Tuesday, April 30, 2013

DOTNATA AWEKEWA TEGO LA SUMU KWENYE JUICE.....



Husna-Poshi-533-K

Muigizaji wa filamu nchini Dotnata Rubagumya anadai kuwekewa sumu kwenye juice na mtu asiyemfahamu ambayo imemsababishia matatizo makubwa ya kiafya.


Amesema alianza kuhisi kupandwa na pressure ambapo alilazwa kwenye hospitali ya IMTU na kuambiwa imepanda hadi kufikia 284 huku wakimweleza huenda ni kwakuwa amenenepa sana.Baadaye alifanyiwa uchunguzi wa moyo kwenye hospitali ya Lugalo kabla ya kupelekwa TMJ kwa vipimo zaidi.
 
Anasema tatizo hilo lilimsabisha ashindwe kuhema, sauti kukata na mara nyingi alikuwa akitapika.
 
“Nimezidiwa usiku wa kuamkia Jumatano nikakimbizwa tena TMJ ndo sasa ikabidi wanichunguze kwa makini kwanini nakuwa hivi ndo wakagundua nimelishwa sumu takriban mwezi wa nane sasa huyo mtu aliyenipa sumu aliipitisha kwa njia ya juice,” amesema Dotnata ambaye kwa sasa ameokoka.
 
Akizungumzia sababu za kuwekewa sumu, Dotnata amesema:
 
“Kila mwanadamu ana mawazo jinsi anavyowaza katika akili yake labda hakupendezewa na mimi niendelea kuishi hivi, labda alifikiria akiniua mimi yeye hatokufa. Lakini natamka wazi kwamba sitokufa nitaishi ili niyasimulie mema ya Mungu. 

 Nimejifunza mtu anaweza kuwa rafiki yako kumbe ndio mbaya wako siwezi kujua ni kwasababu gani, namwachia Mungu.”

"TUNALAZIMIKA KUTUMIA 0718 TUKIWA KATIKA SIKU ZETU HUKU POLISI NAO WAKITUINGILIA KWA NGUVU"....MAKAHABA


Jana CLOUDS FM iliripoti kuhusu kushamiri kwa Biashara ya Ngono katika Maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam  na  jinsi  serikali  inavyolishughulikia  tatizo  hilo  linalokua  kwa  kasi....

Wakihojiwa  kwa  nyakati  tofauti, baadhi ya wasichana wanaojishughukisha na biashara hiyo wameelezea changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika kazi hiyo hususani nyakati za usiku.

Wakizungumzia adha wanazokutana nazo Wasichana hao wamesema kuwa licha ya kukabiliwa hali ngumu ya maisha iliyopelekea kuingia katika biashara hiyo, bado wamekuwa wakikutana na matukio mabaya ikiwemo kukamatwa na kuingiliwa kinguvu na baadhi ya watu wanaojitambulisha kwao kuwa ni askari wa Polisi jamii. 

Mbali na hilo Wasichana hao wamesema hali ngumu ya Maisha imekuwa ikiwalazimu kufanya mapenzi kinyume na maumbile wanapokuwa kwenye Hedhi, pasipo kujali hatari ya kukumbwa na maradhi yoyote. 


Hivi karibuni Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni lilitangaza mpango wa kuwaondoa wasichana wamaojishughulisha na Biashara ya ngono mitaani na kuwashtaki kwa mujibu wa Sheria ya makosa ya uvunjifu amani na ukiukwaji wa maadili.
 



Wakizungumza baadhi ya wadau kutoka mashirika na Taasisi mbalimbali za kutetea haki za Binadamu nchini, ambapo kituo cha Sheria na haki za Binadamu pamoja na taasisi ya kutetea haki za Binadamu ya Chuo Kikuu cha Tumaini, kimesema kuwa kitendo cha kuwakamata wasichana hao hakiwezi kuwa suluhisho la kutokomeza Biashara ya ngono nchini.

 
Eneo la MANZESE Uwanja wa Fisi ni miongoni mwa Maeneo ambayo Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam limeliainisha kuwa limekuwa likikithiri kwa Biashara hiyo

HAMMER Q AMTOA MANUNDU MKEWE BAADA YA UTAMBULISHO WA TX MOSH


I


Baadhi ya picha za mkewe baada ya kipigo






Nguo za Hammer Q zikiwa zimetapakaa damu



Hiki ni kipigo ambacho  Salha  alikipata baada ya kumtambulisha rafiki yake wa kiume ambae ni Tx Moshi kwa mumewe Hammer Q.

