Wednesday, July 3, 2013

MAMA WA MIAKA 52 AKAMATWA KWENYE CHUMBA CHA MTIHANI AKIMFANYIA MTIHANI BINTI YAKE



Mwanamke mmoja mfaransa (52) amejikuta mikononi mwa polisi wa jiji la Paris katikati ya mwezi june, baada ya kukamatwa kwenye chumba cha mtihani akimfanyia mtihani wa Kiingereza mwanae mwenye umri wa miaka 19, huku akijiweka kisichana zaidi wasimshutukie.

Ripoti kutoka nchini humo zinasema mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la Caroline D aliingia kwenye chumba cha mtihani akiwa amevaa skin jeans na viatu aina ya Converse ili aonekane kama mwanae.

Lakini jicho makini la msimamizi wa mtihani lilimnasa mama huyo kwa kuwa msimamizi alikua tayari alishamuona mwanae wakati anafanya mtihani wa Philosophy, kwa hiyo akamshtukia mama huyo kwa muonekano wake na sura yake ya kiutu uzima.

Msemaji wa Polisi wa Paris alisema mwanamke huyo alikiri makosa yake ya udanganyifu na kusema kuwa kiukweli yeye alikuwa anaweza zaidi Kiingereza zaidi ya mwanae.

Mwanamke huyo anakabiriwa na mashtaka ya udanganyifu na anaweza kulipa fine isiyopungua £7,000.

Lakini pia binti yake anaweza kupata msala wa kuzuiwa kufanya mtihani wowote wa kitaifa kwa muda wa miaka mitano. 

"GEREZANI KUMENIFANYA NIMJUE MUNGU VIZURI SANA"....HII NI INTERVIEW YA LULU MICHAEL



Kwa mara ya kwanza muigizaji wa filamu, Elizabeth Michael aka Lulu jana alifanya interview ya kwanza tangu atoke gerezani January mwaka huu. 

Lulu aliye na muonekano wa ‘udada’ zaidi alihojiwa jana kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV kinachoendeshwa na Zamaradi Mketema.
 Katia interview hiyo, Lulu aliongea masuala mengi kuhusu maisha yake ya sasa, mipango yake na mengine lakini akidai kuwa hatopenda kuongelea suala la uhusiano wake na Kanumba kwakuwa anahisi bado hajawa tayari ila muda ukifika atafunguka mengi. Haya ni baadhi ya masuala aliyoyazungumza.

Kuhusu uzinduzi wa filamu yake mpya Foolish Age


Ninaplan kufanya uzinduzi kwaajili ya movie yangu, lengo kubwa la kufanya uzinduzi ni kwamba kwanza nitajiskia vizuri kukutana na ‘okay these are my fans’ kukutana nao sehemu moja. Kuna vitu sitaweza kuongea kwenye interview ntahitaji kuviongea mwenyewe kama mwenyewe. 



Nitahitaji watu waone baadhi ya vitu vilivyopo kwenye movie. Movie inaitwa Foolish Age. Nitaizindua chini ya kampuni ya Proen (????) Promotions Ltd na ni kampuni ambayo ndio inanimanage kwa sasa.

Kuhusu kama ana boyfriend aliyemnunulia vitu vya thamani

Watanzania wengi tulishajiwekea ile dhana kwamba ‘ukiona mwanamke amefanya kitu basi there is a man behind, yaani ni ile dhani ipo tayari ndani yetu kwahiyo hata kama mtu atastruggle kutafuta kitu chake mwenyewe lakini hiyo itakuwa ni ukweli wako na unaujua mwenyewe . 



Kiukweli ni kwamba hakuna mwanaume yeyote ambaye amenifanyia chochote till now. Nachoshukuru tu ni menejimenti yangu, kampuni ambayo nafanya nayo kazi.


 Ni kampuni ambayo inanijali, inajali kazi zangu, inajali msanii wao kwahiyo whatever I’m having, whatever I’m doing ni mimi mwenyewe, ni kazi zangu ni biashara yangu.

Uhusiano wake na Mama Kanumba na jinsi alivyompata kufanya naye movie ‘Mapenzi ya Mungu’

Kwa sasa hivi tupo kama familia kwa hiyo it wasn’t hard mimi kumpata na nilijisikia vizuri kama ntaweza kufanya naye kazi. Kuna spirit ambayo ilinivuta zaidi nifanya kazi na Mama Kanumba kuliko labda mama mwingine.

Anachomiss kwa Kanumba

Busara zake, he was a person ambaye akikuona unaenda hivi he takes you in the right way.

