Mwanamuziki toka mkoani Morogoro anayefanya poa kwa sasa na wimbo wake wa Leo mwanadada Dayna Nyange a.k.a Mkali wao, amefunguka na kumpigia saluti mwanamuziki mkongwe toka hapa Morogoro Afande Sele.
Akiongea na mwandishi wetu toka jijini Mwanza aliko sasa katika ziara ya kimuziki na uzinduzi wa Albam ya Kala. Dayna amesema huwa anamkubali afande kwa tungo zake
'' kwa kweli siku zote, nimekuwa nikimkubali sana Afande sele kwa tungo zake zenye ujumbe, lakini kwa wimbo huu wa Dini tumeletewa, nampigia saluti.
Afande ni bonge la msanii na huwa naskiliza nyimbo zake kwani najuwa nikiskiliza nyimbo zake kuna madini napata, lakini sasa kaka mkubwa kwa hapa alipofikia na kufikilia kwa kina juu ya wimbo huu, anastahili kuwa mfalme wa Rhyme, waliompa tuzo hawakukosea.
Big up sana Afande, saluti kwake, aendelee kuwa mwalimu wa ujumbe , huuwimbo ni zaidi ya Hotuba ya kitaifa Inayotolewa na Rais'' Amesema Dayna
Ubalozini
No comments:
Post a Comment