Thursday, October 17, 2013
Stay tuned and be sure to Subscribe to my YouTube channel @ Jerry Mushala. New Music video dropping out on 20th October, 2013
Stay tuned and be sure to Subscribe to my YouTube channel @ Jerry Mushala.
New Music video dropping out on 20th October, 2013
Friday, September 13, 2013
CHUPI NA SHANGA ALIZOONYESHA SHILOLE ZAMFANYA ACHUKULIWE HATUA ZA KINIDHAMU...!!
Ijumaa, Septemba 13, 2013 shadrack masatu
MWENYEKITI wa Kamati ya Umoja wa Mashirikisho ya Sanaa Tanzania, Kimela Billa, ameutaka uongozi wa Shirikisho la Muziki Tanzania, kumchukulia hatua ya kinidhamu, msanii wa muziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kwa kosa la kukiuka maadili ya Tanzania katika tamasha la Serengeti Fiesta, mkoani Iringa.
Shilole alipanda jukwaani akiwa anacheza wimbo wake wa ‘Nakomaa na jiji’ huku akiwa amevaa nguo ambazo zinaonesha maumbile yake yote ya mwili.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Billa alisema Shirikisho la muziki chini ya rais wake, Addo Novemba wanatakiwa kuchukua hatua zaidi juu ya shilole kwa kosa la kuwadhalilisha wanawake ikiwa ni pamoja na kukiuka maadili ya Tanzania.
“Hatukatai hayo mambo yapo lakini kwa staili ile sisi kama viongozi wa sanaa hatutaweza kuvumilia, shirikisho la muziki wakishindwa kutekeleza hili lazima kamati ilivalie njuga swala hilo, kiukweli wanalidhalilisha taifa hawa wasanii, mbona wanaume hafanyi shoo zao uchi,? Alihoji Billa.
Alisema shirikisho la muziki liige mfano wa shirikisho la filamu kama lilivowaonya Wema Sepetu na Aunt Ezekiel kwa makosa kama hayo, ambapo anamini kwaasilimia kubwa kunachangia kuwa na nidhamu wanapopanda jukwaani.
“Angekua ameenda kwa shughuli za filamu wangelifanya wao lakini hili shirikisho la muziki wanatakiwa wakae meza moja na Shilole kulizungumzia hilo, wao wanakua wazito kuwachukulia hatua wasanii wa muziki kuliko filamu lakini kwa hili haitawezekana, ,” alisema.
Friday, July 5, 2013
Wednesday, July 3, 2013
MAHAKAMA YAWAACHIA HURU VIONGOZI WA CHADEMA BAADA YA MWIGULU NCHEMBA KUSHINDWA KUTHIBITISHA AINA YA TUSI ALILOTUKANWA
Mwita Waitara
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mjini Singida jana imetupilia mbali kesi iliyokuwa inawakabali viongozi wawili wa CHADEMA NduguMwita Waitara ambaye ni afisa sera na utafiti makao makuu na mshauri wa chama hicho Dk Kitila Mkumbo. Katika hukumu yake aliyeiyosoma mbele ya wakili wa washtakiwa hao Tundu Lissu, hakimu wa Mahakama hiyo Masham alisema kuwa washatakiwa hawana kesi ya kujibu kwa kuwa mashahidi wa serikali walishindwa kuthibitisha aina ya matusi yaliyodaiwa kutolewa na washtakiwa.
Aidha, hakimu huyo alisema kwamba upande wa serikali walishindwa kumleta shahidi muhimu katika kesi hiyo Mwigulu Nchembaaliyedaiwa kutukanwa ili athibitishe kwamba yeye ndiye aliyetukanwa na namna ambavyo matusi hayo yamemuathiri.
"Kushindwa kwa Mwigulu Nchemba kufika mahakamani ni kuonyesha kwamba ama hajui kwamba alitukanwa au hakuona kosa lolote alilotendewa na mahakama haiwezi kutoa uamuzi kwa mambo ya kuhisiwa".. alisema hakimu huyo.
Washtakiwa walidaiwa kutenda kosa hilo tarehe 14 Julai mwaka jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Ndago wilayani Iramba ambapo Chama cha Demokrasia na Maendeleo kilikuwa na mkutano wa hadhara.
Kesi hiyo imekuwa ikisuasua mara nyingi kwa upande wa serikali kushindwa kuleta mashahidi mahakamani na kusababisha kesi hiyo kuahirishwa mara kwa mara, jambo ambalo lilikuwa likimkera hakimu wa kesi hiyo.
