Tuesday, April 2, 2013

LADY JAYDEE AAMUA KUFUNGUA KITUO CHAKE CHA REDIO BAADA YA KUCHOSHWA NA MANYANYASO YA CLOUDS FM




Hatimaye tumepata jibu la kwanini Judith Mbibo aka Lady Jaydee amekuwa akitweet vitu vizito weekend iliyopita. Kama hukufaniwa kuziona tweets hizo ni kwamba mwanadada huyo alishusha mfululizo wa mabomu kuelekea kwa kituo kimoja cha radio na kujikuta akiongeza aka mpya, Anaconda.

Na sasa imebainikiwa kuwa mwanamuziki huyo mkongwe na mjasiriamali anakuja na kituo chake cha radio kiitwacho Kwanza FM. Habari hiyo aliibreak mwenyewe jana na bila shaka haihusiani na April’s Fools Day.

    Kwanza FM coming soon. Yangu mwenyewee

    — Lady JayDee (@JideJaydee) April 1, 2013


Inaonesha kuwa mchakato wa kuanzisha radio hiyo unaenda vizuri kiasi cha kuweka wazi na kuwa hiyo ndio sababu alichukua uamuzi huo wa kuandika mambo ambayo yangeweza kuiharibu career yake ya muziki.

    Huwezi kuanza mapambano km hujajizatiti, si utapigwa ufe.? Vita ni pale tu unapokuwa tayari. Sikuwa tayari huko nyuma ndio maana sikuongea

    — Lady JayDee (@JideJaydee) April 1, 2013

Kila lakheri Lady Jaydee. Kwa usimamizi wa mumewe Gadner G Habash ambaye ana uzoefu mkubwa kwenye masuala ya radio, kituo hicho huenda kikafanya vizuri.

Monday, April 1, 2013

SAKATA LA MTOTO ALIYELAZIMISHWA KULA MBEGU ZA KIUME




Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka tisa (jina linahifadhiwa), amefanyiwa unyama wa kutisha na baba yake wa kambo kwa kunajisiwa, kulawitiwa na kulazimishwa kulamba mbegu zake za kiume.

Mtoto huyo anayeishi mkoani Pwani, imedaiwa ana hali mbaya kiafya kutokana na kudaiwa kufanyiwa kitendo hicho kwa muda wa miaka miwili.

Mwanaume anayedaiwa kufanya unyama huo amefahamika kwa jina la Adam Taliani maarufu kama `Kiredio' (37).

Inadaiwa kuwa baba huyo alikuwa akifanya kitendo hicho mbele ya mama wa mtoto huyo ambaye ni mke wake, akiwatishia kuwaua kwa panga kama watatoa siri hiyo.

Akisimulia mkasa huo, mama mdogo wa mtoto huyo Chiku Selemani alisema vitendo hivyo alianza kufanyiwa na baba yake wa kambo tangu mwaka 2011 wakati mama yake alipoanza kuishi na mwanaume huyo.

Alisema, waligundua unyama huo baada ya mtoto huyo kuanza kusema kwa majirani zao jinsi baba yake anavyomfanyia vitendo hivyo usiku huku mama yake akishuhudia.

"Hapo mwanzo tulikuwa tunasikia kwa majirani kuwa mtoto wetu anasimulia mambo mazito, hata hivyo hatukumuamini sana," alisema Chiku.

Chiku alisema kitu ambacho kinamsikitisha kuona dada yake ambaye ndiye mama mzazi wa mtoto huyo alikuwa akishuhudia jambo hilo na wakati mwingine walikuwa wakiingiliwa kwa zamu yeye na mtoto wake.

GIZA LA UNYAMA

Akisimulia huku akimwaga machozi, mtoto huyo ameliambia NIPASHE kuwa baba yake alianza kumuingilia wakati walipohamia kijiji cha Soga, Wilaya ya Kibaha mwaka 2011.

Alisema siku moja usiku wakati amelala, alimuona baba yake akimshika na kumlazimisha kumuingilia huku akimtisha kumkata kwa panga endapo atapiga kelele.

Alisema, aliogopa sana, alimuacha baba yake afanye anavyotaka na hapo ndipo ukawa mlolongo wa kufanyiwa unyama huo kila siku.

"Anaponiingilia napata maumivu makali, nataka kupiga kelele lakini naogopa ataniua kwa panga," alisema mtoto huyo.

