Wednesday, April 10, 2013

IRENE UWOYA AFUNGUKA KUHUSU KUFUMWA HOTELINI AKIWA NA DIAMOND!




Baada ya habari nyingi sana kuhusu Irene Uwoya kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Diamond platnumz kutawala vyombo vya habari na kwenye mitandao hapo juzi, hatimaye bongojunior blog iliamua kutafuta undani kuhusu mwanadada Irene Uwoya ili tuweze kufahamu juu ya tuhuma hizi za yeye kuingilia penzi lwa mwanadada Penny kwa kijana wa “mbongofleva” diamond platnumz.

Baada ya majaribio mengi ya kupiga simu yake ambayo ilikuwa haipatikani muda wote wa mchana baadaye kwenye mida ya saa kumi na mbili hivi jioni tuliweza kumpata hewani na Jibu lake lilikuwa moja tuu kuwa “achana nazo” na sisi tukaona kweli tuachane nazo ila tukufukishie wewe msomaji wetu mpendwa “response” hiyo ili mwenyewe uamue na kutafakari. Hilo ndo jibu alilotupa mwanadada mrembo wa bongo movies Irene Uwoya kuhusu tuhuma za yeye kutoka kimapenzi na msanii Diamond.

No comments:

Post a Comment