Friday, May 31, 2013

MABADILIKO KUHUSU MAZISHI YA NGWEA



Habari kutoka kwa wanakamati wa mipango ya mazishi ya marehem Albert Mangwea zinasema kuwa mwili wa marehem Ngwea utafika Dar siku ya jumapili saa nane mchana na sio jumamosi kama ilivyoarifiwa hapo awali…


Mwili huo utaagwa siku ya jumatatu saa mbili mpaka saa sita machana ambapo safari itaanza kuelekea Morogoro kwa ajili ya mazishi

KIJANA ANUSURIKA KUFA BAADA YA VIBAKA KUMCHOMA MOTO HUKO MKOANI LINDI



Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Ismai Mayoba(31) anayefanya kazi Bar ya Mangrove,Mkazi wa Manispaa ya Lindi amenusurika kifo baada ya kuvamiwa na kundi la Vijana waliotaka kumpora na hatimae kumchoma moto. 

Kwa sasa kijana huyo amelazwa katika Hospital ya Sokoine Mjini humo.

Kufuatia tukio hilo,Jeshi la Polisi wilayani Lindi limefanikiwa kumkamata mtu  mmoja kati ya watuhumiwa saba waliohusika na tukio hilo lilitokea katika eneo la Mtaa wa Congo.


Akithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kukamatwa kwa mtuhumiwa,Afisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi,Renatha Mzinga alimtaja ndugu Ally Manially(22)mkazi wa mtaa wa Kongo kuwa anashikiliwa na Jeshi hilo na atafikishwa mahakamani leo kujibu shitaka la kujeruhi na kujipatia pesa kwa njia ya Udanganyifu ikiwa pamoja na kumchoma mwenzie Moto huku akijua ni kosa kisheria.

Aidha Mzinga alieleza kuwa Jeshi la polisi linaendelea kutafuta watuhumiwa wengine 6 waliohusika na tukio hilo

ZANZIBAR YAPIGA MARUFUKU NDOA ZA JINSIA MOJA.....UKINASWA IMEKULA KWAKO ( MIAKA 30 JELA )




Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imetunga sheria ya kupiga marufuku ndoa za watu wa jinsia moja.Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Bwana Abubakar Khamis Bakar, aliyasema hayo kwenye Kikao cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi, Saleh Nassor Juma kutoka Chama cha Wananchi (CUF).

Katika swali lake, Bw. Saleh Nassor Juma alitaka kujua ni lini Serikali ya Zanzibar itatunga sheria ya kukataza ndoa hizo na kuweka adhabu kali kwa watu ambao watabainika kufanya vitendo hivyo vichafu. 


Waziri Abubakar amesema, ndoa za watu wa jinsia moja ni kinyume na utamaduni wa Zanzibar na kwamba sheria hiyo imeweka adhabu ya kifungo cha miaka saba kwa wale wote watakaopatikana na hatia hiyo.

Pia alisema kama ninavyomnukuu: "Sheria hii inahusu makosa mengi yakiwemo ya ubakaji, zinaa, usagaji na umalaya ambayo yote yana adhabu ya kifungo cha maisha au miaka isiyopungua 30 gerezani," mwisho wa kunukuu.

HUYU NDO MSHIRIKI WA BBA KUTOKA ZIMBABWE ALIYE CHEZA MKANDA WA NGONO.....WANANCHI WAMEJIPANGA KUMNG'OA



Mshiriki wa shindano la Big Brother Africa Chase kutoka nchini Zimbabwe Nare Pokello amejikuta katika kashfa kubwa baada ya mkanda wake wa ngono kuvuja siku chache tu baada ya yeye kuingia ndani ya jumba la BBA.

 kashfa hiyo ambayo sasa ndio habari ya mjini imezagaa  katika  kurasa kadhaa za Facebook huku mashabiki wengi kutoka nchini kwake wakisistiza watu wampigie kura ya kumng'oa  Pokello nje ya jumba hilo  . 