Mtoto huyo alizidi kusema kwamba kwa kuhofia kuendelea kufanyiwa vitendo hivyo, aliamua kutoroka nyumbani kwao kila siku nyakati za jioni na kwenda kwa majirani, lakini wazazi wake walimtafuta na kumrudisha nyumbani.

Kutokana na kutoroka mara kwa mara, uongozi wa kijiji hicho uliamua kuwafukuza kijijini hapo na walirudi Mwandege mwishoni mwa mwaka huo.

"Tuliporudi baba alizidi kuniingilia, sasa ilikuwa anafanya kwa zamu, akitoka kwa mama anakuja kwangu na kuniingilia sehemu zote za siri," aliongeza kusema.

MAMA ASAIDIA KUEPUSHA KUNYIMWA UGALI

Hata hivyo alisema wakati anafanyiwa matukio hayo, mama yake anakuwa akishuhudia, wakati mwingine anamsihi asikatae anapoingiliwa kwa sababu watakosa chakula.

"Kila kitu ninachofanyiwa mama anakiona, nipapokataa mama ananiambia nisifanye hivyo ili tuendelee kula ugali wa baba," alisema mtoto huyo.

Alisema kutokana na kufanyiwa vitendo hivyo anaona sehemu zake za siri zimeharibika kwa vidonda.

ALAZIMISHWA KULA MBEGU ZA KIUME


Katika jambo la kusikitisha zaidi, mtoto huyo kabla na baada ya kuingiliwa hulazimishwa kula mbegu za kiume za baba yake ili kumsafisha.

Alisema, wakati baba yake anapomaliza kufanya mapenzi na mama yake, humfuata na kumwambia alambe mbegu zote, kisha anamuingilia mtoto huyo na anapomaliza humlazimisha tena kumsafisha kwa kumlamba.

NDUGU WAINGILIA KATI


Mama mdogo wa mtoto huyo, Chiku alisema baada ya kupata taarifa hizo, walilifikisha suala hilo ngazi ya ofisi ya kitongoji, kijiji na kituo cha polisi kwa ajili ya kumsaidia.

Alisema kwa kushirikiana na polisi wa kituo hicho, alifanikiwa kumpeleka Hospitali ya Wilaya ya Temeke, ambapo huko ilibainika mtoto huyo ameathirika na magonjwa ya zinaa.

Chiku alisema kwenye vipimo hivyo, iligundulika tumbo lake limejaa uchafu na alipatiwa huduma ya kumuondoa uchafu.

"Walinishauri kutokana na afya ya mtoto kuwa mbaya, nimpeleke hospitali ya karibu ya Mkuranga, huko atapewa huduma zote kulingana na magonjwa aliyokuwa nayo," alisema.

Alisema kutokana na kuwa peke yake katika suala hilo, hakuweza kuendelea nalo na badala yake aliliacha na kuendelea kuishi na mtoto huyo katika hali ngumu.

Chiku alisema hawezi kumlaumu sana dada yake, kwa sababu ana matatizo ya akili, ndio maana mwanaume huyo anaweza kufanikisha mambo yake bila kizuizi.

Alisema kutokana na maisha magumu anayoishi, hawezi kushughulikia tatizo hilo na mtuhumiwa kuchukuliwa hatua, aliomba watu binafsi mashirika mbalimbali ya haki za binadamu kuingilia kati.

Pamoja na hayo, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Pwani, Urich Matei, alipoulizwa suala hilo, alisema bado hajalipata, akamuomba mwandishi asubiri ufafanuzi baada ya kupata taarifa kutoka Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mkuranga.

"Taarifa hiyo sijaipata, ni mpya kwangu nakuomba niwaulize wenzangu wa Mkuranga na baadae nitakupatia ufafanuzi," alisema Kamanda Matei.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwandege Ally Ubuguyu alipoulizwa kuhusu tukio hilo, alithibitisha kutokea.

Ubuguyu alisema baada kupata taarifa hizo, wametoa taarifa katika kituo cha Polisi Vikindu, lakini mpaka sasa hakuna hatua zilizochukuliwa.

"Mtuhumiwa bado yupo hapa kijijini, lakini hakuna polisi aliyekuja kumkamata pamoja na kutaarifu juu ya tukio hili," alisema.

Alisema uongozi wake upo tayari kutoa ushirikiano wa aina yoyote kwa Polisi watakaokwenda kumkamata mtuhumiwa huyo, kwani kitendo alichokifanya ni kibaya.

