Wednesday, April 10, 2013

"MIMI NDIYE NILIYEWAPELEKEA POLISI ILE VIDEO YA LWAKATARE"...MWIGULU NCHEMBA




HATIMAYE Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Mwigulu Nchemba, amekiri kuhusika na video inayomwonesha Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare.

Nchemba amekuwa akitajwa na viongozi wa CHADEMA kuwa anahusika kutengeneza video hiyo, kwa kuwa aliwahi kutamba wakati akihojiwa na kituo kimoja cha televisheni kuwa anayo video inayowaonesha viongozi wa chama hicho wakipanga mauaji.

Hata hivyo, tangu Nchemba atoe kauli hiyo Januari mwaka huu, Jeshi la Polisi lilikaa kimya hadi Machi 12 lilipomkamata na kumhoji Lwakatare, siku moja baada ya video hiyo kuwekwa kwenye mtandao wa You tube na mtu anayejiita ‘Bukoba Boy’.

Akizungumza na gazeti hili kwa simu jana, Nchemba alikiri kuwa ndiye aliyeipeleka video ya Lwakatare polisi na kwamba alifanya hivyo baada ya kuripoti kuandikiwa ujumbe wa simu wa kutishiwa maisha na baadhi ya viongozi wa CHADEMA.

“Niliwapelekea mimi hiyo video polisi na wakati nasema kwenye televisheni nilikuwa tayari nimewapa. Na pale nilisema makusudi baada ya Zitto Kabwe kudai kuwa mwaka jana kulitokea mauaji mengi, ndipo nikataka kumuonesha kuwa chama chake kinahusika na mikakati hiyo,” alisema. Alipoulizwa aliipataje video hiyo na kwanini hajahojiwa polisi ili kutoa uthibitisho wa uhalali wake, Nchemba alisema: “Kuna msamaria mwema aliniletea.”

Nchemba alipobanwa ana uhakika gani kama video hiyo ina ukweli, alijibu kuwa: “Ile huhitaji akili kubwa kutambua uhalisia wake. Suala la Lwakatare CHADEMA wakubali tu na wajitokeze hadharani kwenye makanisa na misikiti, watubu na kuomba radhi kwa umma.”

Ndg wana JF sijashiriki kurekodi mkanda wa video unaomwonesha kiongoz mwandamizi wa CHADEMA akipanga mauaji ya mhariri wa gazeti. Mambo yako dhahiri kwani video inaonesha pale ni nyumbani kwake. Pili sikumtuma mtu akarekodi mkanda huo. Niliwahi kusema nina mkanda haina maana kuwa nilituma mtu.

Mikanda niliyokuwa nayo nilipewa na kiongozi wa CHADEMA anayechukizwa na vitendo hivyo vya kinyama. Ndugu zangu wa CHADEMA, najua nawakera na hampendi kusikia haya nawashauri msihangaikie habari ya Mwigulu ameshiriki bali hangaikieni kwanini kiongozi mwandamizi anafanya hayo pia kwanini anafanya kizembe mpaka mkanda unanaswa na tatu mjiulize. Kwangu mimi sioni kama kupata mkanda huo kwa kupewa au kwa hela ni dhambi kubwa kuliko ya kupanga mauaji.

Niwambie tu mkanda niliopewa sikuweka hata nukta na nilikabidhi vyombo vya usalama.

--- Mwigulu Nchemba via JF - Sijashiriki kurekodi mkanda wa video unaomwonesha ndg Lwakatare
Hata hivyo katika kile kinachoweza kuongeza mashaka ya Nchemba kuhusishwa kutengeneza video hiyo, alikwenda mbali zaidi akitoa hata siri za polisi, akisimulia maelezo aliyodai kuwa ndiyo yalitolewa na Lwakatare wakati akihojiwa na polisi.

“Pale video inaonesha ni nyumbani kwake, tena jikoni na hilo amekiri katika maelezo yake polisi. Pia amekubali kuwa
siku hiyo alipiga chafya kama inavyoonekana. Sasa wewe mwandishi unatetea nini wakati yeye amekiri polisi kila kitu kilichomo mle,” alisema.

Maelezo ya Nchemba yalionekana kumtia hofu mmoja wa mawakili wa Lwakatare, ambaye alikuwepo wakati wote wa mahojiano polisi, Nyaronyo Kicheere, akidai kuwa ni wazi jeshi hilo linafanya kazi ya propaganda za CCM.

“Nchemba hakuwepo wakati Lwakatare akihojiwa na hata baadhi ya wanasheria katika kesi yake ya ugaidi inayomkabili hawajui alichokisema polisi, sasa huyo amepata wapi siri za polisi kama si mchezo unachezwa?” alihoji.

Kuhusu mahusiano yake na mshtakiwa wa pili katika kesi ya Lwakatare, Ludovick Joseph, ambaye anadaiwa na baadhi ya watu kuwa ndiye aliyerekodi video hiyo, Nchemba alisema walifahamiana kupitia mtandao wa kijamii wa facebook.