Mashabiki hao wametengeneza ukurasa hivi karibuni, ambao unashinikiza watu wapige kura za kumng'oa Pokello katika jumba hilo la BBA, Ukurasa huo ulioundwa wiki hii mpaka sasa tayari una zaidi ya wafuasi zaidi ya 4 000.
Katika video hiyo ya ngono, Pokello na mpenzi wake "Desmond Chideme " maarufu kama Stunner wanaonekana wakifanya ngono bila kutumia kinga.

Video hiyo ambayo ilirekodiwa kwa kutumia simu ya iphone na kubadilishwa kwenda kwenye fomati ya avi ilivuja baada ya boyfriend wa pokello kuitoa video hiyo na kumpa rafiki yake wa karibu huku akijisifu.

Katika video hiyo, Stunner anaonekana akizungumza mbele ya kioo cha kamera huku Pokello akiwa anatabasamu. 


video mwishoni inamwonyesha, Pokello akiwa ana ananyonya uume wa Stunner huku Stunner akisema 'wewe msichana ni kituko'.

Chanzo kimoja kilisema Pokello alivujisha video yake mwenyewe na kudai kama siyo yeye aliyevujisha ni Kwa nini alikubali kufanya hivyo kama hawakuwa na nia ya watu kuiona?

Thursday, May 30, 2013

K' LYNE AWEKA WAZI UHUSIANO WAKE NA REGINALD MENGI



Kumekuwepo na Minong'ono mingi lakini hapakuwa na ushahidi wa hili mpaka mwanadada huyo alipoamua kuanika hadharani kuwa mheshimiwa Reginald Mengi ndiye baba halali wa mapacha wake wawili. 

Hongera Mmiliki  wa makampuni ya IPP bwana REGINALD mengi kwa kumiliki mtoto mkali  Jackline Ntuyabaliwe(K'lyne)  ....

Hiyo ndo Tweet ya K'lyne kwa mpenzi wake Mh. MENGI

MBINU ZA KIMAHABA ALIZOZITUMIA KARRUECHE TRAN KUUTEKA TENA MOYO WA CHRIS BROWN




Kwa kawaida mapenzi hutawaliwa na hisia za kimahaba alizonazo mtu kwa mwenziwe ama mtu anaetamani kuwa nae kama boyfriend/girlfriend wake ama mke/wake. Lakini hakukosea aliyesema mapenzi ni kama mmea unaweza kutunzwa na kustawi na ukiachwa bila matunzo unaweza kunyauka. 


Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa mrembo Karrueche Tran aliyetoswa vibaya na Chris Brown lakini kwa kuweka mikakati ya dhati na kuumwagilizia vyema mmea wa penzi kati yake na na Chris hata wakati akiwa hana muda nae na anahang out na Rihanna kumemsaidia kurudisha kwa kasi na nguvu mpya penzi alilopoteza.
 
Moja kati ya mikakati ya kimahaba aliyoitumia Karrueche huku moyoni mwake akiuamini msemo wa ‘mvumilivu hula mbivu’, ni kujiweka karibu na Chris kama rafiki hata wakati akiwa bado yuko na Rihanna na hakuonesha chuki ya wazi kwake japokuwa alikuwa anaumia sana. 


Mkakati mwingine ni kuhakikisha anaonesha moyo wa upendo wa dhati na nia ya kuwa na Chris Brown kwa kuwa alijua kabisa kuwa mwisho wa siku ataangalia zaidi anakooneshwa kupendwa na kuvumiliwa, akijua mwisho wa siku akiumizwa na kulizwa huko aliko atahitaji kufutwa machozi na kutulizwa, na Karrueche atakuwa karibu zaidi, na kweli ndicho kilichotokea.



Chanzo cha karibu na KT kimesema, “Karrueche hakuwahi kuacha kumpenda Chris, hakuwa kulazimisha kitu chochote kwake kwa upande wa mahusiano, na hakuwahi kulazimisha kupewa kitu mkononi au kuomba chochote kwake.”



Mkakati huo pia ulimuongezea alama za ushindi kwa jamaa, lakini pia alijua kabisa ya Rihanna yatapita tena, kwa imani yamepita kweli. “Alijua alikuwa bado anafanya vyote na Rihanna na alitegemea hilo na muda wote alikuwa rafiki kwa Chris Breezy hata wakati akiwa na Rihanna.” Kiliendelea kufunguka chanzo hicho.



