPP haujahojiwa na mtu yoyote.

“Kwa kuwa kesi hii Na.37/2013 ilifunguliwa na upande wa jamhuri MAchi 18 mwaka huu, na leo kesi hii ilikuja kwa ajili ya mahakama kutolea uamuzi wa maombi ya washitakiwa kupatiwa dhamana au la  pamoja na maombi mengine…mahakama hii inasema haitaweza kutoa uamuzi wake kwa sababu DPP amewasilisha hati ya kutotaka kuendelea kuwashitaki washitakiwa  na hivyo mahakama hii inawafutia kesi washitakiwa wote”alisema hakimu Mchauru.

Baada ya hakimu Mchauru kuwafutia kesi, askari kanzu waliwakamata tena washitakiwa hao na kuwaweka chini ya ulinzi wa gari la polisi na ilipofika saa 4:20 asubuhi, washitakiwa hao wakiwa chini ya ulinzi mkali wa wana usalama waliingizwa tena katika ukumbi namba mbili wa mahakama  hiyo mbele ya hakimu mkazi mwingine Aloyce Katemana.

Mawakili Wakuu wa Serikal, Ponsian Lukosi, Prudence Rweyongeza na Wakili Mwanadamizi wa Serikali Peter Mahugo walidai kuwa kesi hiyo nimpya na imepewa Na.6 ya maka huu, ambapo washitakiwa ni Lwakatare na Ludovick wanaotetewa na mawakili wa kujitegemea Profesa Abdallah Safari na Peter Kibatara na kwamba hati hiyo mashitaka ina jumla ya  mashitaka manne ambapo shitaka la kwanza linaangukia kwenye Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002 na makosa matatu yote yanaangukia kwenye Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya mwaka 2002.

 Wakili Rweyongeza alililata kosa la kwanza ambalo linawakabili washitakiwa wote kuwa ni la kula njama kutenda kosa la jinai kinyume na kifungu cha 284  cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002 , na kwamba mnamo Desemba 28 mwaka jana, huko Kimara King’ong’o  Stopover, wote kwa pamoja walitenda kosa hilo kwa kutaka kutumia  sumu kwa lengo la kumdhuru  Denis Msaki  ambaye ni Mhariri wa habari wa Gazeti la Mwananchi ambalo ni kinyume na kifungu cha 227 cha sheria hiyo.

Wakili Rweyongeza alilitaja  kosa la pili kuwa ni la kula njama  ambalo pia ni kwaajili ya washitakiwa wote  ambalo ni kinyume na kifungu cha 24(2) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi Na.21 ya mwaka 2002, ambapo washitakiwa hao walitenda kosa la ugaidi la  kutaka kumteka Msaki  kinyume na kifungu  cha 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya mwaka 2002.

Shitaka la tatu ni la washitakiwa wote ambapo wanashitakiwa kwa kosa la  kupanga kufanya makosa ya ugaidi  kinyume na kifungu cha 59(a) cha Sheria ya Kuzuia ugaidi kwamba Desemba 28 mwaka jana,walishiriki katika mkutano wa kupanga kufanya vitendo vya kumteka nyaraka Msaki  kinyume na kifungu 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi.

Shitaka la nne, Rweyongeza alidai linamkabili Lwakatare peke yake  ni kuwezesha kutendeka kwa kosa la ugaidi kinyume na kifungu cha 23(a) cha sheria ya kuzuia ugaidi , kwamba Desemba 28 mwaka jana, Lwakatare akiwa ni mmiliki nyumba hiyo ilipo Kimaraka King’ong’o  kwa makusudi  aliliruhusu  kufanyika kwa kikao hicho baina yake na Ludovick  cha kutenda kosa la ugaidi la kutaka kumteka nyara Msaki hata hivyo walikanusha mashitaka hayo.

Hata hivyo  Hakimu Katemana alisema washitakiwa hao hawatakiwi kujibu chochote kwasababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na akaiarisha kesi hiyo hadi Aprili 3 mwaka huu, itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

Wakili Kibatala aliomba mahakama isikilize ombi lake alilokuwa akitaka kuliwasilisha, lakini Hakimu Katemana alisema yeye ndiye kiongozi na mawakili wa utetezi, Jamhuri wapo chini yake na akamweleza Kibatala mahakama ni mhimili unaongozwa kwa taratibu zake na nilazima Kibatala azifuate, hivyo, kwa kuwa yeye hakimu ana majukumu mengine, leo hayupo tayari kusikiliza ombi la Kibatala wala ombi la upande wa Jamhuri (lilokuwa linaomba mahakama imruhusu Ludovick aendelee kushikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya hatua  zaidi za kipelelezi,) na kuamuru washitakiwa wapelekwe gerezani. 
Itakumbukwa kuwa Machi 18 mwaka huu, Hakimu Mchauri alitoa fursa kwa washitakiwa ya kukubali au kukanusha mashitaka licha ya Hakimu wa Mahakama hiyo ya Hakimu Mkazi kutokuwa na ruhusa ya kutoa fursa hiyo kulingana na makosa yanayowakabili  watuhumiwa na kwa mujibu wa sheria za nchi.  Mahakama Kuu pekee ndiyo yenye mamlaka ya kusikiliza kesi za  makosa ya tuhuma za ugaidi.