Alipotakiwa kufafanua ukaribu wao hadi kufikia hatua ya kumtumia fedha kwa njia ya M-Pesa kupitia simu yake, Nchemba alisema: “Mimi nilimtumia kama ninavyowapa watu wengine hata wa CHADEMA.

“Mimi sijui kama Ludovick ndiye alirekodi video hiyo, wala sikuwahi kumtuma kufanya hivyo na fedha niliyomtumia si kwamba nilikuwa nikimlipa ujira. Kwani unaweza kumpa mtu sh 50,000 tu kwa kazi hiyo?” alihoji.

Tanzania Daima lilipotaka kufahamu kama anahusika kushirikiana na vyombo vya dola kuwarubuni baadhi ya vijana wa Makao Makuu CHADEMA kwa fedha ili watumike kutoa ushahidi wa kumwangamiza Lwakatare mahakamani, Nchemba alisema: “CHADEMA haijawahi kuongoza serikali, hivyo hawajui mikono ya serikali.”

Alipotakiwa kufafanua kikao baina yake na vijana hao kilichofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff ya jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi uliopita na kisha kuwatumia fedha kwa njia ya M-Pesa, Nchemba aling’aka na kuuliza: “Hiyo Hoteli ya Sea Cliff iko wapi? Maana sipajui na sijawahi kufika.”

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Mkurugenzi wa Mambo ya Katiba wa CHADEMA, Tundu Lissu, alifichua njama zinazofanywa ili kutengeneza ushahidi wa uongo kwa ajili ya kuutumia katika kesi ya ugaidi inayomkabili Wilfred Lwakatare.  Lissu alidai kuwa njama hizo zinafanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama na ujasusi ili kutumia ushahidi huo mahakamani dhidi ya Lwakatare.

Alisema kuna baadhi ya vijana wa CHADEMA wa Idara ya Ulinzi na Usalama wanaopewa fedha na kuahidiwa kufundishwa namna ya kuzungumza katika kesi hiyo ya Lwakatare.

Lissu alisema kuna baadhi ya vijana wakiongozwa na Saumu Mulugu, ambaye alifukuzwa kazi CHADEMA mwanzoni mwa mwaka jana, wamepokea fedha kutoka kwa kigogo mmoja wa CCM (jina linahifadhiwa) ili kufanikisha mpango huo.
Lissu alisema hadi sasa vijana hao wameshapewa sh 400,000 ili wakubali kwenda kufundishwa jinsi ya kuzungumza mahakamani kuwa CHADEMA ni chama cha kigaidi, kwamba Lwakatare alipanga mikakati ya kigaidi.

“Awali walipewa sh 400,000, wakapewa tena sh 300,000, pia wakapewa sh 35,000 mara mbili. Na fedha zote hizi walikuwa wanapewa kwa njia ya M-Pesa,” alisema Lissu.

Alidai kuwa Saumu ndiye anayeratibu mpango wote kati ya Jeshi la Polisi na vijana hao wa CHADEMA kwa kuwarubuni kwa fedha. Alisema vikao baina ya vijana hao wa CHADEMA na Saumu vimewahi kufanyika mara kadhaa katika moja ya hoteli maarufu nchini juu ya mambo ya kwenda kuzungumza kwenye vyombo vya habari au mahakamani kwenye kesi ya Lwakatare.

Siku moja baada ya madai ya Lissu, gazeti hili lilimnasa Saumu akiwa anawasiliana na wenzake, huku akiwatuhumu baadhi yao kuwa ndio waliovujisha siri kwa Lissu. Vilevile alionekana akiwasiliana na kigogo mmoja wa CCM ambaye alikuwa akimwita ‘mkuu’ huku akimsomea baadhi ya taarifa zilizoandikwa magazetini jana yake kuhusu kuvuja kwa siri zao. Saumu akiwa katika grosari karibu na baa maarufu kwa jina la Kwa Kimaro, jirani na eneo la Benki Kuu ya Damu Salama, Mchikichini jijini Dar es Salaam, alisikika akiwalalamikia wenzake kwa kumsaliti na kuvujisha mkakati wao kwa Lissu.

“Kwanini mmelikisha siri zetu kwa Lissu hadi amejua tulikutana katika hoteli ya kifahari na Mwigu…? Sasa nitawaonesha, maana laki tano zenu ninazo mimi. Siwapi bali nitazitumia kujilinda,” alitamba.

Saumu ambaye alikuwa akizungumza kwa sauti kubwa ya ghadhabu kupitia simu, aling’aka: “Nyie kwanini mmeniuza kwenye ishu ambayo tumeipanga wote?”

Baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa ‘mkuu wake’ aliendelea kupiga simu akimlalamikia mtu ambaye hakumtaja, kuwa alikuwa amezima simu yake makusudi kwa kuwa ndiye alivujisha siri zao kwa CHADEMA.

