Saturday, May 4, 2013

ROSE NDAUKA KAAMUA KUTAFUTA MAWAZO YA WATOTO WA MITAANI ILI KUBORESHA FILAMU ZAKE, HIKI NDICHO ALICHOKISEMA




MSANII wa filamu nchini Tanzania Rose Ndauka azidi kujizolea umaarufu na kuongeza mashabiki wa aina zote kwa kuwa karibu na watoto wa mitaani hususani katika matembezi yake ya kila siku

Msanii huyo ambaye anajitahidi kujitofautisha na baadhi ya wasanii wengine wa filamu nchini kwa kuwa karibu na jamii yake kwa vitendo hususani watoto hao wa mitaani

Akizungumza jijini Dar es Salaam Ndauka alisema kuwa katika maisha yake hususani kwa kipindi hiki ambacho yeye ni supar staa anathamini watoto wa aina yote kwani hao ndio moja ya mashabiki wake

Alisema kuwa anawathamini watoto hao hali inayomsababisha kutembea kwa miguu ili kila anapokutana nao apate nafasi ya kuzungumza nao na kubadilishana nao mawazo kwa kufanya hili anaamini kuwa anaongeza mashabiki wake na kuwafanya watoto hao kuwa karibu nao

Ndauka ambaye anaamini watoto wa mitaani wanahitaji upendo wa kila mmoja anayemzunguka alisema kuwa ni jukumu lake na nafsi yake inamsukuma kufanya hivyo ili kuzidisha upendo na kuwafanya wahisi ni sehemu moja ya jamii

Aliongezea kuwa kila anapokutana na watoto hao anahisi faraja moyoni mwake kwani hiyo ni sehemu ya kitu anachokipenda na nyakati za siku ya mapumziko hutumia muda wake mwingi kutembea kwa ajili ya kuwaona watoto na kupata mawazo yao ambayo anayatumia katika kuboresha filamu zak

No comments:

Post a Comment