Sunday, March 31, 2013

TASWIRA YA UOKOAJI UKIENDELEA KATIKA AJALI YA JENGO LA GHOROFA 14 LILILOPOROMOKA DAR NA KUUWA WATU KADHAA



 


Jengo la Ghorofa 14 lililokuwa likiendelea kujengwa pembeni kabisa mwa Msikiti wa SHIA Mtaa wa INDRA GHAND na Zanaki, limeporomoka na kusambaratika na kusababisha vifo vya watu kadhaa ambao hadi sasa idadi haijaweza kupatikana kutokana na waokoaji kukosa vifaa vya kutosha katika zoezi hilo la uokoaji. Imeelezwa kuwa ghorofa hilo limeporomoka leo asubuhi majira ya saa moja na nusu ambapo ulianza kusikika mlio kama 'Tetemeko la ardhi'.
Aidha imeelezwa kuwa katika Jengo hilo walikuwepo mafundi ambao walikuwa wakiendelea na ujenzi na chini alikuwepo Mama Lishe, aliyekuwa akiuza chai na eneo hilo pia walikuwapo watoto wadogo ambao haikuweza kufahamika idadi yao waliokuwa wakicheza eneo hilo, ambao wote inasemekana wamefukiwa na kifusi cha ghorofa hilo, huku waokoaji wakifanikiwa kumpata mtoto mmoja tu ambaye hata hivyo imeelezwa hali yake ilikuwa ni mbaya na kuwahishwa hospitali.
Ni moja ya Kifaa pekee kilichokuwepo eneo hilo Trekta, likifukua kifusi ili kuokoa watu wanaodaiwa kufukiwa na kifusi hicho.
Baadhi ya watu waliwahi kufika kujaribu kutoa msaada bila mafanikio hapa wakiwa wamekwama baada ya kukosa vifaa vya kutosha

No comments:

Post a Comment