MACHANGUDOA WAULAANI UJIO WA OBAMA....WANADAI HAUKUWA NA PESA IKILINGANISHWA NA ULE WA BUSH
Katika hali ilisiyokuwa ya kawaida, machangudoa wameulalamikia ujio wa Rais Barack Obama kwa kile kinachodaiwa kuwa haukuwa na faida yoyote kwa kukosa dili za pesa.
" Tumesikitishwa sana na ujio wa Obama kwani tulikuwa tumejipanga kupiga hela ndefu sana .
"Bahati mbaya watu wake tuliokuwa tunategemea kuwanasa walikuwa busy na wale wa mikoani walizuiwa"Walisema akina dada hao.
Machungudoa hao wanadai kuwa kipindi cha Bush alipokuwa Rais ambaye alikaa nchini karibu wiki moja walinufaika sana ambapo wengi wao walijenga majumba kwa pesa za ziara ya Bush ."Bahati mbaya watu wake tuliokuwa tunategemea kuwanasa walikuwa busy na wale wa mikoani walizuiwa"Walisema akina dada hao.
MAMA WA MIAKA 52 AKAMATWA KWENYE CHUMBA CHA MTIHANI AKIMFANYIA MTIHANI BINTI YAKE
Mwanamke mmoja mfaransa (52) amejikuta mikononi mwa polisi wa jiji la Paris katikati ya mwezi june, baada ya kukamatwa kwenye chumba cha mtihani akimfanyia mtihani wa Kiingereza mwanae mwenye umri wa miaka 19, huku akijiweka kisichana zaidi wasimshutukie.
Ripoti kutoka nchini humo zinasema mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la Caroline D aliingia kwenye chumba cha mtihani akiwa amevaa skin jeans na viatu aina ya Converse ili aonekane kama mwanae.
Lakini jicho makini la msimamizi wa mtihani lilimnasa mama huyo kwa kuwa msimamizi alikua tayari alishamuona mwanae wakati anafanya mtihani wa Philosophy, kwa hiyo akamshtukia mama huyo kwa muonekano wake na sura yake ya kiutu uzima.
Msemaji wa Polisi wa Paris alisema mwanamke huyo alikiri makosa yake ya udanganyifu na kusema kuwa kiukweli yeye alikuwa anaweza zaidi Kiingereza zaidi ya mwanae.
Mwanamke huyo anakabiriwa na mashtaka ya udanganyifu na anaweza kulipa fine isiyopungua £7,000.
Lakini pia binti yake anaweza kupata msala wa kuzuiwa kufanya mtihani wowote wa kitaifa kwa muda wa miaka mitano.
"GEREZANI KUMENIFANYA NIMJUE MUNGU VIZURI SANA"....HII NI INTERVIEW YA LULU MICHAEL
Kwa mara ya kwanza muigizaji wa filamu, Elizabeth Michael aka Lulu jana alifanya interview ya kwanza tangu atoke gerezani January mwaka huu.
Lulu aliye na muonekano wa ‘udada’ zaidi alihojiwa jana kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV kinachoendeshwa na Zamaradi Mketema.
Katia interview hiyo, Lulu aliongea masuala mengi kuhusu maisha yake ya sasa, mipango yake na mengine lakini akidai kuwa hatopenda kuongelea suala la uhusiano wake na Kanumba kwakuwa anahisi bado hajawa tayari ila muda ukifika atafunguka mengi. Haya ni baadhi ya masuala aliyoyazungumza.
Kuhusu uzinduzi wa filamu yake mpya Foolish Age
Ninaplan kufanya uzinduzi kwaajili ya movie yangu, lengo kubwa la kufanya uzinduzi ni kwamba kwanza nitajiskia vizuri kukutana na ‘okay these are my fans’ kukutana nao sehemu moja. Kuna vitu sitaweza kuongea kwenye interview ntahitaji kuviongea mwenyewe kama mwenyewe.
Nitahitaji watu waone baadhi ya vitu vilivyopo kwenye movie. Movie inaitwa Foolish Age. Nitaizindua chini ya kampuni ya Proen (????) Promotions Ltd na ni kampuni ambayo ndio inanimanage kwa sasa.
Kuhusu kama ana boyfriend aliyemnunulia vitu vya thamani
Watanzania wengi tulishajiwekea ile dhana kwamba ‘ukiona mwanamke amefanya kitu basi there is a man behind, yaani ni ile dhani ipo tayari ndani yetu kwahiyo hata kama mtu atastruggle kutafuta kitu chake mwenyewe lakini hiyo itakuwa ni ukweli wako na unaujua mwenyewe .