Kuhusu kwanini mapenzi yake na Kanumba yalikuwa siri
Ni makubaliano tu and there was no need like to let people know yaani kumfanya kila mtu ajue nadhani haikuwa na maana kwetu.

Kuhusu kwanini alinenepa alipokuwa gerezani


Labda kwasababu nilimwachia Mungu kila kitu, nilimkabidhi Mungu kila kitu so I had this peace of mind. Niliacha kwamba yeye ni msimamizi wa kila kitu. Let me confess kwamba gerezani kumenifanya nimjue Mungu vizuri sana,. 



Kumenifanya nimjue na nimwamini na kumjua na kumwamini kumetokana kwamba kuna vitu vingi vimekuwa vinafanyika like naviona hivi kwa macho na naona kabisa kwamba hapa ingekuwa mimi kama mimi ama binadamu yeyote haiwezekani... 

Tuesday, July 2, 2013

HUU HAPA UJUMBE WA RAY C KWA MASHABIKI WAKE BAADA YA AFYA YAKE KUIMARIKA...!!


W

Mwanadada Ray C leo hii kupitia ukurasa wake wa instagram ameachia ujumbe huu kwaajili ya mashabiki zake na kuwashukuru kwa support yao. Ametirikia hivi: 

TAZAMA PICHA:TUZO ZA BILLBOARD AWARDS (BBMA) 2013 ZILIVYOFAANA JIJINI LAS VEGAS...!!



Jana Usiku wa Tarehe 1/7/2013 ulikuwa usiku wa  Tuzo
za Billboard Music Award,Tuzo hizi
ni Maalumu kabisa kwa wanamuziki wanaofanya vizuri na
 nyimbo zao zinazosikilizwa zaidi
kwenye vituo mbalimbali vya redio,television na dunia kwa
kwa ujumla  na Online ni kimaanisha Youtube,Itune na n.k kwa Ujumla......


Usiku wa Jana ndio ilikuwa sherehe ya ugawaji wa tuzo hizo
 uliofanyika kwenye jiji la Las Vegas
uku ikiudhuriwa na Mastaa wengi wanaofanya mziki ndani
 ya marekani na nje ya marekani...
Usiku huo unaweza kujionea kwenye picha jinsi
ulivyofaana kabisa kila mtu akiwa kwenye nyuso za furaha
wakati wa kupokea tuzo na hata wakati wa utumbuizaji

Zifuatazo ni picha za ugawaji tuzo na matukio mbalimbali ya
 utumbuizaji kutoka kwa wasanii
walioalikwa kutumbuiza kwenye usiku huo wa Billboards Award
2013 (BBMA)......



Selena Gomez & Taylor Swift...!!
Akon akitumbuiza kwenye usiku wa Tuzo za Billboard...!!
Nicki Minaj & Lil wayne wakitumbuiza pamoja...!!

Madonna akizungumza kwenye steji kuhusu madawa ya kulevya....!!





Psy & Tracy Morgan wakifanya yao jukwanii...!

Sky Blue akitumbuiza Jukwaa moja na Wiz Khalifa....!!picha zote na dj sek 


Justin Bieber akitumbuiza stejini...!!
Will.Iam akizungumza jukwanii...!!
Msanii mkongwe Prince akitumbuiza jukwanii...!!

Taylor Swift akitumbuiza jukwanii...!!
Taylor Swift akipokea Tuzo usiku wa Tuzo za Billboard...!!
Nicki Minaj akipokea Tuzo...!!
Chris Brown Akitumbuiza...!!

Bruno Mars kwenye Stage....!!
Tracy Morgan ndio aliehendesha Shuguli nzima ya Tuzo hizo..!!


Kelly nae alikuwepo kwenye usiku huo wa Tuzo za Billboard
Madonna & Wil-Iam wakiwa jukwani kuwakilisha Tuzo..!!
Serena Gomez akiwajibika stejini...!!

Taylor Swift akipokea Tuzo...!
Justin Bieber akizungumza baada ya kupokea Tuzo...!!

Pitbull akitumbuiza...!!
Jennifer Lopez akifanya yake stejini.....
Celline Dion akizungumza kwenye usiku wa Tuzo hizo za Billboard kama
mkongwe kwenye muziki wa Marekani...!!
David Guetta akitumbuiza jukwaani pembeni akiwa na
 Akon mkono wa kushoto na kulia kwake ni
Ne-Yo
David Guetta akizungumza baada ya kupokea Tuzo...
Lil wayne a.k.a Tunechi akiwa stejini....
Nicki Minaj & Lil wayne kwenye jukwaa wakitumbuiza kwa pamoja...!!
Ne-Yo akitumbuiza jukwani kwenye usiku wa
 Tuzo hizo za Billboard 2013