Baada ya kesi hiyo kuairishwa wafuasi wa CHADEMA na watu wengine wakiwa wamevalia sare walipaza sauti na kusema ‘Peoples Power… hakuna kulala hadi kwanza walale wao’.

Hali iliyosababisha wanausalama waliokuwa wamevalia sare na wale waliovalia kiraia waliokuwa ndani ya kumbi wa kesi ilipokuwa ikiendeshewa kuwataka watu wote watoke ndani ya ukumbi huo haraka ili waweze kuwapitisha washitakiwa, amri ambayo wafuasi hao waliitii bila shuruti.

Msafara wa magari nane ukiongozwa na magari ya jeshi la magereza, polisi waliondoka ndani ya viwanja hivyo kwa ajili ya kuwapeleka watuhumiwa katika gereza la Keko , huku askari wa kikosi cha mbwa wakiwa  bado katika eneo la mahakama hiyo kwa ajili ya kuimarisha ulinzi. Hata hivyo, hali ilikuwa ni shwari kwa sababu hakukuwepo na vitendo vya uvunjifu wa amani kwani wafuasi wa CHADEMA waliondoka mahakamani hapo kwa utulivu wa hali ya juu huku wengine wakiangua vilio kwa uchungu.

Mbwa waliokuwepo wakiimarisha ulinzi eneo hilo ni Kino, Pd Kambi Simba, Giro, Pd Roja, Pd Ivo, Pd Undra, Pd Bobi ambao wamepata mafunzo ya kuimarisha ulinzi kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Lebanon.

Akizungumza nje ya viwanja vya mahakama  baada ya kesi kuahirishwa, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alisema kwanza asingependa kuingilia mtiririko wa mahakama na kuwataka waandishi wa habari wamuhoji wakili wa washitakiwa. 


Akasema wao wanafanyakazi za mageuzi kwa ajili ya kuwatetea raia wanyonge na maskini na kwamba kilichompata Lwakatare siyo geni, bali ni mtiririko wa mabavu ya dola dhidi ya wanamageuzi.

MSANII MATUMAINI ANAOMBA ASAIDIWE....KWA SIKU ANAMEZA VIDONGE 39





Mchekeshaji na muigizaji wa Tanzania Tumaini Martin ‘Matumaini’ amevunja ukimya kuelezea maendeleo ya afya yake akidai kusumbuliwa na maumivu makali ya miguu kwasasa.

Akiongea na BK Cop leo Matumaini amesema kuwa anaendelea kutumia dozi ingawa hali ya afya yake bado si shwari kutokana na kugulia maumivu makali ya miguu hali inayomfanya ashindwe kutembea.

Msanii huyo ameeleza kuwa kwa siku moja huwa anameza vidonge zaidi ya 39 lakini hapati lishe nzuri kwababu ya kutokuwa na pesa na kujinunulia chakula. 

Aidha amedai kuwa wakati alipokuwa msumbiji alipata misaada ya kifedha kutoka kwa wasanii mbalimbali lakini hasaidiwi tena tangu alipofika Tanzania.
‘Niliomba msaada kwenye magazeti ambapo niliacha namba zangu za tigo pesa lakini meseji nyingi nazopokea ni za pole; hata hivyo kuna watu wanadai wametuma kwa namba ya Michael Sangu (Mkt Chama cha waigizaji) ambayo alitoa gazetini lakini mimi sikuwahi kuonana tena na Michael tangu aliponililipia matibabu wakati natoka hospitali’.Alisema Matumaini

Mnamo Februari 9 mwaka huu Matumaini aliruhusiwa kutoka hospitali ya Amana jijini Dar es salaam alipokuwa amelazwa kwa siku tatu tatizo kubwa likiwa ni miguu na alitakiwa kurudi tena hospitali baada ya kumaliza dozi aliyoandikiwa na daktari.

