Polisi wa Kituo cha Nandi chini Kenya wanamshikiria mwalimu mkuu wa shule ya msingi St. Paul kwa kosa la kumpa mimba mwanafunzi wa darasa la sita na kisha kumlazimisha aitoe....
Kwa mujibu wa bodi ya shule hiyo, mwalimu huyo amekuwa akifanya mapenzi na mwanafunzi huyo wakati wenzie wakijisomea darasani nyakati za usiku katika masomo ya jioni.....
Binti huyo aliyekumbwa na mkasa wa aibu alikuwa ni kiranja mkuu wa shule hiyo na inadaiwa kuwa mwalimu mkuu ndiye aliyesimamia uteuzi wa binti huyo ili aweze kumnasa kiulani.....
Habari zinadai kuwa baada ya mwalimu huyo kugundua kuwa binti huyo anamimba, mipango ya kuitoa mimba hiyo ilianza mara moja....
Kwa mujibu wa mwalimu mmoja wa shule hiyo,Zoezi hilo chafu lilifanyika katika hospitali ya wilaya ya Kapsabet na kwamba wakati oparesheni hiyo haramu ikifanyika, walimu wenzake walipata taarifa kutoka kwa mmoja wa manesi wa hospitali hiyo na ndipo walipochukua hatua ya kuwajulisha wazazi wa binti huyo ambao waliamua kwenda polisi.....
No comments:
Post a Comment