Baada  ya  utambulisho  huo....sinema  ya  ngumi  na  mateke  ilianza....
Inavyosemekana alimpiga mateke, mangumi, akampasulia kioo kichwani, kampiga na jiko la mkaa kichwani

Monday, April 29, 2013

Jihadhari Kufanya Ngono Kwenye Fukwe za Bahari Dar-Ona Hawa Wamekamatwa Coco Beach Wakifanya yao






NI aibu sana! Ndivyo unavyoweza kusema juu ya Oparesheni ya Fichua Maovu iliyosimamiwa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar, OCD Wilbroad Mutafungwa na Ofisa wa Oparesheni, Inspekta Jacob Swai kwa kushirikiana na Global Publishers iliyonasa wanawake wanaojishughulisha na mambo ya ngono usiku kucha.

Katika oparesheni hiyo iliyofanyika usiku wa Jumapili iliyopita watu kibao walinaswa hasa katika Ufukwe wa…

NI aibu sana! Ndivyo unavyoweza kusema juu ya Oparesheni ya Fichua Maovu iliyosimamiwa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar, OCD Wilbroad Mutafungwa na Ofisa wa Oparesheni, Inspekta Jacob Swai kwa kushirikiana na Global Publishers iliyonasa wanawake wanaojishughulisha na mambo ya ngono usiku kucha.

Katika oparesheni hiyo iliyofanyika usiku wa Jumapili iliyopita watu kibao walinaswa hasa katika Ufukwe wa Coco, jijini Dar akiwemo bibi harusi mmoja na mtoto wa kigogo (jina linahifadhiwa).

BIBI HARUSI LAIVU KWENYE BAJAJ
Kwenye ufukwe huo, mwanamke mmoja ambaye jina halikupatikana, aliyedaiwa kufunga ndoa Ijumaa iliyopita, naye alikamatwa katika msako baada ya kunaswa na mwanaume wakifanya ngono kwenye Bajaj.

Katika tukio hilo, mwanaume alifanikiwa kutoka nduki huku akimwacha demu wake akijikusanya kwa kuvaa nguo.
Mwanamke huyo naye alifanikiwa kuwatoka askari hao na kukimbilia chooni ambapo aliwakuta wanawake wengine waliojificha hivyo wakakamatwa wote kwa pamoja.
Ili kuweka ushahidi, askari hao wa kazi waliikamata Bajaj hiyo.

ALIKWENDA KUKUMBUSHIA ENZI ZAKE
Kwa mujibu wa mwanamke huyo, mkazi wa Kinondoni-Manyanya, usiku huo alifika mahali hapo kukumbushia enzi zake kabla ya kuolewa ambapo ilidaiwa kwamba alikuwa akijiuza ufukweni hapo.
Alijitetea kuwa mume wake alisafiri hivyo akaona akakumbushie enzi zake kabla hata ‘hina’ aliyopakwa wakati wa harusi haijafutika mwilini.
Pamoja na maelezo hayo, mwanamke huyo aliishia kwenye ‘difenda’ la polisi tayari kwa kupelekwa kituoni kwa maelezo zaidi.

BINTI WA KIGOGO
Katika kundi hilo la wanawake na wanaume zaidi ya hamsini waliokamatwa ufukweni hapo usiku huo wa saa 9 na ushee, kulikuwa na mtoto wa kigogo mmoja serikalini katika idara nyeti ambaye alinaswa mchangani baharini akiwa kwenye kundi la makahaba.
Mtoto huyo aligundulika kuwa ni binti wa mnene wakati wa kutoa maelezo kituoni Oysterbay.

MASIKINI ALIKUWA NA ‘BOIFRENDI’ WAKE
Akijitetea wakati wa kutoa maelezo, binti huyo aliyeonekana mrembo na mwenye mvuto wa ajabu, alisema kwamba alikuwa na ‘boifrendi’ wake na kuwa alitoroka kwao usiku huo.
Binti huyo aliomba chondechonde asipigwe picha kwani endapo itaonekana gazetini basi atakuwa amejipalia makaa nyumbani kwa vile hataeleweka kwa sababu anapatiwa fedha za matumizi pamoja na ada ya shule.
Ukiacha mwanamke na binti huyo wa kigogo, wanawake wengine wengi walikamatwa, wengi wao walikutwa wakifanya vitendo vya ngono mchangani wakiwa ‘pea’.