“Mimi sitakubali na nimehakikishiwa na bosi wetu kuwa huyo aliyetusaliti tutatumia wale askari kumwekea hata unga. Haiwezekani fedha tumepokea za kwanza, za pili na tatu kwanini tuuzane dakika za mwisho?” alidai Saumu huku akiendelea kugida bia yake.

Huku akihaha huku na kule, Saumu alikuwa akiwapigia simu baadhi ya madereva wa CHADEMA makao makuu na kuwaomba simu za baadhi ya watu, na hata wakati mwingine kuwafokea akidai ndio waliofichua siri hiyo.

Hata hivyo, baada ya kutilia shaka nyendo za chanzo chetu kudaka siri zake, ghafla alitokomea na kuzima simu zake mara moja kwani hata alipotafutwa baadaye hakupatikana hadi leo.

Polisi wafanya unyama

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi nchini limemkamata kada wa CHADEMA mjini Bukoba, Evodius Justinian na kumshikilia kwa siku kadhaa kisha kumsafirisha hadi jijini Dar es Salaam huku akipewa mateso makali ya kulazimishwa akubali kutengeneza video ya Lwakatare.

Justinian (30), ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA) mjini Bukoba, alikamatwa Jumanne ya wiki iliyopita akidaiwa kukabiliwa na makosa ya jinai.

Alishikiliwa kwa siku mbili mfululizo kabla ya kumsafirisha kwenda wilayani Igunga, Tabora ambako alidaiwa kuwa alitenda makosa hayo ya jinai lakini alifichwa jijini Mwanza.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Philip Kalangi hakutaka kulizungumzia kwa undani suala hilo lakini aligusia kuwa alikuwa anakabiliwa na mashitaka ya kushambulia na kujeruhi mtu huko wilayani Igunga.

Hata hivyo, kada huyo alisafirishwa hadi uwanja wa ndege wa jijini hapa juzi, lakini akanyang’anywa simu na kukatazwa kuzungumza na ndugu zake.

Taarifa za kada huyo kuletwa jijini hapa zilikuwa za kificho kwani wakili wake Nyaronyo Kicheere akiongozana na ndugu wa mtuhumiwa huyo walifika Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na kuelezwa kuwa amepelekwa makao makuu.

Walipofika makao makuu kumwona na kumpatia chakula, polisi walisema hawana mtu kama huyo, hivyo wakarudi tena Kanda Maalumu walipohakikishiwa kuwa yuko makao makuu.

Akizungumza mbele ya wakili wake, Kicheere, mtuhumiwa huyo alieleza unyama aliofanyiwa na jeshi hilo wakati wote wa mahojiano mkoani Mwanza na jijini hapa.

Katika maelezo yake yaliyoshuhudiwa na Ofisa wa Polisi Makao Makuu, Advocate Nyombi, Justinian alisema kuwa baada ya kutolewa mjini Bukoba kwa siri bila ndugu zake kujua, alipelekwa jijini Mwanza na kuhojiwa bila kuruhusiwa kuonana na wakili wake.

Alieleza kuwa wakati wote wa mahojiano hayo alikuwa akilazimishwa kukiri kurekodi video ya Lwakatare inayoonesha mikakati ya ugaidi.

Alisema alisafirishwa kwa siri kwa ndege hadi Dar es Salaam, akapelekwa chooni na kumpiga, kutishiwa na kuteswa kwa nyaya za umeme na kumnyima fursa ya kupewa chakula.

Justinian ambaye anaendelea kushikiliwa na polisi, anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo.

Kabla ya maelezo hayo, Kicheere akiwa na Uloleulole Juma Athumani, ambaye ni ndugu wa Justinian, alijitambulisha kwa Nyombi akimweleza kuwa walikuja kuonana na mteja wake pamoja na kumletea chakula.

Hata hivyo, Nyombi alisema hakuwa na habari za kukamatwa kwa kada huyo na kwamba angekuwa amelimaliza mapema suala hilo.

Kada huyo alisimulia unyama aliofanyiwa akisema: “Nimepigwa na polisi nikiwa Mwanza, nikiwa chooni Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam wakati naletwa huku, polisi wakaniambia mimi ni mtu hatari sana, niseme nilifanya nini Igunga.

“Nikiwa Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam niliomba kwenda chooni, waliingia pamoja na mimi wakanipiga sana, nimeshaandika maelezo kwa kulazimishwa, niliomba kuwa na wakili wakanikatalia,” alisema.

Aliongeza kuwa akiwa Dar es Salaam alihojiwa aseme ukweli kuhusu video ya Lwakatare. Akawajibu kuwa ilifanyiwa uhariri na Ludovick lakini akapigwa makofi na askari wakaagiza nyaya za umeme za kutesea.

“Waliposimama kuleta nyaya za umeme, kwa kuhofia mateso ya umeme nikasema hii video ni yangu. Ninaumwa sana tumbo la kuhara damu, natumia dawa nilizonunuliwa na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mkoa wa Kagera tarehe 4 Aprili,” alisema.

