Vurugu kubwa zimeibuka chuo cha uhasibu cha Arusha baada ya mwanachuo kuchomwa kisu na mwanaakijiji na kufariki dunia....
Baada ya tukio hilo, wanafunzi walitoa taarifa kwa mkuu wa chuo lakini hakuwapa msaada wowote.
Walipokosa msaada,wanafunzi hao walianza kuandamana na taarifa zikafikishwa kwa mbunge Godbless lema ....
Mbunge huyo bila hiyana akawasili na kufanikiwa kuwatuliza wanachuo hao maana nyumbani kwa Godbless lema si mbali na chuo hicho ...
Baada ya taarifa kumfikia Mkuu wa mkoa, ilimbidi aliwasili na kuanza kuzungumza na wanachuo lakini baada ya kugundua uwepo wa Lema alianza kuongea kwa lugha mbovu na ndipo wanachuo walipo kasirika na kuanza kumpiga mawe.
Hali ilipochafuka,FFU waliingia kazi ya kutuliza ghasia...Hali ni mbaya sana lakini cha kushangaza askari mmoja aliwatonya wanachuo wamfiche Lema
Godbless Lema anasakwa mpaka sasana hajulikani alipo baada ya wanachuo kumficha kusiko julikana.
No comments:
Post a Comment