MACHANGU WAFUNGUKA
Kati ya wote waliokamatwa, wanawake kumi na tano walikiri kujishughulisha na biashara ya kuuza miili ambapo walisema wanafanya hivyo kutokana na ugumu wa maisha.
ACD MUTAFUNGWA ANASEMAJE?
Kwa upande wake OCD Mutafungwa alisema wameamua kuyafanyia kazi malalamiko ya wananchi kwa kuvamia eneo hilo.

INSPEKTA SWAI ATIA NENO
Naye Inspekta Swai aliyekuwa ‘front’ katika zoezi hilo alisema kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu kila wiki ili kukomesha vitendo viovu katika ufukwe huo.

JB ATANGAZA NIA YAKE YA KUGOMBEA UBUNGE MWAKA 2015........HIKI NDO ALICHOKISEMA




HATIMAYE nguli wa sanaa za maigizo Bongo, Jacob Stephen Mbura ‘JB’ amelianika jimbo atakalogombea ubunge mwaka 2015.


JB aliyaongea hayo mwanzoni mwa wiki hii, jijini Dar es Salaam ambapo alisema macho yake yote yapo Mkoa wa Dar es Salaam ambao una majimbo nane.


JB: Niliposema natangaza kugombea ubunge mwaka 2015 wengi waliamini ni maneno tu, lakini nia yangu ni sahihi. Nitagombea na leo nasema jimbo langu lipo Mkoa wa Dar es Salaam.


Aliongeza kuwa, jimbo atakalogombea litaendelea kubaki kuwa siri ya moyo wake na meneja wake wa kampeni ambaye hakupenda kumtaja jina.


Majimbo yanaounda mkoa wa Dar es Salaam katika uwakilishi bungeni ni Ukonga, Ilala, Kinondoni, Segerea, Kawe, Kigamboni, Ubungo na Temeke.

MAANDAMANO MAKUBWA YANAENDELEA JIJINI ARUSHA BAADA YA GODBLESS LEMA KUACHIWA HURU




Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema ameachiwa kwa dhamana hivi punde baada ya kushtakiwa kwa makosa ya uchochezi katika mahakama ya Mkoa wa Arusha huku maandamano yakifanyika hivi sasa katika mitaa ya Jiji la Arusha, Tanzania.

Katika Mahakama hiyo kulikuwa na umati mkubwa wa wafuasi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Mashabiki, wafuasi na wanachama wa chama hicho walifurika katika mahakama hiyo kwa ajili ya kumuunga mkono mbunge huo.habarimasai.com itaendelea kukuletea Taarifa zaidi baadaye.
 
Hivi sasa mashabiki, wafurukutwa na wanachama wa Chadema wanafanya maandamano makubwa kuelekea katika ofisi za chama hicho ambazo zipo katika eneo la Ngarenaro.

Hivi sasa wanapita katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mulongo kwa maandamano huku wakipiga kelele za kuzomea.

Kesi ya uchochezi dhidi ya Lema imefunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Mkoa wa Arusha na endeshwa na Hakimu Devota Msoffe.

Mwandishi wetu anasema kwamba kesi hiyo imeahirishwa mpaka Mei 29 mwaka huu. 

Katika hati ya mashtaka ambayo ipo katika mahakama hiyo inasema kwamba kosa la Lema ni ' kutoa maneno yanayodaiwa kuwa ni uchochezi. 

Endelea kuwa nasi  kwa taarifa moto moto.