Justinian aliongeza kuwa hakula chakula chochote cha polisi kwa kuwa hawaamini, ila kuhara kulipozidi alikubali kula chakula chao.

Wakili Kicheere alisema ni makosa makubwa sana kumtesa mtu kwa kipigo na vitisho vya umeme na kwamba hayakubaliki hata mahakamani.

“Polisi hawakutaka nionane naye kwa makusudi hadi walipomaliza kumhoji na kumtesa ndipo wakaniruhusu,” alisema.

AKATI RAGE WA SIMBA AKIJIANDAA KUIPELEKA MAHAKAMANI AZAM FC, CLUB HIYO IMEMJIBU NA KUMWAMBIA KUWA ITAMPATIA HADI NAULI YA KUMFIKISHA MAHAKAMANI

W

KLABU ya Azam FC imetoa 'Go Ahead' kwa Simba kwenda mahakamani kwa madai ya fidia ya kuchafuliwa.

Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage alikaririwa mjini Dodoma alipokwenda kuhudhuria vikao vya bunge kuwa klabu yake inaandaa barua ya kuidai fidia ya Sh1.5 Bilioni.

Ni kutokana na klabu ya Azam kuwafungia wachezaji wanne kwa tuhuma za kupokea rushwa ambayo ni  Sh7 milioni ili wapange matokeo wakati wa mechi ya Simba na Azam FC Oktoba 26, mwaka jana ikiwa ni siku moja kabla ya mchezo huo.

Kauli ya Rage inafuatia taarifa iliyotolewa Jumatatu wiki hii na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru) ikieleza kushindwa kuthibitisha tuhuma za kupokea rushwa zilizokuwa ziwawakabili wachezaji wanne wa Azam, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Deogratius Mushi na Said Mourad.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Azam FC, Nassoro Idrisa alisema kuwa, klabu yake haiwezi kuzuia kusudio la Simba

"Kama Simba inataka kwenda mahakamani ni sawa hatuwezi kuwazuia kwani ni haki ya kila moja isipokuwa ninachoweza kusema tupo tayari tukihitajika.

"Azam ina wanasheria ambao watakwenda kukutana nao kwa ajili ya mapambano ya kisheria na huko ndiko tunakapowasilisha hoja zetu,".alisema Idrisa.

Awali, Rage alisema kuwa tayari ameshawasiliana na mwanasheria wa klabu yake baada ya kupata nakala ya hukumu iliyotolewa na Takukuru alisema kuwa klabu yake imefikia uamuzi huo kutokana na kudhalilishwa kwa muda mrefu tangu uongozi wa Azam ulipotangaza kuwafungia wachezaji hao.

KUTANA NA MUUZA DAWA ZA KULEVYA ALIYEISHIA KUKATWA MIGUU NA MIKONO



UKIMUONA kwa mara ya kwanza ni vigumu kufikiri kama anaweza akawa amepitia katika mikasa migumu ya kutisha ya maisha kama ilivyomtokea. 

Nguo zake kuukuu, nywele za chafu na ulemavu alionao vinaficha historia nzito aliyonayo katika maisha pamoja na utaalamu wa kuongea kwa ufasaha lugha za Kiingereza, Kiitaliano na Kireno licha ya kutosomea.

Huyu ndiye ‘Wa Mbele’ kijana aliyejiwekea ndoto za kuishi nje hasa Ulaya akiamini kuna maisha mazuri ambayo yangemfanya naye awe tajiri.

Hata hivyo ndoto zake hizo zilizimika pale hali hali ilivyobadilika na kujikuta akililia kurudi Tanzania baada ya kukumbana na mateso, manyanyaso, ukatili na biashara za kuhatarisha maisha kiasi cha kumfanya awe mlemavu wa viungo vya mwili uliomdhoofisha na kumharibia maisha yake.

Wa Mbele ambaye jina lake halisi ni Mbembele Said Lipwata nilikutana naye katika safari yangu Mjini Mtwara. Mbali na ulemavu wake wa mguu na mkono wa kulia, bado ana uwezo mkubwa wa kutembea kwa kuruka kwa masafa marefu.

Anasema alizaliwa mwaka 1967 mkoani Mtwara, alikulia huko hadi mwaka 1976 alipojiunga na elimu ya msingi katika Shule ya Shangani.

“Hali duni ya maisha ilinifanya nimkimbie baba aliyekuwa akiishi Mtwara, kwenda kwa mama Magomeni Kagera Jijini Dar es salaam, niliendelea na masomo yangu huko” anasimulia Mbembele akieleza kuwa wazazi wake hawakuwa wakiishi pamoja.

Kaka zake wakubwa walikuwa wanajishughulisha na kazi za ubaharia jambo ambalo lilimpa matumiani makubwa ya kukamilisha ndoto ambazo alikuwa nazo kwa miaka mingi kwamba siku moja angezamia kwenda Ulaya akiamini angepata maisha mazuri.

