Wednesday, March 27, 2013

YULE MTOTO WA MIAKA 8 ALIYEOA BIBI WA MAIAKA 61 ADAI KUFURAHIA FURAHA KUITWA BABA





KUSHOTO: Sanele akibusiana na mkewe, Helen siku ya harusi yao wiki mbili zilizopita. KULIA: Sanele na Helen walipata chakula cha usiku pamoja nyumbani kwa mkewe huyo.

Huku miguu yake ikining'inia juu ya sakafu na sehemu yake ya chakula cha mtoto, inaonekana kama anakula chakula cha usiku na bibi yake.Ukweli ni kwamba Sanele Masilela, mwenye miaka 8, anafurahia chakula cha usiku na mke wake, baada ya kumuoa wiki mbili zilizopita, na inasemekana kwa sasa ameanza kujisikia kama mume kamili.

Mwanafunzi huyo alimuoa Helen Shabangu baada ya mababu zake kuwasiliana naye kutoka nyuma ya makaburini wakimweleza kwamba anatakiwa kuoa.Mwanafunzi huyo alimchagua rafiki wa familia yao na mama wa watoto watano Helen na familia yake ikalipa Pauni za Uingereza 500 kuwezesha mama huyo kuwa mkewe katika sherehe iliyogharimu Pauni 1,000 mjini Tshwane, Afrika Kusini.

Sanele alikiri kwamba tangu harusi hiyo, ameanza kujisikia kama mwanandoa.Alisema: "Siku hiyo ilikuwa ya kipekee na hakika ilikuwa kama alivyokuwa akifikiria itakuwa."Marafiki zangu walifikiri ni mzaha kwamba nilikuwa naoa lakini sasa najisikia kama mume."

Akiwa amevalia tai na suti ya rangi ya shaba, Sanele, mtoto wa mwisho katika familia ya watoto watano, alivalishana pete mbele ya wageni 100 na hata kufikia kupigana mabusu na mkewe huyo.Lakini, licha ya muonekano, haikuwa halisia, ndoa hiyo ilikuwa ni kutimia mila na haikufungwa kisheria.

Wanandoa hao hawaishi pamoja lakini Helen mara kwa mara anamwalika kula naye chakula cha usiku pamoja kwenye nyumba anayoishi na familia watoto wake.Sanele amerejea kwenye maisha yake na kuendelea kufurahia shule na kucheza kandanda na marafiki zake lakini anakiri kwamba ndoa hiyo ilikuwa muhimu mno kwake.

Alisema: "Babu yangu aliwasiliana nami kupitia picha ya harusi ya mama yangu."Tuna mahusiano maalumu sababu nimerithi jina lake."Alisema aliona picha hiyo na kujihisi mnyonge kwamba hakuwahi kuweza kufunga ndoa yake mwenyewe hivyo alinitaka mimi nifunge ndoa. Nilimchagua Helen sababu nampenda sana."

Habari za harusi hiyo zimeshitua dunia nzima lakini Helen, ambaye ameshaolewa kwa miaka 30 sasa na kupata watoto watano wenye umri wa kati ya miaka 37 na 27, ametetea sherehe hiyo.Alisema: "Nafahamu habari hiyo imesambaa dunia nzima na kubwa ni kuwa nchi nyingine zimeweza kujifunza kuhusu utamaduni wetu na mababu zetu.

"Tulichofanya hakikuwa makosa. Ni utamaduni wetu tu. Pale mababu zetu wanapoagiza kitu, tunafanya kile wanachosema. Sidhani kama watu wengine wanaelewa hilo."Nafahamu mababu wamefurahi sasa sababu tuko sawa na kila kitu kinaonekana safi."Familia nzima imefurahi sana kuliko ilivyowahi kutokea."

Helen alikiri sherehe hiyo ya gharama ilikuwa kubwa kuzidi ilivyokuwa harusi yake halisi na mumewe, Alfred, mwenye miaka 65, na hakuna cha kujutia.Aliongeza: "Kila mara nitakuwa karibu na familia ya Sanele kuliko ilivyokuwa kabla ya harusi hiyo na kabla Sanele kunichagua mimi kama mkewe tulikuwa karibu mno.
"Hakuna kilichobadilika tangu wakati huo."

Mumewe kwa miaka 30, Alfred mwenye umri wa miaka 65, alisema: "Watoto wangu na mimi tumefurahi.
Sanele pia alisema anatarajia atafunga ndoa sahihi kwa mwanamke wa umri kama wake wakati atakapokuwa mkubwa.

Aliongeza: "Nilimweleza mama yangu kwamba nilitaka kuoa kwa sababu hakika nilikuwa nataka kufanya hivyo."Nimefurahi kwamba nimemuoa Helen - lakini nitaenda shule na kusoma kwa bidii."Pindi nitakapokuwa mkubwa nitaoa msichana wa rika langu."

Mama wa Sanele mwenye miaka 46, Patience Masilela aliongeza kwamba anaamini sherehe hiyo 'haikuwa na tatizo' na kwamba imewatuliza mababu.Alisema: "Hii ni mara ya kwanza kutokea katika familia hiyo."

No comments:

Post a Comment