Hii ndiyo Shule ya Msingi ya Besta Sae Mbeya.
Vibarua waliopewa jukumu la kuhamisha mizigo shuleni hapo
Viti vikiwa vimetolewa eneo la shule ya Msingi Besta
Gari la mizigo likichukua mizigo kuelekea eneo Jengine
Waliopewa Dhamana ya kuchukua mizigo wakiwa wanaingia ndani kwa nguvu kutoa vitu katika shule hiyo ya Besta
Wanafunzi wa Shule ya Besta wakiwa Hawaelewi cha kufanya wakati mizigo yao aikichukuliwa
Mmiliki wa Kampuni ya Ulinzi ya Retired Army Bwana Kubaja akiimarisha ulinzi baada ya kupewa jukumu la kulinda shule hiyo na Wamiriki wapya.
Kipande cha Shule ya Besta
Polisi wakiwa na watu waliopewa dhamana ya kutoa vitu Besta wakiwa wanaendelea kutoa vitu hivyo
Baadhi ya vitu ambavyo vilitolewa nje ya Shule ya Besta
Vijana waliopewa Dhamana ya kutoa vitu vya Shuleni hapo wakitoa Magari nje ya Shule hiyo
Msikiti ambao upo ndani ya shule ya Msingi Besta ambao pia wananchi wa Jirani wanatumia , nao pia umenunuliwa kwa Amri ya Mahakama
Wanafunzi wa Shule ya Msngi ya Besta wakiwa Bado hawajui cha kufannya
Wanafunzi wa Shule ya Msingi wa Besta wakiwa wanakusanya Madftari yake pamoja na Mitihani yao.
Mmiriki wa Shule ya Besta Ndugu Hamis Othnman akimsihi Askari ampe nakala ya kuondolewa kwake Shuleni Hapo.
Mmiriki wa Shule ya Besta Ndugu Hamis Othnman akikataliwa na Askari hoja yake yakupewa nakala ya kuondolewa kwake na kutakiwa kumuona Mkuu wa kituo cha Polisi kati au Kumuona msajili wa Mahakama Kuu
***************
Na Ezekiel Kamanga
Mahakama kupitia dalali wa Mahakama imepiga mnada Shule ya Msingi Besta iliyopo Sae jijini Mbeya kutokana na madai ya mdai katika kesi hiyo .
Mdai wa kesi hiyo namba 212 ya mwaka 2003 ni Kampuni ya Mohamed Enterprises ambapo alikuwa anamdai Hamis Othman kiasi cha Shilingi Milioni 270 ambazo alishindwa kulipa . Kesi hiyo namba 27 ilianza kusikilizwa mwaka 2003 huku Othman akitetewaa na Wakili Mkumbe ambapo hukumu ilitolewa 4.6.2012 majengo ya shule yauzwe, mpaka sasa madai hayo hayaja jurikana yalikuwa yanahusiana na nini.
Wamiliki wapya wa majengo hayo ni Mbeya Heritage Company ambao walikabidhiwa majengo hayo na Dalali wa Mahakama Chini ya usimamizi wa mtendji kata ya Ilomba Erasto Mwakapoma na Mwenyekiti waa Mtaa wa Sae Erias Mwakyusa huku Jeshi la Polisi Likishuhudia makabidhiano hayoyakifanyika kwa amani.
Zoezi lilisitishwa kwenye Msikiti kutokana na Imani waumini wa Msikiti huo wataalifiwe ili ndani ya siku Mbili wawe wameondoka eneo hilo.
Adha kubwa ilikuwa ni kwa wanafunzi wliokuwepo shuleni hapo ambapo mitihani yao ilioekana kuzagaa hovyo kutokana na purukushani zilizo kuwepo bila taarifa yoyote na kutojua Hatma yao ya masomo yao kutokana na Madarasa kuhodhiwa na mmiliki mwengine Licha ya kuwepo kwa mabweni kando ya Shule hiyo na kufanya mizigo yote kulundikwa nje ya mabweni.
No comments:
Post a Comment