WALIOFUKIWA NA KIFUSI KWENYE MGODI WA MORRUM JIJINI ARUSHA YAFIKIA 20




WATU zaidi ya 20 wamefariki dunia kwa kufukiwa na kifusi wakati wakichimba  mchanga aina ya Moramu katika machimbo  yaliyopo Moshono nje kidogo ya jiji la Arusha.


Tukio hilo ambalo limegubikwa na simanzi na vilio kwa ndugu jamaa na wananchi, limetokea leo majira ya saa 5 asubuhi wakati marehemu hao wakichimba na kupakia Moramu hiyo kwenye magari .


Pamoja na vifo hivyo magari mawili aina ya Fuso na Scania yameharibiwa vibaya baada ya kufukiwa na kifusi kilichoporomoka umbali unaofikia mita 50 kutoka usawa wa bahari.


Tayari kikosi cha uokoaji ambao ni  Jeshi la Wananchi Kambi ya Tanganyika Parkers kimefanikiwa kuopoa miili ya marehemu 16 waliofukiwa.


Baadhi ya miili ya marehemu  imetambulika kwa majina kuwa ni  Alex Maliaki, Gerald Hamis, Sauli Rafael (Mbu), Barick Loselian, Kababuu Lowasale, Mwenda Kibobori, Japhet Mjivaine na Garald Masai.


Taarifa za mashuhuda zimebainisha kwamba chanzo cha kuporomoka kwa kufusi hicho ni mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Arusha zilizosababisha kukatika kwa Ngema baada ya kuzidiwa na maji ya mvua.

JUMA NATURE AIBUKA MFALME WA TEMEKE BAADA YA KUMFUNIKA VIBAYA TEMBA NA CHEGE




Kundi la wasanii machachali la muziki wa kizazi kipya TMK Wanaume Halisi linaloongozwa na Juma Nature lenye maskani yake Temeke Jijini Dar es Salaam limeibuka kidedea na kuwa mfalme wa Temeke baada ya kulibwaga kundi la Tmk Wanaume Famili katika mpambano wa kumtafuta mfalme wa Tmk lililofanyika jana katika ukumbi wa Dar live Mbagara jijini Dar es Salaam

Juma Nature ambaye ndiye kiongozi wa kundi hilo aliibua hisia za mashabiki wake baada ya kupanda raundi ya kwanza na ngoma aina ya mchiriku huku akisindikizwa na baadhi ya wasanii wanaounda kundi hilo

Akizungumza katika shoo hiyo Nature alisema kuwa aliamini kundi la Tmk wanaume hawataweza kufika round ya pili katika mpambano huo kutokana na uzoefu aliokuwa nao katika fani hiyo

"Aibu yao aibu yao, wamekuja wenyewe hapa ni tatu bila hawafiki round ya pili hao sasa hivi watatoka wenyewe sisi ndio baba zao" alisema Nature
Kundi la Tmk wanaume halisi wakiwa nyuma ya stage teyari kwa kupanda jukwaani kuanza round ya kwanza ya mpambano wao waliingia jukwaani kwa mtindo wa mchiriku


Dogo Lina akiwasalimia mashabiki waliohudhuria pambano hilo yeye aliongoza mpambano wa round ya kwanza na kusababisha kujizolea mashabiki

NATURE NDIYE MFALME WA TEMEKE AWAFUNIKA VIBAYA TEMBA,CHEGE NA KUNDI LAO TAZAMA ILIVYOKUWA


.

Top Talent
Sir Kassim Juma Nature, kinara wa kundi la TMK Wanaume Halisi akiwanyooshea Mike mashabiki wake usiku wa kuamkia leo katika mchuano wa NANI MFALME ambapo mashabiki walimkubali kuwa Mfalme wao dhidi ya mahasimu wao, TMK Wanaume Family.
Mhe. Temba akicheza na mashabiki katika mpambano huo wa kukata na shoka
Sir Nature (kulia) na Doro..kazini

Sunday, March 31, 2013

MIILI YA WATU ILIYOPATIKANA KWENYE GHOROFA LILILOANGUKA DAR IMEFIKIA 21 MPAKA SASA



Miili ya watu iliyoopolewa kutoka kwenye vifusi vya jengo lenye ghorofa 16 lililoanguka jana katikati ya jiji la Dar es Salaam, imefikia 21. 
BGkNxjCCQAEyljV
Shughuli za uokoaji zilizoanza jana bado zinaendelea kwa siku ya pili huku kukiwa na taarifa za kuwepo miili zaidi kwenye vifusi hivyo.

