Friday, April 5, 2013

MPENZI WANGU AKITONGOZWA HUNIAMBIA NA KU "FOWARD" MESSAGE KWANGU...JE HII NI SAWA?




 -Wadau  Naomba mnipe mwongozo kwa hili la mpenzi wangu.

 -Kuna mambo mawili yamejitokeza hv karibuni:

 - kwanza, juzi alinipigia simu[hatuko mkoa mmoja, anasoma] na katika maongezi akasema kuwa X-boy wake kampigia simu nanukuu.."eti kanipigia simu, nikamuuliza leo umekumbuka nini?....akaniambia eti anakuja huku[alipo huyu demu] mm nikamwambia nasafiri, sitakuwepo"

  -Pili, jana kaniambia "mpenzi kuna sms zinachekesha...ngoja nikuforwadie...sms 1 ilisomeka "nakuhitaji"....


Sms ya Pili ipo hivi.."leo umependezaa, nataka nije kwako"..hizi sms anadai katumiwa na mshikaji anayeonyesha kumtaka kimapenzi

No comments:

Post a Comment