Sunday, April 28, 2013

MUME WANGU HANA PUMZI KITANDANI....KWAKE DAKIKA TATU NI NYINGI SANA....NAOMBENI USHAURI



Mimi ni mdada wa miaka 27 na nina watoto wawili kwa sasa nimeolewa na mkaka mwenye miaka 32.

Kwa kweli mume wangu ni kijana handsome. Katika maisha yangu ya usichana mpaka kuolewa nimekuwa na mahusiano na wanaume takribani 4 kabla ya mume wangu.

Wanaume hao wote kwakweli walikuwa nao wazuri  na kati yao wawili walikuwa waume za watu na walikuwa na maumbile yakunitosha.... 



Pamoja na maumbile  yao,sikuwahi kufika kileleni japokuwa walikuwa wanapumzi ndefu yaani walikuwa wanaweza kuplay for about  1 hour . Tena kama tutalala pamoja usiku huo walikuwa wanaweza hata 4-5.

Nilipompata mume wangu nilimpenda toka rohoni na baada ya mhusiano ya miaka miwili tulioana,tatizo ambalo lipo kwenye ndoa yangu na nililiona toka mwanzo ni kwamba mume wangu hana pumzi kitandani japokuwa ndio mwanaume pekee anayenifikisha kileleni .

Yaani mume wangu yeye ni 3 minutes tu amemaliza  na baada ya muda anakoroma, hatuwezi kufanya hata mara  mbili kwa usiku hata nikimchezea anashindwa kusimama labda afanye kimoja asubuhi kingine usiku.

Na ili nikojoe kuna staili lazima niziapply mimi mwenyewe niwe najigusa kwake maana yeye tukifanya anashindwa kujizuia mara moja anakojoa.

Nisaidieni wapendwa nifanyaje maana  bado  nampenda  mume  wangu."
---------------


Jibu la Dyna: 

Shukurani sana kwa ushirikiano, hongera kwa kufanikiwa kufika kileleni kwani sio wanawake wote hufika hapo. Sidhani kuwa ni kweli kuwa mumeo anakojoa ndani ya dakika 3 na wakati huohuo wewe unafika kileleni.

Unapokuwa kwenye uhusiano wa kudumu au ndoa hupaswi kabisa-kabisa kurudisha mawazo yako nyuma na kuanza kufananisha utendaji wa wanaume uliokuwa nao na mpenzi wako wa sasa/mumeo. Jifunze kukubali jinsi mumeo alivyo na ridhika na uwezo wake aliojaaliwa na Mungu.

Ndio maana kabla ya uchumba kutangazwa kule kwetu huwa kuna swali unaulizwa na mama au bibi au shangazi


- "je una uhakika kuwa unataka kuolewa na huyu bwana? 


-je uko radhi kuishi nae hata kama siku moja utagundua kasoro zake? (kasoro hapa wanamaanisha kushindwa kufanya tendo). 


Hivyo basi unapofunga ndao na mtu na kugundua kuwa uwezo wake kitandani umebadilika ghafla kutokana na umri au mataizo mengine ya kiafya, unatakiwa kukubali tatizo na kumpa ushirikiano ili kuepusha matatizo.

Kilele na mwanamke:
Mwanamke anafika kileleni kuanzia Dk 10 mpaka dk 45 tangu tendo lianze na pengine inaweza kuchukua muda mrefu zaidi, hivyo basi kama unafanikiwa kufika kileleni ni wazi kuwa mumeo anauwezo wa kwenda mwendo wa angalau Dk15-20 sio dakika  3  kama  ulivyosema!

Napenda utambue kuwa uwezo wa tendo kwa wanawaume unatofautiana kama ilivyo kwa baadhi ya wanawake, suala muhimu ni upendo mlionao (mnapendana) na yeye anauuwezo wa kulifanya tendo mpaka wote mnafikia mshindo nakuridhika.

Mawasiliano wakati wa Tendo:
Suala lingine hapa ni kutojua namna ya kucheza na wewe au mwili wako, kama unapenda kuchezewa zaidi kabla ya tendo la ndoa ni wajibu wako kuliweka hilo wazi na kumuelekeza mumeo wapi pa kushika, usitegemee yeye afanye hivyo kwani hajui nini unachokitaka au kukipenda. Ili ufurahie tendo na lifanywe your way unatakiwa kuwasiliana na mumeo wakati tendo linaendelea....


Kama nilivyosema hapo awali sio wanaume wote wanauwezo wa kufanya  mapenzi unaofanana, hivyo basi kama yeye anamudu asubuhi na jioni au asubuhi mchana na jioni (weekends) then kubali utaratibu huo kuliko kulazimisha afanye ulivyozoea wewe mara tatu katika saa moja.....ni ngumu kwa baadhi ya wanaume hasa wenye umri wa miaka 35 na zaidi.

Ni matumaini yangu utafanyia kazi ushauri kutoka kwa wachangiaji wengine na kuongezea maelezo ya hapo juu  ili kuishi maisha mazuri na yenye amani kwa faida yako, mumeo na watoto wenu

No comments:

Post a Comment