PADRI WA KANISA KATOLIKI HUKO MOSHI AFUMANIWA LIVE NA MKE WA MTU AKIWA UCHI WA MNYAMA



KANISA Katoliki Jimbo la Moshi limeingia katika kashfa nzito baada ya padri wake, Father Urbanus Ngowi wa moja ya parokia zake kudaiwa kufumaniwa na mwanamke anayesemekana ni mke wa mtu

Father Ngowi akiwa ameduwaa baada ya kufumaniwa akiwa na mke wa mtu aliyejulikana kwa jina la kijamii la Mama P.
Sakata la fumanizi hilo linadaiwa kutokea Jumatatu ya wiki iliyopita chumbani kwa padri huyo, Marangu Wilaya ya Moshi  Vijijini ambako Father Ngowi inasemekana alikutwa ‘laivu’ akiwa na mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la kijamii la Mama P.

Pamoja na kunaswa huko, vyanzo havijaeleza humo chumbani wawili hao walikuwa wakifanya nini!


Habari zinadai siku ya tukio, mwanamke huyo aliingia nyumbani kwa padri huyo ambapo baadhi ya ndugu wa mumewe walikuwa wakimfuatilia baada ya madai yaliyokuwepo kwamba ana ukaribu wenye maswali mengi na mtumishi huyo wa Mungu.


“Unajua siku nyingi ilivuma kwamba Mama P na Father Ngowi wana ukaribu wenye maswali mengi, mume wake alifuatilia na kubaini ni kweli lakini akashindwa kuutenganisha ukaribu wao,” kilidai chanzo.

Father Ngowi akijaribu kuomba samahani baada ya kufumaniwa.

Chanzo kikaendelea kudai kwamba baada ya kuona mkewe amejikita kwa mtumishi wa Mungu, mumewe alinyoosha mikono juu na kumwachia Mungu.

Chanzo: Sasa siku hiyo baada ya ndugu wa mume kumfuatilia mpaka anaingia kwa Father Ngowi, wakaona ni bora watafute mpigapicha ili kupata picha za tukio ambazo zitakuwa ushahidi siku za mbele.


“Walipompata wakazama ndani, sekeseke likaanzia hapo. Walimkuta mwanamke huyo na mtumishi wa Mungu wapo kitandani.”

 
Father Ngowi na Mama P wakivaa nguo zao kwa aibu baada ya kufumaniwa.

Habari zinadai kwamba kufuatia tukio hilo, tayari Kanisa Katoliki limemweka kitimoto padri huyo ambaye alikuwa akihudumu katika Parokia ya Korongoni, Moshi Vijijini kabla ya kuhamishwa na kupelekwa Parokia ya Makomu, Marangu ambako inadaiwa ameshushwa cheo.


Inadaiwa kuwa baada ya tukio hilo, Father Ngowi alikana kukutwa na mke wa mtu chumbani kwake lakini alipobanwa sana na mabosi wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki Moshi, alikiri na kudai ibilisi alimpitia na kuomba kanisa limsamehe na kutompa adhabu kali ambayo itamuathiri kisaikolojia.


Hili ni tukio kubwa na la aina yake kuwahi kulikumba Kanisa Katoliki nchini kwa padri wake kudaiwa kukutwa na mke wa mtu chumbani kwake!

Father Ngowi na Mama P wakiwa na nyuso za aibu baada ya tukio hilo.

Kuna madai kwamba mwaka jana (2012), Father Ngowi, mbele ya waumini wake alisoma barua yenye kukana shutuma zote zilizoelekezwa kwake kwamba amekuwa na ukaribu wenye maswali mengi na wake za watu.


Taarifa zilidai kuwa padri huyo aliweka wazi akisema si kweli kwamba amekuwa na ukaribu unaotajwa, akawataka waumini wake wapuuze tuhuma hizo alizosema  zina mwelekeo wa kuchafua sifa yake na taswira ya Kanisa Katoliki kwa jumla.


Hayo ni madai ya vyanzo vyetu ambavyo viliambatanisha na picha mbalimbali za tukio hilo lenye kushtua waumini sambamba na namba za simu za padri huyo kwa ajili ya mawasiliano ili kujiridhisha.

 Father Ngowi akipatiwa suruali yake.

KITENDO CHA WANAWAKE KUNYONYANA NDIMI HUKU WAKIWA NUSU UCHI KIMEMFANYA PREZZO AIPITIE UPYA VIDEO YAKE




Inaonekana baadhi ya vituo vya runinga nchini Afrika Kusini, zikiwemo Channel O na Soundcity zimetaka video mpya ya Prezzo, Liqher ifanyiwe marekebisho kadhaa ili vianze kuicheza.
Prezzo 5

Hiyo ni kwa mujibu wa mawasiliano kwenye mtandao wa Twitter kati ya msichana aitwaye Tricia Stever anayetumia jina GOLDIE 4EVER GOLDEN aliyetaka kufahamu kwanini video hiyo haioni ikichezwa kwenye vituo hivyo.

