Monday, May 20, 2013

NISHA WA BONGO MOVIE AWATALEKEZA WATOTO YATIMA




MSANII wa maigizo, Salma Jabu ‘Nisha,’ amedaiwa kuwatosa watoto yatima waliokuwa wakimsubiri baada ya kuweka ahadi kuwa angekwenda kuwatembelea na kuwapa msaada. 


Tukio hilo lilitokea hivi karibuni ambapo Nisha aliahidi kwenda kuwapa msaada watoto yatima wa kituo cha Hisan Orphan Center kilichopo maeneo ya Mbagala Charambe, jijini Dar lakini ulipofika muda, hakutokea.
 


Rafiki wa karibu na staa huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake, alipoulizwa kulikoni alikiri kutotoa taarifa kwa uongozi wa kituo hicho cha watoto yatima na kudai walikuwa na dharura siku hiyo.

“Kuna tatizo lilitokea ikabidi tughairi. Tunaomba radhi kwa kuwafanya wasubiri sana ila niwaambie kuwa mpango wa Nisha kuwatembelea watoto yatima bado upo palepale,” alisema

MADAM RITA WA BONGO STAR SEARCH ANATIA HURUMA...




Kilichompata Madam Rita kinasikitisha! Ndivyo unavyoweza kusema ukibahatika kumuona the big boss wa Benchmark Production inayoratibu Shindano la Bongo Star SearchRita Poulsen ‘Madam’ anayetembelea magongo baada ya kupata ajali mbaya ya gari.

Akizungumza na mwandishi wetu baada ya kuwa kimya muda mrefu ikielezwa kuwa alipata ajali hiyo kitambo, Madam Rita alisema kuwa kwanza kabisa anamshukuru Mungu kwani anaamini kila kitu kinachotokea chini ya jua kina sababu yake na hata alipopata ajali hiyo alimshukuru kwa kutoka salama.

 Kabla ya ajali


Madam Rita aliendelea kueleza kuwa ajali hiyo aliipata katikati ya Jiji la Dar  na kusababisha kuvunjika kwa kifundo ‘enka’ cha mguu wa kulia hivyo kumsababishia kutembelea magongo baada ya hospitali kumuwekea ‘hogo’.

“Namshukuru Mungu kwanza kwa kunitoa salama katika ile ajali japokuwa sijapona vizuri,” alisema Madam Rita.

Mkurugenzi huyo aliendelea kueleza kuwa alipopata ajali hiyo alikimbizwa katika Hospitali ya Muhimbili kwenye Taasisi ya Mifupa ya Moi lakini hali ilipokuwa kuwa mbaya alihamia katika hospitali moja ya Kichina ambapo kwa sasa amepata nafuu.