Vituko mjini Iringa haviwezi kuisha kama jamii haitakubali kwa moyo mmoja kupambana na ukatili wa kijinsia. Huyu ni Binti ZAWAD KARIM miaka 16 mkazi wa mshindo nyuma ya banki ya NBC manispaa ya Iringa amepigwa na hatimaye kunyweshwa mkojo na mama yake mdogo aitwaye Ever ubamba.
Tukio lilikuwa hivi:
Zawadi kimsingi anaishi na mama yake mzazi ambaye kwa kipindi hicho dada mtu huyo alikuwa anaumwa. Ever alikuwa nje na marafiki zake ndipo mama yake mdogo huyo akamwiita ndani ya nyumba yao hiyo wanayoishi mtaa wa mshindo.
Baada ya kumwita na kisha mtoto huyo kushindwa kusikia baadaye aliitika na kuingia ndani na ndipo alipo ambiwa avue nguo zote na huyo mama yake mdogo Ever .Baada ya muda mfupi Zawadi alianza kupokea kipigo kikali kutoka kwa mama yake mdogo.
Katika kipigo hicho Zawadi alipigwa pamoja na kunyweshwa mkojo kutoka kwa mama yake mdogo huyo.Zawadi ambaye ni mtoto wa kuzaliwa na Dada yake Ever inadaiwa kipigo hicho kimesababishwa na tuhuma kwamba eti familia hiyo haina mtoto kama yeye zawadi.
Zawadi inadaiwa aliwahi kwenda zanzibar kwa nia ya kufanya kazi na baada ya muda mama yake mzazi ambaye jina lake bado halijafahamika alimpigia simu arudi nyumbani na mara baada ya kurudi ndipo kutokuelewana huko kukajitokeza.
Aidha taarifa za ndani kuhusu tukio hilo zinasema kuwa Mama yake Msichana Zawadi alitupwa akiwa mchanga na kuokotwa na wasamalia wema na hatimaye kulelewa na Bibi yake ambaye hata hivyo amefariki duni.
Kisa cha yote hayo ni madai ya mtoto zawadi kuomba aoneshwe Baba yake mzazi ili walau aweze kupata pumziko la adha anazo zipata kutoka kwa ushirika wa ndugu zake hao.Zawadi pamoja na majirani wameuambia mtandao huu kuwa vitu vilivyo tumika kumwadhibu vilikuwa ni pamoja na nyaya za simu,mkandaa,na vipande vya chupa katika kumchoma navyo.
Hata hivyo hadi mtandao huu unachapisha taarifa hii watuhumiwa wa tukio hili yaani Mama mzazi pamoja na Mama mdogo wa Zawadi wanashikiliwa na jeshi la polisi kitengo cha dawati la jinsia kwa mahojiano zaidi.
No comments:
Post a Comment