Awali Matumaini alikwenda kuishi nchini msumbiji na kuripotiwa kusumbuliwa na maradhi, lakini alishindwa kutibiwa akiwa huko ambako Naibu Waziri wa Habari vijana na utamaduni na michezo Bw Amos Makalla akishirikiana na baadhi ya wasanii alichukua jukumu la kutoa nauli ya kumrudisha nchini.

MAGAZETI 14 YA LEO MARCH 20 2013 NA STORI ZAKE KUBWA YAKO HAPA



.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

BREAKING NEWS YA MTU KUPIGWA RISASI AKIWA KWENYE FOLENI KINONDONI 11:08 AM No comments


Mtu Mmoja Kauawa Akiwa Na Gari Lake Katika Foleni Mitaa Ya Kinondoni Na Watu Wasiojulikana Walikua Wawili Kwenye Pikipiki, Ilitokea Ghafla Walimiminia Risasi Mtu Huyu Wakatoweka Ilikua Mida Ya Saa Moja Jioni Hii.. Habari Kamili Endelea Kutembelea Blog Hii Kwa Habari Zaidi...


UPDATE: DEREVA ALIYEMGONGA TRAFIKI JANA AMEKAMATWA





Taarifa iliyotufikia inaeleza kuwa  yule Dereva aliyemgonga askari polisi wa usalama barabarani WP 2492 CPL-Elikiza na kutokomea, amekamatwa jana usiku masaa kadhaa baada ya kupoteza uhai wa askari huyo maeneo ya Bamaga mapema jana mchana.

kwa Mujibu wa kamanda wa Polisi kikosi cha Usalama barabarani nchini,Kamanda Mohamed  Mpinga amesema leo kuwa gari lilohusika kwenye ajali hiyo limepatikana likiwa limefichwa maeneo ya Tabata dampo jijini Dar.

Kamanda Mpiga ametoa taarifa hiyo mbele ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete nyumbani kwa Marehemu,hukoUnunio,kaskazaini mwa jiji la Dar. Rais Kikwete alifika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu ambaye ameacha  Mume na watoto watatu.

Habari kamili zitawajia baadae. My izac


"UHABA WA WANAUME UMEWAFANYA MASTAA WA KIKE WATOE PENZI KWA WATOTO WADOGO"...BABY MADAHA





MSANII wa nyimbo za muziki wa bongo fleva  anayefahamika kwa jina la  Baby Madaha amewashukia baadhi ya wasanii wa kike nchini wanaojihusisha na maswala ya ngono na wanaume wenye umri mdogo maarufu kwa jina la 'Kijibwa' kuwa ni hali ya kukata tamaa na ushamba ndio unaochangia kufanya kitendo hiko

Akizungumza jijini Dar es Salaam Msanii huyo alisema kuwa anashangazwa na baadhi ya wasanii hususani wa kike kujihusisha na maswala ya ngono na wavulana wenye umri mdogo huku wakitumia jina la 'kijibwa' kwa ajili ya kukidhi matakwa yao ya kingono

Alieleza kuwa hali ya kukata tamaa ndio chanzo kinachopelekea baadhi ya wasanii hao kujihusisha na maswala ya ngono na vijana wadogo huku wakijipa moyo kuwa wanatafuta faraja wakiwa na vijana hao

"Unajua hao wasichana wanaonekana kukata tamaa kwa kukosa mwanaume wanaolingana kiumri ndio maana ajimchukua mtoto mdogo na kumuhudumia kila kitu na ndipo hapo jina la 'kijibwa' linapotumika kwa kumfananisha mvulana huyo na mbwa unayemuudumia kila kitu huku kazi yake kubwa inakuwa ni kumlinda tu "  aliongezea kuwa

"Kwa sababu mvulana huyo anapewa kila kitu ikiwemo kununuliwa hadi nguo yeye anakuwa na kazi moja tu hivyo hapo hamna mapenzi zaidi ya utumwa na kumsababisha mvulana huyo kukosa uhuru wa kuwa na maamuzi ya mambo yake binafsi" alisema Madaha

Kutokana na hicho kitendo Madaha alikiita ni ushamba kwa kuwa na mahusiano ambayo hayana msingi wowote ule na si kwa ajili ya mtazamo wa maisha hivyo mahusiano hayo hayaendana na mazingira ya nchi na kusababisha kudharaulika kwenye jamii inayomzunguka

Alitoa wito kwa wasichana hao wanaojihusisha na maswala hayo kuwa wanachotakiwa ni kujiamini na kujipanga upya kwa ajili ya kupambana na maisha na kutoyaogopa maisha hivyo wanachotakiwa ni kujipanga upya

Lets Meet All Africans Stars Online on www.africanstube.com (playlist)