Wednesday, April 10, 2013

"JAPOKUWA SIJAONA MSANII ANAYENIFIKIA KWA HELA NINAYOPATA KWENYE RINGTONE LAKINI UKWELI NI KWAMBA WASANII TUNANYONYWA"...DIAMOND





Suala la wasanii kunyonywa na makampuni ya simu kwenye mauzo ya ringtone linamuuma kila msanii, hata Diamond ambaye ndiye msanii anayeingiza fedha nyingi zaidi kuliko yeyote Tanzania katika biashara hiyo.


Jana kupitia Instagram, aliandika kilio chake:

Dah! hivi kweli Serikali imekosa majibu ya swali la mh: Mbunge kuhusu mapato ya biashara ya ringtones..!? Kweli sasa naanza kuamini kuwa Serikali Inatukumbatiaga tu kwa Mda mfupi na kututumia Wasanii kwenye Kampeni zao kwa Maslahi yao Binafsi, kisha wanatudump baada ya kufanikiwa kwenye uchaguzi wao, bila kujali thamani na Mmhango wetu kwao.

Hata hivyo kuna watu wanaoamini kuwa Diamond hapaswi kulalamika kwakuwa ndiye msanii anayefaidi zaidi matunda ya muziki Tanzania.

Mmoja wa followers wake aitwaye Princestepp aliandika: Hupaswi kulaumu wewe maanake kati ya wasanii wachache walioweza kula hela za watanzania chini ya ya serikali ya rais wetu Kikwete ni wewe acha unafiki wasanii wengine ambao hawajapata fursa kama yako walaumu vipi sasa?

Diamond alijibu: Mi nimekula pesa na bado nakula pesa kwa juhudi zangu za kujituma jukwaani na kufanya show nzuri, sio kuwa naitwa kupewa pesa za ringtones nah! Napewa show…. So nikiwa kama mfano mzuri kwa wasanii lazima niwe mstari wa mbele kupigania haki za wasanii kiujumla. 

Aliongeza, “Mi napigania haki zetu upande mwingine wananiona snitch.. wakati mi naamini katika wasanii wote japo nadhulumiwa lakini hakuna hata anayefikia hela nnayolipwa kwa rintones.. ila naona haiwezekani kwanini watufanye wajinga watu wapewe haki zao.”

No comments:

Post a Comment