Tuesday, June 4, 2013

MWANADADA WA KITANZANIA ANAYETARAJIWA KUNYONGWA IJUMAA HII NCHINI MISRI BAADA YA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA



Kuna hizi habari  ambazo  zimeanza  kusambaa  kwa  kasi  siku  ya  jana  katika  mitandao  ya  kijamii.....

Taarifa  hizo  zinamuonesha  msichana  ( pichani)  wa  kitanzania  ambaye  anadaiwa  kunyongwa  ijumaa  ya  wiki  hii  baada ya  kukamatwa  na  madawa  ya  kulevya....

Mtandao  huu  bado  haujathibitisha  ukweli  ama  undani  wa  habari  hizo....

LAKINI  kwa  tahadhari, tunaomba  kama  kuna  yeyote  anayemjua  afanya  mawasiliano  na  ndugu  zake  maana  huenda  ikawa  ni kweli.

Na  kama  si  kweli, basi  habari  hii  ipuuzwe..!!

SIMULIZI: MZEE WA MIAKA 80 ATENDEWA UNYAMA WA KUTISHA...... FAMILIA YAKE YATUPWA NJE NA KUBEBEWA VITU VYOTE




MAISHA ya familia ya mzee Athumani Mwenda, 80, ni ya mateso makali baada ya nyumba yao kubomolewa ikiwa na vitu ndani.

Mzee huyo na familia yake sasa wamekuwa wakiishi nje huku wakikabiliwa na njaa pamoja na maradhi mbalimbali.
 
Tukio la kuvunjiwa nyumba lilitokea Mei 24, mwaka huu katika Kitongoji cha Mvuti, Ilala, Dar na inadaiwa kuwa ubomoaji huo ulifanyika chini ya mtu aliyejitambulisha kwa jina la Boatu Msuya ambaye ni dalali wa mahakama huku akiongozana na polisi sita wenye bunduki aina ya SMG.
 
Akielezea tukio hilo kwa masikitiko makubwa, mzee Mwenda ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sangara, Kata ya Msongora alikuwa na haya ya kusema:
 

“Sina mahala pa kwenda na hawa watoto, nani anaweza kutupa hifadhi, chakula na matibabu? Tunaishi kama wanyama porini.

“Sijatendewa haki hata kidogo, ni bora wangetuua kuliko kutufanyia kitendo hiki kilichosababisha tuishi kwa dhiki. 

Sidhani kama kuna mahakama inayotoa amri ya kugawa ardhi yangu bila kutembelea eneo la tukio, anayedaiwa kuwa ni dalali amegawa na kuchukua eneo kubwa tofauti na tulivyopatana mahakamani.
“Ni zaidi ya nusu ekari na ndiyo maana wamechukua na eneo la nyumba yangu na kuibomoa huku nikiwa nimelala ndani na wajukuu zangu, niliamshwa dakika za mwisho, nikaokolewa na wajukuu zangu, nusura tufunikwe na kifusi.
 
“Nilipotoka nje nilikuta kundi la vijana na askari, niliwauliza kwa nini wananibomolea nyumba, wakanijibu nikae kimya. Hakuna kiongozi yeyote wa serikali aliyekuja naye wala barua inayonitaka nihame au kubomoa nyumba.

“Ninachokijua ni kwamba tulikubaliana mahakamani kuwa nigawe nusu ekari ya ardhi yangu ninayoishi nimpe tuliyekuwa naye kwenye kesi mahakamani.
 
”Naamini kungekua na watendaji wa mahakama hapa au kiongozi yeyote wa serikali wa kusimamia zoezi hili haya yote yasingetokea, nimeonewa.
 

“Kwa sasa tunalala nje, mvua, jua na maradhi ni vyetu, nimeishi hapa tangu mwaka 1980 enzi hizo hapa likiwa pori, leo hii wameona lipo karibu na barabara ya lami wanaamua kujigawia, sikubali hata kidogo,” alisema.

Afisa Mtendaji wa kata hiyo, Omar Ali Khalfan alipoulizwa juu ya sakata hilo, alisema kwamba mzee huyo tayari ameshachukua hatua ya kuandika barua kwenda mahakama kuu na ameshaipitisha na kumgongea muhuri.

ALBERT NGWEA APOKELEWA KWA HUZUNI KUBWA, MWILI WAKE UMEPELEKWA HOSPITALI YA MUHIMBILI




 Mwili ukipelekwa  muhimbili....

Mwili wa Marehemu Albert Mangwea aliyefariki dunia May 28 huko Johannesburg leo umeingia Dar es salaam na kupelekwa moja kwa moja hospitali ya Muhimbili, umati wa watu  umefika uwanja wa ndege kushuhudia na kumpokea Ngwea.
 

KIFO CHA ALBERT MANGWEA FURAHA KWA DIAMOND, APONDA MARAHA BAHARI YA HINDI WAKATI WASANII WENZAKE WAKISUBRI MWILI WAKE AIPORT


Popin champagne wit my Fam
ily Cc @rommyjones.Hapa akiendesha boti la kifahari katika bahari ya hindi jijini Dar es salaam na rafiki zake.akiendesha gari wakati akielekea katika kuponda bata.
MASHABIKI WAMPONDA KATIKA MTANDAO MARA BAADA YA KUPOSTI NA HIKI NDICHO WALICHOANDIKA KATIKA MTANDAO WA FACEBOOK.