Jana Rais Jakaya Mrisho Kikwete alitembelea katika eneo la jengo hilo lililoporomoka lililopo Mtaaa wa Indira Gandhi/Morogoro.
BGhTCALCEAA5EUX
BGhxvZyCAAACKUS
BGj2L20CcAAk2Qh
BGk_iPYCMAA0JzE
BGkGOFQCAAAxCuR
BGkHMJ2CYAAqKHE
BGkhNw7CAAA6hR1
BGkOUrrCIAAEF5U
BGlcQBeCUAA_li0
BGlhHCDCAAEk1YB
BGlHo3LCAAEzet7
BGlKKpQCEAAD_Nd
BGlNk-ACMAIQnCd
BGlTF1nCQAEJ5Sx
BGlTUDmCAAAtzar
BGlvUhpCEAAbSNA

MAHAKAMA YASEMA Uchaguzi Kenya ulikuwa huru na wa haki





Willy Mutunga rais wa mahakama ya juu zaidi Kenya
Mahakama ya juu zaidi nchini Kenya, imeamua kuwa rais mteule Uhuru Kenyatta atasalia kuwa rais mpya wa Kenya baada ya kusema kuwa uchaguzi ulifanywa kwa njia huru na ya haki.
Uchaguzi wenyewe ulifanyika tarehe nne mwezi Machi, ambapo hesabu ya kura ilimpa ushindi Kenyatta kwa zaidi ya laki nane.

Rais wa mahakama hiyo jaji mkuu Willy Mutunga alisema kuwa mahakama imekubali kwa kauli moja kuwa uchaguzi ulifanywa kwa njia ya huru na wazi na kuwa Kenyatta na mgombea mwenza wake walichaguliwa kihalali.

Uamuzi huu una maana kuwa Uhuru Kenyatta ndiye ataapishwa kama rais mpya wa Kenya tarehe tisa mwezi ujao
Kesi hiyo iliwasilishwa katika mahakama ya juu zaidi na mpinzani mkuu wa Kenyatta, Raila Odinga baada ya uchaguzi uliofanyika mapema mwezi huu.


Matokeo rasmi yalionyesha kuwa Uhuru alishinda uchaguzi kwa kumpiku Raila kwa asilimia 50.07 huku Raila akipata asilimia 43.28. Matokeo haya yalizuia kufanyika kwa duuru ya pili ya uchaguzi kwa kura 8,100.


Bwana Odinga aliishutumu tume huru ya uchaguzi na mipaka kwa kuhujumu matokeo ya uchaguzi ili kumpa ushindi Uhuru Kenyatta.


Uchaguzi wa urais, wabunge na wajumbe wengine wa serikali, ulifanyika tarehe nne mwezi Machi, ukiwa wa kwanza tangu uchaguzi uliokumbwa na ghasia mwaka 2007 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya elfu moja.


Bwana Kenyatta na mgombea mwenza wake ,William Ruto,wanakabiliwa na kesi katika mahakama ya jinai kwa kuchochea ghasia za mwaka 2007. Hata hivyo wamekanusha vikali mashtaka.


Mahakama ya juu zaidi inaweza kuthibitisha ushindi wa Kenyatta au kuubatilisha uamuzi wa wakenya na hivyo kuitisha uchaguzi mpya.Vyovyote matokeo yatakavyokuwa kuna wale watakaoghadhabika mno.


Rais anayeondoka mamlakani, Mwai Kibaki amewataka wakenya kuwa watulivu na kukubali uamuzi wa mahakama lakini wengi wanatagemea sana idara ya mahakama ambayo imekuwa na mageuzi makubwa na ambayo sasa watu watu imani nayo.


Mawakili wa Odinga wanasema kuwa kesi yao ilihusisha madai ya kuhujumu hesabu ya kura pamoja na matatizo ya usajili wa wapiga kura na vile vile matatizo ya mitambo ya usajili wa wapiga kura.


Mnamo Ijumaa mahakama ya juu zaidi ilidurusu matokeo ya kura katika vituo 22 vya kupigia kura. Na pande zote mbili zilisema matokeo yalithibitisha misimamo yao.


Kenyatta ameutaja uchaguzi huo kama ishara ya kukuwa kwa demokrasia Kenya na ulifanywa kwa njia ya amani.


Tume ya uchaguzi, pia imesisitiza kuwa uchaguzi ulikuwa huru licha ya hitilafu za kimitambo....


Wachunguzi wa kimataifa nao walisema kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki na kuwa tume huru ya uchaguzi uliendesha uchaguzi huo kwa uwazi.

