Wednesday, May 22, 2013

KAKA NA DADA WANASWA WAKIVUNJA AMRI YA SITA KATIKA MAPANGO YA UFUKWE WA COCO





UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya Firauni. Usemi huu unakamilishwa na tukio la kunaswa kwa vijana wawili wenye undugu wa damu wakifanya mapenzi   kando ya Ufukwe wa Bahari ya Hindi

Imefahamika kwamba vijana  hao, kaka na dada   wamenaswa ‘wakingonoka  katika mapango yaliyopo kando ya Ufukwe wa Coco, Oysterbay jijini Dar es Salaam.


Tukio zima lilitokea mchana kweupe wa saa 9 na kudhihirisha habari za mara kwa mara zinazoeleza kwamba Ufukwe wa Coco umekuwa ukitumika kwa ufuska usiku na mchana.

Risasi  lilinasa tukio hilo kwa kutumia mitambo maaalum iliyoelekezwa kando ya bahari.
 
Wawili hao walinaswa tangu walipokuwa wakiingia katika ufukwe huo na kuwafuatilia nyendo zao, hatua kwa hatua.



Haikufahamika mara moja kama wawili hao walikuwa na makubaliano ya kwenda kuduu katika ufukwe huo au la, lakini kwa mbali ilionekana kama vile dada mtu alikuwa akizingua kwenda kutenda dhambi hiyo.
 
Picha za video zilizonaswa, zinamuonesha dada huyo akionekana kutoa upinzani pale alipokuwa akishikwashikwa na kaka yake.

Alionekana kama vile hakuwa tayari kwa mchezo huo.
Hata hivyo, kaka mtu anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 23-26 alikuwa akilazimisha kitu fulani ambacho kilionekana dhahiri kupitia kamera zetu.
Ni kama vile hawakuwa na makubaliano na kile walichokuwa wakienda kukifanya.
 
Mara kadhaa dada huyo alionekana kumkwepa kaka yake na alikuwa akijiondoa karibu yake pale alipomlazimisha kutaka kumfanyia kitu kisichokuwa cha kawaida.



Kamera za Risasi ziliwafuatilia wawili hao kwa kuwa walionekana kuwa na kitu ‘spesho’. 

 Mpaka wanazama katika mapango yaliyopo kando ya ufukwe huo wa Coco, kamera zilikuwa zikiendelea kuwachukua hadi walipozama ndani kabisa ya mapango hayo. 
 

Walipozama ndani ya mapango hayo, ghafla walitokea askari ambao nao walikuwa wakifuatilia nyendo za wawili hao.
 

Askari hao wa Kituo cha Oysterbay, wakiongozwa na kamanda wa oparesheni maalumu katika Wilaya ya Kinondoni, Kamanda Swai walifuatilia kwa umakini tukio hilo.
 

Wakiwa chini ya mapango, kaka na dada waliondoa vinguo vilivyokuwa maungoni mwao na kuanza kuduu kama vile walikuwa katika ufukwe unaoruhusiwa kufanya vitendo hivyo.
 
Kabla askari hawajawavamia, waliwashuhudia wawili hao wakiwa katika kilele cha sterehe yao huku dada mtu akionesha kutoa ushirikiano kwa shingo upande.


Ghafla, askari waliwavamia na kuwatibulia starehe yao kisha kuwatia mbaroni.
 

Baada ya kuona kuwa wamevamiwa na askari, kaka mtu alichomoka na kutafuta silaha ili kuweza kujihami na wavamizi wake bila ya kujua kama ni askari.
 

Katika hilo nusura zipigwe kati ya askari na kaka huyo ambaye alikuwa akitaka kupigana na watu asiowajua kwa kuwa walikuwa wametinga mavazi ya kiraia.
 

Hata hivyo, alitulizwa na kutakiwa kuvaa pensi yake ili aweze kutoa maelezo kwa kina. 
 

Wakati yote yakiendelea, dada mtu alikuwa amepigwa na butwaa na kutojua cha kufanya hadi aliporushiwa kitenge chake kilichokuwa pembeni ili ajisitiri mwili wake. 

Katika mahojiano ya awali yaliyoongozwa na Kamanda Swai, ilibainika kwamba wawili hao ni ndugu wa damu yaani kaka na dada.  

Maelezo hayo yanasema kuwa dada mtu alitoka mkoani na alikuja kutembea jijini Dar es Salaam, ndipo kaka yake alipomtaka watoke kwenda kumuonesha vivutio vya jiji hilo. 

“Nina miaka 19, nimetokea Iringa kuja Dar kutembelea familia lakini kaka akanileta huku na kunifanyia vile, siyo kama tulikuwa tumekubaliana,” alisema dada huyo kwa aibu.

Kaka mtu alikiri kile kilichosemwa na dada yake na kushindwa kujitetea kwa kuwa kila kitu kilikuwa hadharani. 


Wawili hao walichukuliwa na kupelekwa katika Kituo cha Oysterbay kwa ajili ya kufunguliwa kesi ya uzembe na uzururaji na kusekwa rumande kabla ya kufikishwa mahakamani.

KUNDI LA CAMP MULLA LAZIDI KUPASUKA....



Hivi karibuni tuliandika habari kuhusu kundi linaloundwa na vijana wanne wenye vipaji kutoka Kenya linalofahamika kama Camp Mulla kumpoteza member mmoja ambaye ndio aliyekuwa msichana pekee katika kundi aitwaye Miss Karun.


Mwanzo ulianza kama uvumi kuwa Miss Karun amepigwa chini na kundi hilo na nafasi yake kuchukuliwa na msichana mwingine aitwaye Tiri, lakini habari mpya habari zilizothibitishwa Kupitia mtandao wa kituo kikubwa Africa Kusini Channel O, zinasema Miss Karun ameamua kujiondoa kwenye kundi kwaajili ya maandalizi ya kujiunga na chuo. 
  