Baada ya kumaliza masomo yake ya msingi mwaka 1983, Mbembele hakuwa na kazi ya kufanya kutokana na kushindwa kuendelea na masomo ya Sekondari, akaanza kuzunguka na kaka zake katika meli tofauti ndani ya Pwani ya Afrika Mashariki na kujaribu mbinu za kuzamia Ulaya.

Majaribio ya kuzamia
Kutokana na kupata uzoefu kidogo katika safari za meli, Mbembele anasema alianza majaribio ya kuzamia yeye na rafiki zake. Bandari ya Mtwara na Dar es salaam ndiyo vilikuwa vituo vikuu vya majaribio yao.

“Kwa nyakati tofauti tangu mwishoni mwa mwaka 1984 nilianza kufanya majaribio ya kuzamia kwenye meli zilizokuwa zinaenda Asia na Ulaya lakini sikufanikiwa kwa sababu walinzi wa meli walinikamata mara kwa mara,” anasema Mbembele.  

KIM AAMUA "KULIFOTOA" TUMBO LAKE LA MIMBA NA KULIANIKA MTANDAONI



Kim Kardashian ameamua  "kulifotoa"  tumbo  lake  la  mimba  na  kulitupia  mtandaoni  ili  watu  walishuhudie.....

Uamuzi  huo  mgumu  umekuja  baada  ya   mtandao  maarufu  wa TMZ kumvaa  Kim   kwa  madai  kuwa amekuwa  akipotosha  uma  kwa  kutoa  picha feki  za  mimba  hiyo  na  kudai  kuwa  ni  zake. ...

ZIFF YAKERWA NA USHIRIKI MDOGO WA FILAMU ZA TANZANIA






Waandaaji wa tamasha la kimataifa la filamu la Zanzibar, ZIFF wamedai kusikitishwa na muitikio hafifu wa waigizaji wa filamu Tanzania katika kuwasilisha filamu zao.


Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, ZIFF imedai iliitisha upokeaji wa filamu kwaajili ya tamasha la 16 la nchi za Jahazi Septemba 2012 na kuweka mwisho wa kupokea kuwa ni tarehe 31 Machi, 2013 lakini wamepokea filamu chache kutoka Tanzania ukilinganisha na za nje. Jumla ya filamu 200 zimeshawasilishwa mpaka sasa lakini filamu za Tanzania ni tano pekee.
Painkiller
“Filamu za Tanzania ambazo tumepokea mpaka sasa hazi zidi 5 ukijumla na zile zinazoingia katika uchaguzi wa jumla (General Selection) na zile kwajili ya Swahili Movie/Bongo Movie competition,” imesema taarifa hiyo.

“Tukumbuke filamu hizi ndio zitatoa Filamu Bora ya Kitanzania na pia kugombea Filamu Bora ya Afrika Mashariki na maeneo mengine Tumekuwa wavivu wa kusoma websites, blogs na hata magazeti kwa kutegemea kupata taarifa za mdomo au taarifa kwa mtu mmoja mmoja ili kujua nini kinaendelea, jambo ambalo si sahihi, tujifunze kupitia vyombo vya habari ili tupate habari kwa wakati muafaka,”imeendelea kusema taarifa hiyo iliyoandikwa meneja wa tamasha hilo, Daniel Nyalusi.

“Hivyo basi natoa nafasi mpaka tarehe 15 Aprili, 2013 filamu zote za Kitanzania ziwe zimetumwa ZIFF au kupatiwa Ndugu Ibrahim Mitawi (Outreach Officer) – Dar es Salaam (0713-300997) au Mohamed (Film Coordinator) – Zanzibar (0718115468).”

"JAPOKUWA SIJAONA MSANII ANAYENIFIKIA KWA HELA NINAYOPATA KWENYE RINGTONE LAKINI UKWELI NI KWAMBA WASANII TUNANYONYWA"...DIAMOND





Suala la wasanii kunyonywa na makampuni ya simu kwenye mauzo ya ringtone linamuuma kila msanii, hata Diamond ambaye ndiye msanii anayeingiza fedha nyingi zaidi kuliko yeyote Tanzania katika biashara hiyo.


Jana kupitia Instagram, aliandika kilio chake:

Dah! hivi kweli Serikali imekosa majibu ya swali la mh: Mbunge kuhusu mapato ya biashara ya ringtones..!? Kweli sasa naanza kuamini kuwa Serikali Inatukumbatiaga tu kwa Mda mfupi na kututumia Wasanii kwenye Kampeni zao kwa Maslahi yao Binafsi, kisha wanatudump baada ya kufanikiwa kwenye uchaguzi wao, bila kujali thamani na Mmhango wetu kwao.

Hata hivyo kuna watu wanaoamini kuwa Diamond hapaswi kulalamika kwakuwa ndiye msanii anayefaidi zaidi matunda ya muziki Tanzania.

