Zamani kulikuwa na bia moja ambayo kauli mbiu ya kibiashara ya bia hiyo ilikuwa maneno “Baada ya kazi ,Burudika” , . Wachezaji wa Manchester United waliifanyia kazi kauli mbiu hii na kuitendea haki kisawasawa baada ya kukesha wakila bata kwenye casino na bar za jijila Manchester kufuatia ushindi wa 3-0 walioupata dhidi ya Aston Villa ambao ulihakikisha ubingwa kwa klabu hiyo kwa msimu wa 2012/2013.
Wakiongozwa na kamanda wa bata kwenye kikosi hicho beki Rio Ferdinand , wachezaji wa United hawakuruhusu uchovu wa mechi uwazuie kula raha na huwezi kuwalaumu kwani kazi kwa msimu huu imekwisha na wanaruhusiwa kufanya wanachotaka kwa sasa.
Hakuna aliyebaki nyuma kuanzia kwa wachezaji wa kikosi cha pili kama kipa Ben Amos mpaka kwa mkongwe Ryan Giggs na kipa David De Gea ndio alikuwa mtu wa mwisho kuondoka club saa 12 asubuhi baada ya usiku wa raha akienjoy na washkaji zake baada ya kazi ngumu ya msimu huu.
Zifuatazo ni baadhi ya picha za jinsi hali ilivyokuwa wakati wachezaji wa Man United walipoliteka jiji la Manchester usiku wa juzi.
No comments:
Post a Comment