HIZI NDO PICHA ZA MTUHUMIWA WA MAUAJI YA PADRI- ZANZIBAR




 Hapo ndio tujue kuwa wenzetu hawabahatishi na hawana siasa kwenye kazi zao proffessional....kazi kweli kweli!!wamehadithiwa tu wamemchora mtu yule yule!!Angalia Mchoro wa Polisi Hapo chini na Ufananishe na mtu Huyu..


KIJANA AAMUA KUCHOMA MOTO KITAMBULISHO CHA TAIFA CHA KENYA MARA BAADA MAHAKAMA KUHALALISHA USHINDI WA KENYATTA HAPO JANA




Kijana ROBERT STEPHENE OKELLO mwenye asili ya Luo ameingia matatani mara baada ya kuamua kuchoma kitambulisho chake cha Utaifa mara baaada ya mahakama kutengua Pingamizi la Mgombea kupitia Tiketi ya  ODM bwana RAILA ODINGA kupinga Uchaguzi huo.

Kijana huyo aliamua kufanya hivyo kutokana na kile alichokiita kuwa ni Uonevu wa kisiasa na hivyo kupelekea kukichoma kitambulisho hicho ambacho kikatiba ni mali ya Jamhuri ya watu wa Kenya.

Hata hivyo Mahakama Nchini humo haijazungumza kitu chochote mpaka sasa na kuna wasi wasi mkubwa kuwa huenda pakatokea hali ya hatari zaidi kama mahakama itachukua Uamuzi wa kumtia mbaroni kiajana huyo

TASWIRA YA UOKOAJI UKIENDELEA KATIKA AJALI YA JENGO LA GHOROFA 14 LILILOPOROMOKA DAR NA KUUWA WATU KADHAA



Jengo la Ghorofa 14 lililokuwa likiendelea kujengwa pembeni kabisa mwa Msikiti wa SHIA Mtaa wa INDRA GHAND na Zanaki, limeporomoka na kusambaratika na kusababisha vifo vya watu kadhaa ambao hadi sasa idadi haijaweza kupatikana kutokana na waokoaji kukosa vifaa vya kutosha katika zoezi hilo la uokoaji. Imeelezwa kuwa ghorofa hilo limeporomoka leo asubuhi majira ya saa moja na nusu ambapo ulianza kusikika mlio kama 'Tetemeko la ardhi'.
Aidha imeelezwa kuwa katika Jengo hilo walikuwepo mafundi ambao walikuwa wakiendelea na ujenzi na chini alikuwepo Mama Lishe, aliyekuwa akiuza chai na eneo hilo pia walikuwapo watoto wadogo ambao haikuweza kufahamika idadi yao waliokuwa wakicheza eneo hilo, ambao wote inasemekana wamefukiwa na kifusi cha ghorofa hilo, huku waokoaji wakifanikiwa kumpata mtoto mmoja tu ambaye hata hivyo imeelezwa hali yake ilikuwa ni mbaya na kuwahishwa hospitali.
Ni moja ya Kifaa pekee kilichokuwepo eneo hilo Trekta, likifukua kifusi ili kuokoa watu wanaodaiwa kufukiwa na kifusi hicho.
Baadhi ya watu waliwahi kufika kujaribu kutoa msaada bila mafanikio hapa wakiwa wamekwama baada ya kukosa vifaa vya kutosha.
Wahindi nao walikuwapo kutoa msaada hapa wakilielekeza Trekta kusogea mahala walipo wao wakihisi kuwa kuna mtu mahala hapo.
Waokoaji wakijitahidi kutumia mikono kuondoa kifusi hicho ili kuweza kuwaokoa watu waliofukiwa.
Trekta likiendelea kuondoa kifusi hicho.
Waokoaji wakiwa hoi......
Juhudi zinaelekea kulala.........
Moja kati ya magari yaliyokuwa eneo hilo likiwa limeangukiwa na mabaki ya jengo hilo.
Trekta likiendelea kuondosha kifusi......../
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik, akihojiwa na wanahabari kuhusu tukio hilo.
Moja ya ghorofa lililo karibu kabisa na jengo hilo lililoanguka nalo likiendelea kujenga nalo pia likiwa na ghorofa 14.....
Sehemu ya wananchi wakishuhudia tukio hilo.
Vijana wakishusha mitungi ya gesi ili kuwasaidia kukata nondo.... baada ya kuona vimekosekana vifaa vya haraka