Friday, May 17, 2013

SAKATA LA SHOW YA JIDE : MATONYA NAYE AUNGANA NA KINA LINAH KUICHOMOLEA SHOW...PESA KALAMBA, SHOW KAGOMA KUPIGA....TIRIRIKA HAPA




Seif Shaban ‘Matonya’.
Na Mwandishi Wetu
WAKATI wasanii wa Bongo Fleva, Elias Barnaba na Estalina Sanga ‘Linah’ wakidaiwa kupokea fedha na kuitolea mbavuni shoo ya Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ au Jide, msanii Seif Shaban ‘Matonya’ naye ameuvaa msala mpya wa kuikacha shoo hiyo huku akiminyia mshiko wa kianzio (advance) aliolipwa tangu  mwishoni mwa Aprili, mwaka huu.
Kwa mujibu wa mtandao wa Lady Jaydee, Matonya alikuwa miongoni mwa wasanii watakaopafomu katika shoo ya kuadhimisha miaka 13 ya Lady Jaydee inayotarajia kufanyika Mei 31, mwaka huu katika Ukumbi wa Nyumbani Lounge, jijini Dar lakini baadaye akagaili.
Kwenye maelezo ambayo Jide ameyaweka katika mtandao wake, aliainisha madai kuwa huenda Matonya naye akawa ametumiwa na watu wasioitakia mafanikio shoo hiyo baada ya kupata taarifa kuwa anatarajia kutumbuiza kwenye shoo hiyo kama ilivyotokea kwa Barnaba na Linah.
Kudhihirisha hilo, Lady Jaydee ameanika mahojiano kati ya Gardner G. Habash ‘Captain’  kama meneja wa Lady Jaydee na Matonya kwenye blogu yake kuonesha namna ambavyo anahisi staa huyo ametumiwa. Yafuatayo ni baadhi ya mahojiano haO:
Matonya: Kaka kumbe tarehe ni lini kumbe?
Captain: Ni Ijumaa tar 31 Mei 2013 kaka mwezi ujao. Tutakuwa na Linah, Jay, Barnaba, Matonya, TID, Hamza Kalala.
Matonya: Kaka kumradhi sana kuimba na bendi kwa sasa sitoweza manake mtahitaji mandalizi makubwa ili nifanye kazi vizuri ningeomba nitizamwe katika kazi nyingine kaka kumradhi sana.
Captain: Duh! nilishatangaza kaka, lakini sawa. Je, nitapata ile hela nilipe wengine ndugu yangu?
Matonya: Aisee! hata nimekosa raha kukujuza ili swala bro,  kesho saa tano nitampa yule rafiki yangu anaitwa Pizon walikuja kuleta ile pesa ya gari kwa hiyo wataileta hapo hapo ofisini.
Captain: Sawa kaka usijali, nitashukuru akiileta ili huku nisipate lawama.
Matonya: ok bro.
Mara kimyaaaaaaa... baada ya siku mbili tatu maongezi yakaendelea
Captain: Naam kaka, mzigo haujaletwa. Tafadhali ileteni tu hiyo hela ya watu kaka. Napewa lawama, isitoshe we ni ndugu yangu usikubali hela ndogo iharibu.
Matonya: Gadner haiwezi kuwa hivyo, kuna mapungufu kidogo nayaweka sawa uipate. Kumradhi sana blaza.
Captain:  Asante
Pamoja na kukubaliwa kutoshiriki shoo hiyo kutokana na sababu alizojitetea, Matonya bado hajarejesha fedha za kianzio alizolipwa kwa ajili ya shoo hiyo hali ambayo inaleta mtafaruku mwingine licha ya kuwa alisisitizwa kurejesha

No comments:

Post a Comment