Miss Karun anategemewa kwenda masomoni nchini Marekani mwezi August mwaka huu, lakini ataendelea kufanya muziki kama solo.

camp m

Kama vile haitoshi, kwa mujibu wa mtandao huo member mwingine aitwaye Thee Mc Africa zamani alifahamika kama Taio Tripper naye amejitoa katika kundi hilo na ataendelea kufanya muziki kama solo. 
  

Kundi hilo lilianzishwa mwaka 2009 likiwa na members wanne, Kwa sasa limebaki na members wawili wa mwanzo pamoja na msanii mpya wa kike aitwaye Tiri.

VURUGU ZA MTWARA ZASABABISHA BUNGE LIAHIRISHWE....




Spika wa bunge , Anne Makinda ameahirisha Bunge kutokana na hali ya Mtwara na ameiagiza serikali kuwa kesho wawasilishe taarifa bungeni kuhusiana na hali hiyo.

Makinda ameitisha kamati ya uongozi ili kuona kama wanaweza kutuma kamati ya Bunge kesho kwenda huko.

UKICHECHE WAMFANYA MR. NICE AZOMEWE NCHINI KENYA




Mtandao wa ghafla kutoka Kenya umeripoti kuwa, msanii Mr Nice, amejikuta akizomewa na umati wa watu waliokuwa katika Club moja inayoitwa I club, ambapo wachekeshaji Fred Omondi na Mc Antonio hufanya show zao pale kila siku za jumapili.

Inasemekana Mr Nice alikua ameenda pale kwa ajili ya kula good time tu, na kufurahisha nafsi yake, lakini matokeo yake hayakuwa kama alivyotarajia....

Aibu  ilianza pale mchekeshaji Mc Antonio alipomuona Mr Nice katikati ya watu, na kwakuwa ni mtu maarufu, Mc akamuambia awapungie mikono watu waliokuwepo pale...


Mr Nice hakufanya hivyo wala kusimama akidai kuwa yeye ni msanii ambae amesainiwa na mtu mwingine na Mc huyo hawezi kumlipa yeye, na akipanda jukwaani hapo atashitakiwa na magement yake.
 
 " Hamnilipi ninyi... nikipanda hapa kwenye jukwaa, nitashtakiwa mimi"..Mr.Nice

Baada ya kusema maneno hayo mashabiki walianza kumzomea huku wakipiga kelele wakisema Mac "Muga" wimbo  wa Ally Kiba, ambao unasemekana kuwa unamdiss yeye. na dj hakuwa na hiyana aliupiga wimbo huo maana mashabiki waliutaka.

Djfetty

"WASANII WANAOVAA VIMINI KWENYE FILAMU HUWA WANAJIUZA"....MWAKIFAMBA




RAIS wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifwamba amesema wasanii wanaovaa mavazi yasiyo na staha ikiwemo vimini kwenye sinema wanajiuza.

Mwakifwamba aliyasema hayo katika mahojiano na kituo kimoja cha runinga, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, akiwa ameongozana na msanii Riyama Ally.
 

Kauli hiyo ya Mwakifwamba imekuja siku chache baada ya sakata la uvaaji vimini na udhalilishaji wanawake na wototo kwenye filamu kuzungumziwa bungeni, Dodoma.

“Hili suala nimeshalikemea kwa muda mrefu sana... naamini kama ni watu wa kuelewa watakuwa wameelewa na wale ambao wanaendelea na hayo mambo maana yake ujue wana mambo yao.


“Siyo wote wanaoingia kwenye filamu ni wasanii wa kweli, wengine wanatumia tasnia hii kutafuta mabwana ndiyo maana wanavaa mavazi ya ajabu ili waonekane, jambo ambalo tunalikemea kila wakati

"Sikatai wakati mwingine kuna ‘scene’ zitahitaji uhusika fulani kama uchangudoa lakini utakuta msanii anatakiwa kuvaa uhusika wa ofisini, yeye anavaa vinguo vya hovyo, maana yake ni nini kama si kutafuta soko?” alisema Mwakifwamba na kuongeza:
 

“Imefika wakati wasanii wanatakiwa wabadilike kwani hali ilipofikia siyo pazuri. Bado msanii anaweza kuonekana ana kiwango kizuri bila kuvaa nguo zinazomdhalilisha na kumtafsiri vibaya mbele ya jamii.”
 

Akasema: “Sasa nasema hivi, yeyote atakayekiuka utaratibu tuliokubaliana tutamchukulia hatua. Hatutamfumbia macho. Tunahitaji kuwa na tasnia yenye heshima.”
 

RIYAMA SASA
Mkali wa kucheza na hisia, Riyama naye alitoa maoni yake kuhusu mavazi na mwenendo mzima wa filamu za Kibongo ambapo kwa upande wake alisema anaamini wanaofanya hivyo wanatafuta kuwa mastaa kwa njia ya mkato.
 

“Tatizo ni ulimbukeni wa kuiga wasanii wa nje. Wasanii tunakiwa kujitambua na kufahamu na kulinda utamaduni wetu. Wasanii wengi hawajui thamani zao, jamani ustaa siyo kukaa uchi.
 

“Tujue kuwa kwenye filamu siyo sehemu ya kutafutia mabwana. Kuonesha urembo wetu wa nje na wa ndani kwenye hadhara siyo kitu kizuri kwa utamaduni wetu... hao wanaofanya hivyo wanasababisha wasanii wote tuonekane machangudoa,” alisema Riyama.