Kwa sasa KT amehamia nyumbani kwa Chris na ripoti zinasema ni takribani nusu mwezi hivi na wanaishi kama mke na mume.

AIBU YA BIG BROTHER: VIDEO ZA MAPENZI ZAANZA KUONEKANA KATIKA NYUMBA ANAYOIONGOZA FEZA KESSY WA TANZANIA



Ikiwa ni usiku wa pili (usiku wa kuamkia leo)katika reality show ndani ya jumba la Big Brother Africa mwaka huu lilipewa jina la ‘The chace’ mambo mengi mapya yameanza kuonekana kwa washiriki ambao wameanza kufahamiana.
 
Katika hali ambayo mara nyingi haikwepeki hasa wanapokutana wanawake warembo na wanaume watanashati, scene za mapenzi zimeanza kuonekana katika Diamond house inayoongozwa na mtanzania Fezza Kessy (Head of house) ....

‘Bolt’ , mshiriki kutoka Sierra Leone na Betty ambae ni mshiriki kutoka Ethiopia walipata nafasi ya kufahamiana zaidi na kuvuka mstari wa urafiki wa kawaida wakati washiriki wengine wakiwa wamelala  ndani ya jumba la Kessy
Betty na Bolt..

Betty ambae yuko nominated pasipo yeye kufahamu, sasa yeye na Bolt ndio waliothibitishwa kuwa couple ya kwanza, japo hatima ya mahusiano yao huenda ikawa hatarini kwa kuwa jumapili hii kura za watazamaji zitaamua hatima ya Betty kuendelea kuwa katika jumba hilo au kurudi Ethiopia. 

"SITAKI KUSIKIA NYIMBO ZA NGWEA ZIKIPIGWA CLOUDS FM..WAO NDO WALIOMFANYA AANZE KUVUTA BANGI ILI KUONDOA MAWAZO"...P FUNK




Muda mfupi uliopita djchoka amepokea simu kutoka kwa Producer mkongwe hapa bongo anayejulikana kwa jina la P Fuck Majani na kumuuomba aipokee msg hii hapa chini na kuwaomba watanzania walijue hili na baadae atatoa barua rasmi.

Tuesday, May 28, 2013

CHANZO CHA KIFO CHA MSANII ALBERT MANGWEA



Ngwea akiwa na msanii M to the P jana south africa.

Hussein Original ambaye yupo Pretoria amesema Ngwear  na   M to the P  ambaye walikuwa room moja walitakiwa kurudi Tanzania leo  wakitokea  Afrika kusini..

Walipowapitia,  waliwakuta wamezima kwenye room wote wawili baada ya kuji overdose madawa ya kulevya...
 
Mpaka sasa M to the P yupo hoi  katika  hospitali ya St. Hellen  huku  msanii Ngwair  akiwa  tayari  amekwishaaga  dunia.....

Tunaendelea  kufuatilia  undani wa  tukio  hili

R.I.P NGWAIR 

Mke wa Mshikaji Wangu Aniduwaza!



Jana nimeduwazwa sana baada ya mke wa rafiki yangu kunitamkia wazi kuwa ananipenda na anataka kutoka na mimi.
Tangu nifahamiane naye miaka takribani mitano sasa tumekuwa tukiheshimiana naye sana kama mashemeji. mwaka huu akaniambia kuwa mumewe ameanza kubadilika kwa kuzidisha ulevi, kuchelewa kurudi nyumbani na wakati mwingine kulala nje na pia alizifuma meseji za mapenzi kwenye simu ya mumewe kutoka kwa mtu aliyemsave kwa jina la kiume, hivyo nimsaidie kumshauri ili abadilke ila akanionya nisimwambie kama ni yeye ndiye kaniambia.

Nilimtia moyo kuhusu hali hiyo na kumwomba awe mvumilivu na asichoke kuongea na mumewe kuhusu hali hiyo ili abadilike. Binafsi nilipata wakati mgumu wa namna gani nitamshauri jamaa bila kumtajia makosa yake na wapi nimeyapata hivyo nikashindwa hiyo kazi.
 

