Msanii wa Kundi la Tip Top Connection, Madee au Rais wa Manzese ameeleza kuwa wimbo wake wa Nani Kamwaga Pombe Yanguumempa heshima kubwa.
Akiongea na mwandishi wetu, Madee, ambaye jina lake halisi ni Hamad Ally Seneda alisema licha ya kupata shoo nyingi, lakini pia ni wimbo ambao unapigwa sana kwenye klabu mbalimbali na kila unapopigwa hakuna anayekaa kitini.
Alisema kuwa kufuatia kutoa wimbo huo ameshakusanya Shilingi 16 milioni.
Alisema pamoja na kupata fedha nyingi kupitia wimbo huo bado hajaamua azifanyie nini ila ameamua atulie kwanza akitafakari nini kinafuata.
“Wimbo bado upo juu na unafanya vizuri, hivyo ninachofanya kwa sasa ni kuendelea kukusanya fedha kutokana na shoo ambazo nitapata kutoka kwenye wimbo huo baada ya hapo ndio nitajua nifanyie nini,” alieleza.
Aidha, Madee alisema kuwa anafurahi kuona amefanya kitu ambacho kila mpenda burudani kinamfurahisha kwani sio wasanii wengi ambao wanaweza kufanya kitu kama hicho hasa kwa wale waliopo kwenye usanii kwa muda mrefu. Kalunde Jamal
No comments:
Post a Comment