Saturday, May 4, 2013

Jack Wolper Aijutia Historia yake ya Mapenzi



DIVA wa kiwango cha juu cha filamu hapa Bongo, Jacqueline Wolper, ameonekana kujutia historia yake ya kimapenzi baada ya kufungukia kitendo cha yeye kumuanika kila aliyekuwa akimpenda kwamba kimemtibulia na sasa amejifunza kutokana na makosa.
Jacqueline Wolper.

Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Wolper alisema kuwa, kwenye maisha yake ya huko nyuma ameshajianika akiwa na wapenzi tofauti lakini sasa atakayempa nafasi kwenye moyo wake hatamuanika ila hilo litakuja baadaye sana kwani sasa hivi kaweka pembeni kwanza mambo ya mapenzi.
“Sitaki yajirudie yaliyotokea katika maisha yangu ya huko nyuma, hata hivyo sasa hivi niko bize sana na kazi, mambo ya wanaume nimeamua kuyaweka pembeni kwanza,” alisema Wolper na kuongeza:
“Sitaki itokee kama ilivyokuwa kwa Dallas ambapo kila mtu alijua alikuwa ni mtu wangu, kwa sasa nimeamua kutulia kwanza na hata nikimpata mwingine watu hawatamjua hadi wakati wa ndoa.”

No comments:

Post a Comment