Biahara zote zilisimama kwa muda katika stendi kuu ya mabasi ya Bomet nchini kenya wikiendi hii baada ya kundi kubwa la wanaume kumvamia mwanamke mmoja aliyekuwa amevaa kingua kifupi na kisha kumvua huku wengine wakimchezea nyeti zake.....
Mwanamke huyo ambaye inadaiwa alienda katika stendi hiyo kufanya booking ya basi,alikutwa na kisanga hicho baada ya kuvamiwa na kundi kubwa la wapiga debe na vibaka ambao walianza kwa kumzomea na kumrushia makopo ya maji......
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo,sakata hilo lilichukua takribani dakika 15 za kumzomea na kumtukana wakiwa wamemzunguka kabla ya kumvua nguo zake.....
"Walimzomea na kumtukana vibaya huku wakiwa wamemzingira.Juhudi za wanawake wasamaria wema kumuokoa zilikwama kwa kuwa kundi lilikuwa kubwa na wao walikuwa wanaogopa kufanyiwa hivyo"...Alisema shuhuda huyo
Mbali na shuhuda huyo,Bwana Sang naye analielezea tukio hilo kwa kudai kuwa ile sketi ilikuwa ni zaidi ya fupi na pia ilikuwa nyepesi na ndani ndani hakuwa na kitu, hali iliyosababisha wapiga debe hao wamvae na kumvua.....
Bwana Sang anadai kuwa kesi nyingi za ubakaji zimekuwa zikisababishwa na wanawake wenyewe kutokana na mavazi yao wanayoyavaa....
Baada ya tukio hilo kupamba moto, polisi walifika japo walichelewa na hatimaye kufanikiwa kumwokea mrembo huo mikononi mwa vibaka hao....
Kutokana na tukio hilo,shirika la maendeleo ya wanawake limelaani vibaya tukio hilo na kuahidi kuchukua hatua kali zaidi endapo udhalilishaji huo utaendelea na kufumbiwa macho....
No comments:
Post a Comment