“Pls y is d video for #liqher not being shown on soundcity, channel o n other music channels @amb_prezzo #justcurious,” aliuliza msichana huyo jana.
Prezzo akiwa kwenye jacuzzi
Prezzo akiwa kwenye jacuzzi
Wanawake wakionesha vitendo vya usagaji
Wanawake wakionesha vitendo vya usagaji
Wanawake wakinyonyana ndimi kwenye video hiyo
Wanawake wakinyonyana ndimi kwenye video hiyo
Prezzo 5
Prezzo alijibu, “Working on it, had 2 make sme changes……if u know wht I mean.”

“Yeah i understand but pls try n hasten it up, cos dat video is dope n d whole of africa need to watch it,” alitweet Tricia.
prezzo 2
prezzo 3
Prezzo 4
Video ya Liqher inamuonesha Prezzo katika baadhi ya scenes akiwa kwenye Jacuzzi na wasichana walio nusu utupu na wengine wakinyonyana ndimi.

 Katika sehemu zingine anaonekana msichana mrembo akijig’ata vidole vyake kimahaba na hivyo kuamsha hisia kali .

Sunday, April 28, 2013

Nassari Akiwa na Lema Mahabusu



Kushoto ni Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akiwa katika chumba alikohifadhiwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.Dar es Salaam, Tanzania. Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari LEO amemtembelea Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ambaye yuko mahabusu baada ya kutiwa mbaroni na Jeshi la Polisi, mkoani Arusha, Tanzania.

Nassari pamoja na mambo mengine amemtembelea Lema ili kujua kilichotokea wakati akizungumza na wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu  Arusha (IAA) na baadaye kukamatwa na polisi.

Mbunge huyo Arumeru Mashariki amewasili Leo Arusha na kwenda moja kwa moja katika Kituo Kikubwa Cha Polisi (Central).

Jana Nassari alinukuliwa akisema kwamba Leo yeye na Halima Mdee (Kawe) watakutana na kuzumgumza na Mulongo kuhusu

kilichotokea katika chuo hicho cha uhasibu na kusababisha kukamatwa kwa Lema.

“Jumatatu (leo) tunatarahia kuonana na mkuu wa mkoa na tayari nimempa taarifa. Tunataka kuzungumza  naye kilichotokea na hali ya kisiasa  iliopo Arusha hivi sasa,” alisema Nassari.

Mpaka sasa haijafahamika Nassari amezungumza nini na Lema.

BAJETI KIPORO WIZARA YA MAJI YATINGA TENA BUNGENI LEO





Mkutano wa 11 unaendeleo leo mjini Dodoma, ambapo Bajeti ya Wizara ya Maji iliyokwama kupitishwa baada ya wabunge kuigomea, inatarajiwa kuwasilishwa, ikiwa na  maboresho, hususani eneo la nyongeza ya fedha katika miradi ya maji.

Bajeti hiyo ilitarajiwa kupitishwa tangu Alhamisi wiki  iliyopita, lakini kutokana na ufinyu wa fedha zilizotengwa, takribani wabunge wote waliochangia mjadala wake, wakiwemo wa CCM, waligoma kuiunga mkono.
 
Kutokana na hali hiyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda alisema suala la maji haliwezi kufanyiwa utani na kuitaka Wizara ya Maji, Kamati ya Bajeti na Wizara ya Fedha, kufanyia kazi suala hilo na walete majibu ya uhakika.
 
Leo wabunge hao wanatarajia upande wa Serikali kuwasilisha bajeti hiyo, ikiwa na maboresho mapya ya nyongeza ya fedha za miradi inayotarajiwa kufikia zaidi ya Sh milioni 185, ambazo wabunge hao walipendekeza ili kutekeleza miradi ya maji na kupunguza tatizo la maji katika maeneo yao.
 