Mke wa jamaa akaanza kunipigia simu usiku kulalamika kila mumewe anapochelewa kurudi na wakati mwingine akinipigia alfajiri kuniambia kuwa mumewe hajarudi hadi muda huo. Niliendelea kumtia moyo ingawa mambo hayo yalikuwa ni ya kweli.
 

Cha ajabu kuanzia wiki jana amekuwa akinitumia meseji za mapenzi, nikajua ni hizi meseji ambazo watu hutumiana hivyo sikujali sana hadi pale aliponiandikia akiniambia kuwa yuko serious anataka kutoka na mimi. Sikuamini nikampigia simu kusikia sauti yake kama ni yeye kweli, ndipo aliponithibitishia kuwa yuko serious na atatunza siri na kunitunzia heshima yangu kwa jamaa kwani tayari moyo wake umeangukia kwangu.
 

Sikuweza kumjibu kitu kwa namna nilivyopatwa na mshangao. hadi sasa anaendelea kunibembeleza na kunipa mbinu nyingi za kutimiza lengo lake bila kujulikana na watu.
 

Binafsi sina lengo la kumsaliti mshikaji wangu ila nimelileta kwenu ili mnishauri nimjibu vipi huyu mwanamke ili heshima yangu kwa familia hii iendelee kuwapo na pia kusitokee chuki yoyote kutokana na kadhia hii itakayopelekea urafiki wangu na familia hii kuyumba au kupotea.

AIBU: KIJANA ANASWA AKIUZA UUJME WA MTU....POLISI WATIA MBARONI



Jeshi la polisi nchini malawi wanamshikilia kijana mmoja baada ya kumkuta akiuza sehemu ya siri ya mwanaume.

Kijana huyo mwenye miaka 24 alikamatwa baada ya wananchi kutoa ripoti kituo cha polisi kuwa kunamzee kalala relini huku akiwa anatokwa damu nyingi 
 Polisi walifika eneo la tukio na kumkuta mzee huyo akiwa hoi na kuamua kumkimbiza hosipitali.

Baada ya kufikishwa hosipitali, madaktari  gundua kuwa mzee huyo alikuwa amejeruhiwa kwa kukatwa sehemu zake za siri...

Madaktari hao walilipoti kwa maofisa hao wa polisi na ndipo msako mkali ulipo pita katika wilaya ya Lakeshore mjini Salima na polisi hao kufanikiwa kumtia mbaroni kijana huyo baada ya kumkuta  akiwa katika gesti bubu akijaribu kuuza uume huo kwa dola za kimarekani 360.
  Mtuhumiwa Samuel Banda

Polisi walisema mtuhumiwa Samuel Banda alikamatwa na kiungo hicho ambacho alikuwa amekifunga katika karatasi nyeupe.

Mtuhumiwa alikiri kuwa huwa anauza viungo mbalimbali vya binadamu kwa wafanya biashara maarufu nchini humo ambao wanaamini wakivipata viungo hivyo huwasaidia katika biashara zao na huwaongezea utajiri.

AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA KWA KOSA LA KUMLAWITI MTOTO WA MIAKA WA MIAKA 7


MKAZI wa kijiji cha Turiani, Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga, Athuman Rashid (25) amehukumiwa kutumikia kifungo cha maisha jela na adhabu ya kuchapwa viboko sita baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa miaka saba. 
Hukumu hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Korogwe, Arnold Kirekiano.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka iliyosomwa na Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Janson Zakaria alidai Athuman alitenda kosa hilo Juni 21 mwaka jana, saa 11.00 jioni katika kijiji cha Turiani wilayani hapo. 
 
Hati hiyo ya mashitaka inadai Athuman alimuita mtoto huyo ambaye alikuwa akiishi na bibi yake kijijini hapo kwa lengo la kumtuma dukani ndipo alipomtendea unyama huo. 
 
“Alipokuwa akifanyiwa tendo hilo mtoto huyo alipiga kelele na baadhi ya majirani kujitokeza kufika eneo hilo huku, mtoto huyo akilalamika kwa maumivu sehemu ya siri na akimtaja mtuhumiwa,” alidai Zakaria. 
 