Kiukweli ni kwamba hakuna mwanaume yeyote ambaye amenifanyia chochote till now. Nachoshukuru tu ni menejimenti yangu, kampuni ambayo nafanya nayo kazi.
Ni kampuni ambayo inanijali, inajali kazi zangu, inajali msanii wao kwahiyo whatever I’m having, whatever I’m doing ni mimi mwenyewe, ni kazi zangu ni biashara yangu.
Uhusiano wake na Mama Kanumba na jinsi alivyompata kufanya naye movie ‘Mapenzi ya Mungu’
Kwa sasa hivi tupo kama familia kwa hiyo it wasn’t hard mimi kumpata na nilijisikia vizuri kama ntaweza kufanya naye kazi. Kuna spirit ambayo ilinivuta zaidi nifanya kazi na Mama Kanumba kuliko labda mama mwingine.
Anachomiss kwa Kanumba
Busara zake, he was a person ambaye akikuona unaenda hivi he takes you in the right way.
Kuhusu kwanini mapenzi yake na Kanumba yalikuwa siri
Ni makubaliano tu and there was no need like to let people know yaani kumfanya kila mtu ajue nadhani haikuwa na maana kwetu.
Kuhusu kwanini alinenepa alipokuwa gerezani
Labda kwasababu nilimwachia Mungu kila kitu, nilimkabidhi Mungu kila kitu so I had this peace of mind. Niliacha kwamba yeye ni msimamizi wa kila kitu. Let me confess kwamba gerezani kumenifanya nimjue Mungu vizuri sana,.
Kumenifanya nimjue na nimwamini na kumjua na kumwamini kumetokana kwamba kuna vitu vingi vimekuwa vinafanyika like naviona hivi kwa macho na naona kabisa kwamba hapa ingekuwa mimi kama mimi ama binadamu yeyote haiwezekani...
Tuesday, July 2, 2013
TAZAMA PICHA:TUZO ZA BILLBOARD AWARDS (BBMA) 2013 ZILIVYOFAANA JIJINI LAS VEGAS...!!
Selena Gomez & Taylor Swift...!! |
Akon akitumbuiza kwenye usiku wa Tuzo za Billboard...!! |
Nicki Minaj & Lil wayne wakitumbuiza pamoja...!! |
Madonna akizungumza kwenye steji kuhusu madawa ya kulevya....!! |
Psy & Tracy Morgan wakifanya yao jukwanii...! |
Sky Blue akitumbuiza Jukwaa moja na Wiz Khalifa....!!picha zote na dj sek |
Justin Bieber akitumbuiza stejini...!! |
Will.Iam akizungumza jukwanii...!! |
Msanii mkongwe Prince akitumbuiza jukwanii...!! |
Taylor Swift akitumbuiza jukwanii...!! |
Taylor Swift akipokea Tuzo usiku wa Tuzo za Billboard...!! |
Nicki Minaj akipokea Tuzo...!! |
Chris Brown Akitumbuiza...!! |
Bruno Mars kwenye Stage....!! |
Tracy Morgan ndio aliehendesha Shuguli nzima ya Tuzo hizo..!! |
Kelly nae alikuwepo kwenye usiku huo wa Tuzo za Billboard |
Madonna & Wil-Iam wakiwa jukwani kuwakilisha Tuzo..!! |
Serena Gomez akiwajibika stejini...!! |
Taylor Swift akipokea Tuzo...! |
Justin Bieber akizungumza baada ya kupokea Tuzo...!! |
Pitbull akitumbuiza...!! |
Jennifer Lopez akifanya yake stejini..... |
Celline Dion akizungumza kwenye usiku wa Tuzo hizo za Billboard kama mkongwe kwenye muziki wa Marekani...!! |
David Guetta akitumbuiza jukwaani pembeni akiwa na Akon mkono wa kushoto na kulia kwake ni Ne-Yo |
David Guetta akizungumza baada ya kupokea Tuzo... |
Lil wayne a.k.a Tunechi akiwa stejini.... |
Nicki Minaj & Lil wayne kwenye jukwaa wakitumbuiza kwa pamoja...!! |
Ne-Yo akitumbuiza jukwani kwenye usiku wa Tuzo hizo za Billboard 2013 |
Subscribe to:
Posts (Atom)