Wakati akiiwasilisha makadirio ya bajeti hiyo wiki iliyopita bungeni, Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe, alibainisha kuwa Wizara hiyo imetengewa Sh bilioni 398, fedha ambazo wabunge hao walibainisha kuwa hazitoshi, ikilinganishwa na mahitaji makubwa ya maji nchini.
 
Wakati akiahirisha mjadala huo wa Bajeti ya Maji, Spika alisema: “Naona sasa mahitaji ya wabunge wote na wananchi kwa ujumla ni bajeti hii, kwa kweli iboreshwe ili kufikia malengo stahiki katika maeneo yetu.”

Viongozi wa Wizara ya Fedha, Kamati ya Bajeti na Wizara ya Maji, kwa takribani siku tatu, walikutana na kujadili suala hilo na namna ya kupata fedha za kuongezea kwenye bajeti hiyo, huku wabunge wa CCM nao wakikutana ili kuwekana sawa, kutokana na kilichotokea bungeni kuhusu bajeti hiyo.

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe, alipongeza hatua za wabunge hasa wa CCM, kuweka itikadi zao pembeni na kuungana pamoja kuikataa bajeti hiyo, ambayo haikuwa na mfumo mzuri wa kumaliza tatizo la maji nchini.
Hata hivyo, alipendekeza leo Serikali ije na maboresho yatakayoainisha namna ya kutekeleza Mpango wa Miaka Mitano wa Maendeleo, uliozinduliwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete, ambao katika eneo la maji utahitaji Sh bilioni 500.

Pamoja na mjadala wa Bajeti ya Maji kuendelea leo, pia Wizara ya Maliasili na Utalii, inatarajiwa kuwasilisha bajeti yake ya mwaka 2013/2014, itakayojadiliwa kwa siku mbili, ambapo wabunge wengi wanatarajia kuzungumzia suala la mgogoro wa ardhi Loliondo.

Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria nayo inatarajiwa kuwasilishwa kesho huku suala la Mabaraza ya Katiba likiwa ajenda kuu, iliyopaniwa kujadiliwa hasa na wapinzani, ambao wamekuwa wakilalamikia mchakato wake wa uchaguzi, kwamba umekuwa ukitawaliwa zaidi na masuala ya siasa.

Katika wiki hii, bajeti nyingine itakayojadiliwa ni ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), ambayo itajadiliwa kwa siku moja.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA TAASISI YA 'CONFUCIUS' YA CHUO KIKUU CHA DODOMA




 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya 'Confucius' ya Chuo Kikuu cha Dodoma, ambayo ni maalumu kwa ajili ya kufundishia Lugha na Tamaduni za Kichina. Uzinduzi huo umefanyika jana Chuo Kikuu cha Dodoma.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti cha kuhitimu mafunzo ya Lugha ya Kichina, mmoja kati ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Jamillah Dauda, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya 'Confucius' ya Chuo Kikuu cha Dodoma, ambayo ni maalumu kwa ajili ya kufundishia Lugha na Tamaduni za Kichina. Uzinduzi huo umefanyika jana Chuo Kikuu cha Dodoma. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma, Prof. Idrs Kikula.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipongezana na Balozi wa China nchini Tanzania, Lu Youqing, baada ya kuzindua rasmi Taasisi ya 'Confucius' ya Chuo Kikuu cha Dodoma, ambayo ni maalumu kwa ajili ya kufundishia Lugha na Tamaduni za Kichina. Uzinduzi huo umefanyika jana Chuo Kikuu cha Dodoma. Kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma, Prof. Idrs Kikula.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma, Prof. Idris Kikula, wakati akitembele kukagua majengo ya Taasisi ya 'Confucius' ya Chuo Kikuu cha Dodoma.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kuhusu Lugha na Tamaduni za Kichina, kutoka kwa Mkuu wa Taasisi ya 'Confucius', Zheng Xueyu, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi hiyo ya Chuo Kikuu cha Dodoma.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia michoro ya picha zinazochorwa na wanafunzi wa Taasisi ya Confucius.
 Makamu wa Rais Dkt. Bilal;, akiagana na baadhi ya viongozi wakati akiondoka eneo hilo baada ya uzinduzi rasmi.
 Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akitembelea kukagua ujenzi wa Chuo cha Afya kinachojengwa Chuo Kikuu cha Dodoma.
 Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi na viongozi mbalimbali.
Picha ya pamoja.