Kabla ya Hakimu Kirekiano kutoa hukumu alimtaka mshitakiwa kama ana chochote cha kujitetea aeleze mahakamani; naye akasema hana cha kujitetea, Mahakama iamue. 
 
Hakimu alisema kifungo hicho cha maisha jela na viboko sita, iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

DIVA WA CLOUDS FM AMPA SUPPORT "MKE MWENZA WA KENYA " ANAYEIWAKILISHA NCHI HIYO KWENYE BIG BROTHER AFRICA


juzi (May 26) ndio ulifanyika ufunguzi rasmi wa shindano kubwa Africa la Big Brother ambalo mwaka huu limepewa jina la “The Chase”, na tayari washiriki wa nchi zote ikiwemo Tanzania wamekwisha fahamika.

Huddah Monroe a.k.a The boss lady ambaye ni model mwaka huu ndio amebeba imani za wakenya za kurudi na kitita cha $300,000 zinazoshindaniwa katika msimu wa 8 wa shindano la Big Brother “The Chase” baada ya kuchaguliwa kuiwakilisha nchi hiyo ya jirani. 
 
Siku chache zilizopita jina la Huddah limeonekana kupata umaarufu zaidi Tanzania hasa kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, baada ya binti huyo mwenye historia ya matukio mengi ya utata huko Kenya (pamoja na kujihusisha na upigaji wa picha za utupu) kujikuta anaingia katika ugomvi wa maneno na mtangazaji maarufu hapa Tanzania Loveness Love a.k.a Diva kutokana na kinachoaminika kuwa sababu ni Prezzo. 
 
Diva a.k.a mimi Kupitia akaunti yake ya twitter, juzi (May 26) aliandika tweet inayoonesha kuweka kando tofauti alizokuwa nazo na Huddah na kuahidi kumsupport kwa kutokumwandikia “shit” kama njia ya kumuunga mkono “wifi” katika BBA.

Diva amekuwa akidai kuwa na mahusiano ya kimapenzi na rapper kutoka Kenya CMB Prezzo, kitendo kilichopokelewa tofauti na mrembo Huddah ambaye pia kulikuwa na tetesi aliwahi kudate na “Liq Her” hit maker, Rapcellency, Prezzo.

Monday, May 27, 2013

JACK WOLPER ALIA NA MATAPELI YANAYOTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KWA JINA LAKE KUOMBA HELA WATU



Katika kile kinachoonekana ni mwendelezo wa matapeli wa mjini kutumia majina ya waigizaji maarufu nchini kutapeli watu kwa njia ya mtandao, dhahama hii sasa imemkuta mwanadada Jacqueline wolper baada ya watu wanaoaminika kuwa ni matapeli kutumia jina lake kujipatia fedha na vitu vingine kiudanganyifu.

Akizungumza kwa simu na tovuti ya bongomovies, mwanadada Jacqueline wolper  alisema matapeli hawa sasa wameamua kutumia mtandao wa instagram na mtandao mwingine wa kijamii uitwao badoo kwa jina la “wolper gambe25” katika kutapeli watu kwa kuwaomba hela au michango mbalimbali kupitia account hizo feki

“Leo nilikuwa naenda saluni, baada ya kufika tuu, yule dada wa saluni akaanza kunilalamikia kuwa mbona sijaenda kuchukua viatu nilivyomuagiza pamoja na hela? 

  
Nikawa sijui cha kumwambia maana sikumuagiza viatu na wala sijampigia simu kumwambia anitumie hela, ndipo aliponionesha huo ujumbe kwenye simu yake na ndio nikagundua hizo account feki za hao watu wanaoutumia jina langu kutapeli watu” Alisema Jack.

“Mimi sipo facebook na wala sitarajii kujiunga, nawaomba sana mashabiki wangu wajue hilo. Natumia mtandao wa instagram kwa jina la wolpergambe au jacklinewolperjacklinewolper.”
 Alisisitza Wolper

Pia alisema kuwa amegundua leo kuna mtu mwingine anayetumia jina lake kuomba watu wamchangie kuhusu kampeni inayoitwa“Zinduka” na amewataka sana mashabiki wake wasije wakafanya hivyo kwani mtu huyo ni mwizi na analengo la kumchafulia jina lake.

