Pichani ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Mizengo Kayanza Peter Pinda (wa Kwanza Kushoto) akiwa pamoja na Mbunge wa Simanjiro, Bwana Christopher Ole Sendeka (Wa pili kushoto), Aliyekuwa Mkuu wa Mikoa Mbalimbali hapa Nchini, Bwana Ditopile Ukiwaona Mzuzuri (wa tatu kushoto) na wa mwanzo upande wa kulia ni Kijana wa Mjini William Vangimembe Lukuvi.
Picha hii ilipigwa Miaka ya 80 wakati huo Vijana hawa wakiwa ni Viongozi wa Jumuia ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete akionekana katika Sare zake za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Picha hii inatajwa kupigwa Mwanzoni mwa Miaka ya 80 wakati huo Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Jeshini.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Anne Simamba Makinda katika Kivazi chake na Namna alivyotengeneza nywele zake.
Picha hii ilipigwa Mwaka 1994 wakati Mama Anne Semamba Makinda akiwa ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto.
Gavana wa Kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania, Waziri wa Zamani wa Fedha, Mfanyabiashara na Mkulima Mashuhuri, Mchunga Mbuzi aliyebobea, Fundi Viatu aliyepata Elimu kwa Msaada wa Chama cha Ushirika, Mwasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA na Mmoja wa Viongozi Madhubuti wa Taifa hili, Mzee Edwin Mtei
.Picha hii ilipigwa Mwezi Aprili Mwaka 1974 wakati Bwana Edwin Mtei alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki.




Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Maarufu zaidi kama "Rais wa Mbeya", Mwanaharakati wa Utetezi wa Haki za Wanamuziki na Mwanamuziki Mkongwe wa Muziki wa Kughani wa Kitanzania Bwana Joseph Mbilinyi "Mr 2/Too Proud/Sugu" (Katikati mwenye Kofia) akiwa na Maswahiba zake miaka kadhaa Nyuma.




Rais Jakaya Mrisho Kikwete pamaoja na Mwadhama Kardinali Laurean Rugambwa, Picha hii ilipigwa katikati ya miaka ya 90.


Bibi Titi Mohammed. Hii ilipigwa Mwaka 1957 wakati Bibi Titi Mohammed akiwa anahutubia Wananchi katika moja ya mikutano ya Chama cha TANU.


Waziri Mkuu wa Zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr, Salim Ahmed Salim.
Picha hii ilipigwa Mwaka 1970 wakati Dr. Salim Ahmed Salim akiwa katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kujitambulisha kama Balozi Mpya Mteule wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
Mbaraka Mwinshehe Mwaruka japo Vijana wenzie wa Zamani walipenda kumuita majina Mbalimbali kulingana na Umahiri wake katika Kutunga, kuimba na Kupiga Gitaa akiwa katika Bendi ya Morogoro Jazz mpaka alipounda Bendi yake ya Super Volcano.

Haijalishi ulizaliwa enzi za uhai wake au baada ya kifo chake, jambo moja ambalo wote tunafanana ni kwamba ukisikia muziki wake sio
 ajabu utatikisa kichwa, kutabasamu, kucheza au kurukaruka.

Alifariki kwa ajali ya gari Nchini Kenya tarehe 13 Januari mwaka 1979, kifo chake kikichangiwa zaidi na kuvuja damu nyingi na asipatikane wa kumchangia damu ili kuokoa maisha yake pale hospitalini Mombasa.

Pichani ni Mbaraka Mwinshehe akimvisha Pete ya Ndoa mke wake, Amney Shadad, Hiyo ilikuwa tarehe 17/3/1972 Mjini Morogoro.




Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwa anazungumza na Mfalme wa Muziki wa Pop Duniani na Mwanamuziki Mashuhuri wa Marekani, Marehemu Michael Joseph Jackson Ikulu Jijini Dar es salaam. Picha hii ilipigwa Mwaka 1992 wakati Mfalme huyu wa muziki wa Pop wa Marekani, hayati Michael Jackson alipoitembelea Tanzania na kufanya Kitendo cha Kiungwana kwa kufika katika Shule Maalum ya Watoto Yatima na wenye Mtindio wa Ubongo iliyopo Sinza, Jijini Dar es salaam. Mwanamuziki huyo aliyekuwa maarufu zaidi duniani hadi anakufa 2009, alifika nchini akiwa Balozi wa ziara ya Umoja wa Mataifa na akapokelewa kiserikali na Waziri wa Mambo ya Nje wakati huo, hayati Balozi Ahmed Hassan Diria.


Meya wa wa Kwanza Mweusi wa Jiji la Dar es salaam, sheikh Amri Abedi Kaluta (wa Nne Kulia) akimtambulisha Mume wa Malikia waUingereza ambaye pia ni Bwana Jumbe wa Edinburg (Duke of Edinburg) Prince Philip (wa Pili kulia Mwenye Sare za Jeshi) kwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania na Kardinali wa Kwanza Mwafrika Duniani, Mwadhama Laurean Rugambwa (wa Kwanza kulia). Pamoja na Kuwa Meya wa Jiji la Dar es salaam Sheikh Amri Abedi Kaluta pia alikuwa Kiongozi Mkubwa wa Kidini wa Waislam hapa Nchini Tanzania.

Credits: Jamii Forum