Wednesday, April 10, 2013

ZIFF YAKERWA NA USHIRIKI MDOGO WA FILAMU ZA TANZANIA






Waandaaji wa tamasha la kimataifa la filamu la Zanzibar, ZIFF wamedai kusikitishwa na muitikio hafifu wa waigizaji wa filamu Tanzania katika kuwasilisha filamu zao.


Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, ZIFF imedai iliitisha upokeaji wa filamu kwaajili ya tamasha la 16 la nchi za Jahazi Septemba 2012 na kuweka mwisho wa kupokea kuwa ni tarehe 31 Machi, 2013 lakini wamepokea filamu chache kutoka Tanzania ukilinganisha na za nje. Jumla ya filamu 200 zimeshawasilishwa mpaka sasa lakini filamu za Tanzania ni tano pekee.
Painkiller
“Filamu za Tanzania ambazo tumepokea mpaka sasa hazi zidi 5 ukijumla na zile zinazoingia katika uchaguzi wa jumla (General Selection) na zile kwajili ya Swahili Movie/Bongo Movie competition,” imesema taarifa hiyo.

“Tukumbuke filamu hizi ndio zitatoa Filamu Bora ya Kitanzania na pia kugombea Filamu Bora ya Afrika Mashariki na maeneo mengine Tumekuwa wavivu wa kusoma websites, blogs na hata magazeti kwa kutegemea kupata taarifa za mdomo au taarifa kwa mtu mmoja mmoja ili kujua nini kinaendelea, jambo ambalo si sahihi, tujifunze kupitia vyombo vya habari ili tupate habari kwa wakati muafaka,”imeendelea kusema taarifa hiyo iliyoandikwa meneja wa tamasha hilo, Daniel Nyalusi.

“Hivyo basi natoa nafasi mpaka tarehe 15 Aprili, 2013 filamu zote za Kitanzania ziwe zimetumwa ZIFF au kupatiwa Ndugu Ibrahim Mitawi (Outreach Officer) – Dar es Salaam (0713-300997) au Mohamed (Film Coordinator) – Zanzibar (0718115468).”

No comments:

Post a Comment