Mmoja wa followers wake aitwaye Princestepp aliandika: Hupaswi kulaumu wewe maanake kati ya wasanii wachache walioweza kula hela za watanzania chini ya ya serikali ya rais wetu Kikwete ni wewe acha unafiki wasanii wengine ambao hawajapata fursa kama yako walaumu vipi sasa?

Diamond alijibu: Mi nimekula pesa na bado nakula pesa kwa juhudi zangu za kujituma jukwaani na kufanya show nzuri, sio kuwa naitwa kupewa pesa za ringtones nah! Napewa show…. So nikiwa kama mfano mzuri kwa wasanii lazima niwe mstari wa mbele kupigania haki za wasanii kiujumla. 

Aliongeza, “Mi napigania haki zetu upande mwingine wananiona snitch.. wakati mi naamini katika wasanii wote japo nadhulumiwa lakini hakuna hata anayefikia hela nnayolipwa kwa rintones.. ila naona haiwezekani kwanini watufanye wajinga watu wapewe haki zao.”

"MUME WANGU KAZIDI USALITI NA NDO MAANA NIMEAMUA ''KUGAWA NJE'".. MKE WA MTU




Mimi nimeolewa miaka 15 sasa na tumejaaliwa watoto 4. Ndoa yetu ilipofikisha miaka 4-5 mume wangu alicheat, nikamkamata through sms akapinga sn lakini baadae alikubali akakiri kosa na kuomba msamaha. nikamsamehe

Tumeendelea kuishi na nilipopata mtoto wa tatu akanicheat tena, safari hii alikuwa nje ya nchi kimasomo, napo alikiri na kuomba msamaha, nikamsamehe..


Wakati niko mjamzito mimba ya mtoto wa nne alinicheat tena, kibaya zaidi alinicheat na house girl wng akampa ujauzito. kwa ivo wkt mimi nina mimba na House girl naye mjamzito(japo sikujua km house girl alikuwa mjamzito kwani aliondoka nyumbani) niligundua baadae kuwa mtt wa aliyekuwa house Girl wangu ni wa mume wangu..


Kama kawaida yake akaomba msamaha safari hii hadi kupiga goti na kulia ili nimsamehe...na mimi kwa kuwa bado nampenda na nimemvumilia kwa mengi nikaamua kumsamehe tena..ila tulikubailana masharti mengi na akakubali masharti yote niliyompa..mwanzoni alibehave vizuri sn akawa muwazi kwng hanifichi chochote kuhusu huyo mtt.. na tuliishi maisha ya furaha kwn alinijali mno na alionekana kweli amerigrate.


Sasa cha kushangaza siku za karibuni amebadilika san, amekuwa msiri na hasemi chochote kuhusu huyo mtt wa nje..siku hizi anatuma hela kwa siri na pia anawasiliana na huyo mama wa mtoto kwa siri haniambii chochote..

Nilipoona mabadiliko niliamua kumuuliza imekuwaje tena mbona siri tena wkt tulikubaliana kila kitu kiwe open? hakunijibu isipokuwa alikuwa mkali na kufoka na kusema hilo swala tumeshamalizana nalo sitaki kulisikiasikia tena..


Nikajaribu tena siku nyingine kumuuliza na majibu ndio hayo hayo, kwa kifupi hataki na anakwepa kuzungumzia hilo suala kabisa...sasa najiuliza kwa nini anafanya siri? km hakuna jambo lolote baya basi anaficha nini? ina maana kuna kitu zaidi ya mtoto.

Sasa jamani mimi nimeamua km ifuatavyo


1. Na mimi nimeamua kuwa na mahusiano nje ya ndoa, jamani msinilaumu nami pia nahitaji kuliwazwa na kufarijiwa kwa kifupi nimechoka na mastress yasiykuwa na mwisho, sikuwahi kumcheat mume wng ktk maisha yote ya ndoa. ila sasa atanisamehe tu ht akijua wl sijali, nipo tayari kwa lolote..


2. Sina mpango wa kuondoka kwenye nyumba tuliyojenga pamoja nitaishi hapa hapa kwani sipendi wtt wng walelwe na mzazi mmoja..wtt hawajui kinachoendelea in fact hata ndugu na jamaa hawajui chochote kwani mimi sijawaambia na wala sijawahi kuwaeleza matatizo ya ndoa yng..kwa nje tunaonekana familia iliyobarikiwa na ina furaha lkn wenyewe ndio tunaojua ndani kukoje


3. Kwa sababu sisemagi matatizo yangu kwa ndugu na marafiki nimeamua kuweka hapa labda nitapunguza kitu fulani kichwani kwani sometime naona km nazidiwa mawazo vile

MADHARA KWA WANAUME WANAOPENDA KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE.



Madhara anayoyapata mwanaume anayependa mchezo huo wa kufanya Mapenzi kinyume na maumbile ni kama ifuatavyo:-

Kwanza: Husababisha kusinyaa au kuweka makovu kwenye njia ya haja ndogo.

Pili: Njia ya haja ndogo kuziba kiasi au kuziba kabisa.