HII NI NEEMA KWA WALIOFELI KIDATO CHA NNE....UFAULU WAONGEZEKA, MATOKEO NI MUDA WOWOTE


Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana imeongezeka kwa kati ya asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kufanya marekebisho alama za viwango vya ufaulu, Mwananchi limebaini.

Habari ambazo gazeti hili imezipata zinasema matokeo hayo ambayo yamewezesha kiwango cha ufaulu kupanda na kufikia asilimia kati ya 54 na 57, huenda yakatangazwa wiki hii pamoja na yale ya kidato cha sita ambayo pia yamechelewa kutangazwa.

Chanzo cha habari kutoka Necta kimesema matokeo hayo mapya yanaonyesha kuwa, ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la nne umeongezeka kutoka asilimia 34.5 kwa matokeo yaliyotangazwa awali na huenda yakafikia asilimia 57. Hii inamaanisha kwamba watahiniwa wapatao 82,000 ambao awali walikuwa wamepata sifuri katika matokeo ya awali sasa wamepanda na kupata madaraja ya ufaulu katika matokeo mapya.

Kwa matokeo hayo, watahiniwa wa mwaka 2012 watakuwa wamefanya vizuri kuliko wa mwaka 2011, ambao watahiniwa 225,126 sawa na asilimia 53.37 ya 349,390 waliofanya mtihani huo walifaulu.

Msemaji wa Necta, John Nchimbi alisema upangaji wa matokeo hayo ulikuwa bado unaendelea. “Ninachojua kwa sasa ni kuwa mchakato unaendelea na matokeo yatatangazwa mapema tu ili watoto waweze kujiunga na shule mapema,” alisema Nchimbi.

Pia alisema usahihishaji wa mitihani ya kidato cha sita umekamilika.

Matokeo ya awali

Matokeo ya awali yaliyotangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa yalionyesha kuwa kati ya watahiniwa 367,756 waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, waliokuwa wamefaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu walikuwa 126,847 sawa na asilimia 6.4. Waliopata daraja la nne walikuwa ni 103,327 sawa na asilimia 28.1.

Katika matokeo hayo, watahiniwa 240,909 sawa na asilimia 65.5 walipata sifuri, hesabu ambayo imebadilika katika matokeo mapya ambayo yanaonyesha kuwa sasa waliopata daraja hilo ni 158,100 ambayo ni asilimia 43.

Hata hivyo, habari kutoka Necta zinasema kuwa licha ya kuwezesha kuongezeka kwa waliofaulu, matumizi ya kanuni mpya ya kukokotoa matokeo hayo yalisababisha zaidi ya wanafunzi 2,500 kushuka ufaulu ikilinganishwa na awali.

Maofisa mbalimbali wa Necta pamoja na wale wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na taasisi zake, walikutana mwishoni mwa wiki iliyopita kukubaliana masuala mbalimbali juu ya matokeo hayo pamoja na suala la matokeo ya wanafunzi hao 2,500 kabla ya kutangazwa wiki hii.

“Baada ya wajumbe kujadili suala lile, busara ilibidi itumike kwa hiyo hakuna mwanafunzi ambaye alama yake itashuka, kwa kawaida isingewezekana mtoto ambaye matokeo yalitoka akiwa amefaulu leo umwambie ameshuka,” kilieleza chanzo chetu.
Matokeo ya awali ndiyo chimbuko la kupitiwa upya baada ya wadau kuyalalamikia na kumlazimisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuunda tume ya kuyachunguza Februari 23, mwaka huu.
Kabla ya tume hiyo kuhitimisha shughuli zake, ilitoa taarifa ya awali ambayo ilipendekeza kufutwa kwa matokeo hayo kwa maelezo kwamba Necta ilitumia kanuni mpya ya kukokotoa matokeo bila kushauriana na wadau.
Serikali ilitoa taarifa bungeni kwamba imeamua kufuta matokeo ya 2012 na kuamuru yapangwe upya kwa kufuata madaraja yaliyotumika mwaka 2011.