Sunday, April 28, 2013

Nassari Akiwa na Lema Mahabusu



Kushoto ni Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akiwa katika chumba alikohifadhiwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.Dar es Salaam, Tanzania. Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari LEO amemtembelea Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ambaye yuko mahabusu baada ya kutiwa mbaroni na Jeshi la Polisi, mkoani Arusha, Tanzania.

Nassari pamoja na mambo mengine amemtembelea Lema ili kujua kilichotokea wakati akizungumza na wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu  Arusha (IAA) na baadaye kukamatwa na polisi.

Mbunge huyo Arumeru Mashariki amewasili Leo Arusha na kwenda moja kwa moja katika Kituo Kikubwa Cha Polisi (Central).

Jana Nassari alinukuliwa akisema kwamba Leo yeye na Halima Mdee (Kawe) watakutana na kuzumgumza na Mulongo kuhusu

kilichotokea katika chuo hicho cha uhasibu na kusababisha kukamatwa kwa Lema.

“Jumatatu (leo) tunatarahia kuonana na mkuu wa mkoa na tayari nimempa taarifa. Tunataka kuzungumza  naye kilichotokea na hali ya kisiasa  iliopo Arusha hivi sasa,” alisema Nassari.

Mpaka sasa haijafahamika Nassari amezungumza nini na Lema.

No comments:

Post a Comment