Tatu: Kupata saratani (kansa) ya tezi za figo (prostate gland).

Nne: Kupata magonjwa sugu ya uti wa mgongo.

Tano: Kuharisha.

Sita: Maambukizi ya VVU ambapo mwisho wake ni Upungufu wa Kinga Mwilini (Ukimwi).

Saba: Baadaye mhusika kupata msongo wa mawazo au sonona kwa kujutia tendo hilo.

Kila mwenye tatizo aende kwenye hospitali yoyote kubwa iliyo karibu au Tiba ya kwanza ni kuachana na mchezo huo kisha unaweza kufanya taratibu zingine za kucheki afya yako.


SHILOLE ANASWA AKIVINJARI NA BWANA WA KIZUNGU!











Siku chache baada ya kuripotiwa akijiachia kimalavidavi na ‘lejendari’ wa Bongo Fleva, Aboubakar Katwila, staa wa muziki na filamu za Kibongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amenaswa hotelini na bwana Mzungu aliyetajwa kwa jina moja la George, kamera za Risasi Mchanganyiko ni noma.

Kwa mujibu wa shushushu wetu, tukio hilo lilijiri hivi karibuni katika hoteli moja maarufu jijini hapa ambapo Shilole alikuwa kwenye ziara ya shoo yake.
Ilidaiwa kuwa mara tu baada ya kumaliza ziara ya shoo, Shilole hakuondoka jijini hapa na badala yake alionekana sehemu tofauti akijivinjari na jamaa huyo ambaye uchunguzi wetu ulibaini kuwa ni bosi wa klabu moja maarufu ya usiku Kanda ya Ziwa.

Kabla ya kuondoka katika jiji hili la sangara na sato, Alhamisi iliyopita na ndege ya jioni, Shilole alinaswa kimalavidavi na Mtasha huyo Jumatano katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere wa Gold Crest kulipokuwa na maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Syria.
Shilole alishuhudiwa akifanyiwa ‘shopping’ ya kufuru na bwana huyo ambapo gazeti hili lilinasa mpango mzima ambapo lilipotaka kujua kama ni wapenzi, Mtasha huyo alijibu kwa kifupi sana  (sina la kusema).

Kwa upande wake Shilole alipobanwa mbavu alifunguka: “Nisingependa kuongelea jambo hilo kwani sasa najipanga kimuziki zaidi, shopping ni mambo ya kawaida sana kwa hiyo ni vyema tukaongelea muziki wangu kwani shoo yangu ya Pasaka ilijaa mashabiki wa kufa mtu so nakubalika sana Mwanza na siku moja nitaweka makazi hapa.”

IRENE UWOYA AFUNGUKA KUHUSU KUFUMWA HOTELINI AKIWA NA DIAMOND!




Baada ya habari nyingi sana kuhusu Irene Uwoya kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Diamond platnumz kutawala vyombo vya habari na kwenye mitandao hapo juzi, hatimaye bongojunior blog iliamua kutafuta undani kuhusu mwanadada Irene Uwoya ili tuweze kufahamu juu ya tuhuma hizi za yeye kuingilia penzi lwa mwanadada Penny kwa kijana wa “mbongofleva” diamond platnumz.

Baada ya majaribio mengi ya kupiga simu yake ambayo ilikuwa haipatikani muda wote wa mchana baadaye kwenye mida ya saa kumi na mbili hivi jioni tuliweza kumpata hewani na Jibu lake lilikuwa moja tuu kuwa “achana nazo” na sisi tukaona kweli tuachane nazo ila tukufukishie wewe msomaji wetu mpendwa “response” hiyo ili mwenyewe uamue na kutafakari. Hilo ndo jibu alilotupa mwanadada mrembo wa bongo movies Irene Uwoya kuhusu tuhuma za yeye kutoka kimapenzi na msanii Diamond.

HAYA NI MAJIBU YA SINTAH ALICHOGUNDUA KUHUSU IRENE UWOYA NA DIAMOND.


.





Haya Chini ni Maneno ya Sinta
"Sincerely, mmenishangaza na comments zenu kuyaamini magazeti, mengine yameandika hiki ama kile sasa nataka kukwambia si magazeti yote yanaandika ukweli, jana usiku wawili hawa walikuwa tight na kukumbatiana century cinemax  na lile baridi kama nawaona.

Mimi sisemi mengi mliniomba nifuatilie na haya ndiyo majibu,,,, Diamond na Irene si wapenzi

MWANAHARAKATI WA MASHOGA AKAMATWA HUKO ZAMBIA





Mwanaharakati mashuhuri wa kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja, amekamatwa nchini Zambia kwa kuonekana kwenye televisheni akitaka uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja kutofanywa kuwa hatia.

Paul Kasonkomona alishatakiwa kwa kosa la ''kuwachochea watu kushiriki vitendo visivyokubalika,'' alisema mkuu wa polisi Solomon Jere.
Paul alikamatwa alipokuwa anaondoka nje ya studio hizo za kampuni ya kibinafsi ya Muvi.

