Wednesday, March 27, 2013

SHIRIKISHO LA FILAMU TANZANIA LAMMPONGEZA WEMA SEPETU




SHIRIKISHO la Filamu Tanzania (TAFF) limempongeza msanii wa kike Wema Sepetu kwa moyo wa upendo aliouonyesha kwa msanii mwenzie Kajala Masanja kwa kumlipia faini ya sh. milioni 13 alizotozwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na kupatikana na hatia katika kesi ya utakatishaji fedha iliyokuwa inamkabili mahakamani hapo

Akizungumza kwa niaba ya viongozi wengine rais wa shirikisho hilo Simon Mwakifwamba alisema kuwa imani na moyo wa upendo aliokuwa nao msanii Wema ndio uliomsukuma kumlipia kiwango hicho cha fedha bila ya kujiuliza mara mbili kitendo hiko kimeonyesha jinsi gani wanavyohitaji kushirikiana katika matatizo

Alisema kuwa wasanii wanatakiwa kujifunza kutoka kwake kwani wanahitaji kuwa kitu kimoja kujaliana kwenye matatizo na kutambua kuwa wao ni familia moja wanaojenga nyumba moja

"Kitendo alichoonyesha msanii mwenzetu ni kitendo cha kuigwa na cha kiimani siyo kwamba anauwezo sana hapana ila kujali na utu ndio kilichomsukuma atoe fedha hizo" alisema Mwakifwamba

"Unajua kuwa nacho na kutoa ni vitu tofauti wengi pale walikuwa navyo ila labada hawakuwa na moyo wa kutoa hivyo Wema mungu atambariki na kumuongezea pale alipopunguza " aliongeza Mwakifamba

Mwakifamba alimtaka Kajala kutoa shukurani kwa mungu kwa kumsaidia kumtoa kule alipokuwa kwani sehemu yenye mateso na inayoumiza katika maisha ya kila siku

Wakati huo huo kwa upande wake Msanii Wema Sepetu "Imenichukua masaa mawili kufanikisha hili,nilienda benki nikatoa fedha na kuja hapa kulipa, ni sh.milioni 13".Hii ni kauli ya Msanii wa Filamu Wema Sepetu akizungumza na waandishi wa habari buda mfupi baada ya kukamilisha zoezi la kumlipia faini ya kiasi hicho cha fedha msanii mwenzake Kajala Masanja.

Wema alisema kuwa mumlipia Kajala kiasi hicho cha fedha haoni kama amepoteza kwani msanii huyo ni kama ndugu yake wa karibu.

"Katika vitu vingi sana,kumsaidia kwangu sijaona kama nimepoteza chochote,naona kama nimetoa kitu kama mtu  yoyote anayeweza kufanya hivi kwasababu kutoa ni moyo,sihitaji kulipwa chochote mwenyezimungu ndiye atanilipia"alisema

Aliongeza kuwa "Nahakika hakuna mtu anayependa kukaa gerezani,kwahiyo nimeona kama nitafanya hivyo nitamuokoa katika hali zote mbaya"

Kwaupande wake Dkt.Cheni alimewataka wasanii nchini kuwa na ushirikiano pale mmoja wao anapopatwa na matatizo kwani wao ni kitu kimoja na ni familia moja hivyo kushirikiana kwao ndio kutaendelea kuimalisha undugu walio nao na kufanikiwa katika kazi wanayoikusudia

Alisema katika maisha hakuna mtu aliyewekwa alama usoni kuwa atakuwa wa matatizi tu bali kila mtu anaweza kupata tatizo kwa aina yoyote hivyo tunatakiwa tuwe karibu.

"Kiukweli sina la kusema zaidi kwani matatizo yanamkuta kila mtu na yanapokukuta unakuwa haujajua,Mtu unaweza kuona unafanya jambo sahihihi lakini kijamii au kisheria linakuwa tatizo,ninachoomba kwa wasanii wenzangu tuwe na ushirikiano pale mwenzetu anapopatwa na tatizo kama hili tujitoe kwa mwenzetu"Alisema Dkt.Cheni.

Awali Dk.Cheni alisema kuwa wangeweza kuchangishana kiasi hicho cha fedha na kuzilipa lakini baadaye Wema alionekana akitoka mbio katika viwanja vya mahakama hiyo na kwenda katika gari lake ambapo ilidaiwa alikwenda benki kutoa fedha.

Kajala alitoka gerezani baada ya kulipiwa kiasi hicho cha fedha na msanii mwenzake Wema Sepetu muda mfupi baada ya kusomwa hukumu hiyo.

No comments:

Post a Comment