Vitendo vya mapenzi ya jinsia moja, ni haramu nchini Zambia.

Wadadisi wanasema kuwa watu wengi, wanaamini kuwa ni kinyume na imani zao

Duru katika stesheni hiyo, mjini Lusaka zilisema kuwa polisi walijaribu kukatiza mahojiano lakini wakuu wa stesheni hiyo walikataa.

Katika ombi lililotolewa kwa rais wa Zambia Michael Sata, kundi moja la wanaharakati nchini Afrika Kusini Ndifuna Ukwazi, lilitaka kuachiliwa mara moja kwa bwana Kasonkomona.

Kundi hilo pia lilisema linataka serikali ya Zambia kuanzisha mara moja mpango wa kutofanya vitendo hivyo kuwa kinyume na sheria ikiwa itakuwa kati ya watu wazima licha ya jinsia yao.

Vitendo kama ulawiti na uhusiano wa mapenzi kati ya wanawake, vina adhabu ya miaka 15 au kufungwa maisha jela.

Wiki jana kikundi cha wapenzi wa jinsia moja kilijaribu kujisajili kama wanandoa lakini wakakatazwa na serikali ikaamuru kukamatwa kwa yeyote atakayepatikana akihusika na vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.

Muungano wa ulaya mwezi jana ulitoa msaada wa kifedha kwa mashirika yaliyotaka kuhamasisha kuhusu haki za wapenzi wa jinsia moja nchini Zambia.

Mnamo mwaka 2011, Marekani na Uingereza zilionya kuwa zitatumia msaada wa kigeni kama kikwazo cha kutoa ufadhili kwa nchi za kiafrika ili kuhalalisha mapenzi ya jinsia moja.
Afrika Kusini ni mojawapo ya nchi chache barani Afrika zilizohalalisha mapenzi ya jinia moja.

LULU MICHAEL NA POZI LA MITEGO KATIKA SIKU YA KUMUENZI X- WAKE




 Hii ndo picha ya kimitego imewekwa kwenye instagram na Lulu kwenye siku ya kumuenzi marehemu Kanumba  ikiwa  ni  masaa  machache  tu  baada  ya  kutoka  katika  kaburi  la  marehemu Kanumba.....

BINTI ANASWA AKIFANYA MAPENZI NDANI YA GARI ...




Hawa binadamu  wasiokuwa na aibu  walikutwa barabarani wakifanya mapenzi huku wakiwa wameegesha gari lao pembeni

Tukio hili chafu lilitokea week end iliyopita wakati  binti  huyu  akitoka  club  huku  akiwa  tungi.Alipotoka  nje  ya  ukumbi  huo  wa  starehe, alionekana  kumvaa  dreva  tax  mmoja  ili  ampeke  nyumbani.....

Mdau   aliyeinasa  picha  hii  anadai  kuwa  walipoondoka  naye  aliwasha  gari  yake  tayari  kwa  safari  ya  kurudi  kwake.Wakiwa  njiani, alishtuka  kuona  gari  hiyo  ikipakiwa  pembeni  mwa  barabara....

Jamaa  anadi  kuwa  alilipita  gari  hilo  na  alipofika  mbele  alikaa  kidogo  na  kuamua  kurudi  tena  na  ndipo  alipowafuma  live  wakifanya  uchafu  huo  na  kuwapiga  picha....

Walipokurupushwa  na  mwanga wa kamera  ya  jamaa  huyo, mbulula  hao  waliliondoa  gari  lao  kwa  kasi  na  kutokomea

TABIA YA MWANAMKE ASIYEWAJIBIKA KITANDANI!!






Inasemekana wanawake wengi wenye ndoa wanakuwa na tabia zifuatazo zinazosababisha waume zao kwenda nje ya ndoa na wale wasio na tabia ya nyumba ndogo wanaishia kubakwa na waume zao

Mwanamke asiyemtamkia kabisa mumewe kuwa anajisikia kuwa naye.

Mwanamke ambaye baada ya mechi huwa haonyeshi dalili yoyote kama ameridhika na tendo au hakuridhika

Mwanamke ambaye akiwahi kulala yeye mume akija hataki kuguswa

Mwanamke ambaye mumewe akimgusa anakubali huku analalamika .. kama ulikuwa unataka kwa nini hukuwahi kulala unangoja nilale ndo unakuja kunisumbua

Mwanamke huyo hatingishiki kwenye mechi kata kidogo tena amenuna  anangalia kushoto au kulia anangoja goli liingie ... kama golikipa aliyekata tamaa ya kudaka penati

Mwanamke haweki kabisa maandalizi kama zana za kufanyia usafi baada ya mechi kama taulo, kitambaa na kadhalika

Ziko nyingine nyingi ambazo ni kero zinazowafanya wanaume kusononeka....na mara nyingine juamua kuzira na kuwa mwanzo wa mmoja kuhama chumba..... Wanawake wenye tabia hizi jirekebisheni