Tuesday, April 9, 2013

MWAKYEMBE ASHANGAZWA NA ONGEZEKO KUBWA LA NAULI.... AMETOA AGIZO LA KUZUIA KUPANDA KWA NAULI ZA TRENI



 
 Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amewatuliza Watanzania kuhusu kupanda kwa nauli akisema ameyapokea malalamiko  yao na atayafanyia kazi.
 
 Kwa kuanzia ameagiza nauli za treni jijini Dar es Salaam zisipande bali ziendelee kutozwa za zamani  mpaka taarifa zaidi itakapotolewa.
 
Mwakyembe alitoa kauli hiyo alipozungumza kwenye Bonanza la Vyombo vya Habari lililofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Alisema ni kweli Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra|) ilitangaza nauli mpya, lakini kwa kilio cha Watanzania ataangalia sababu za kupandisha huku akishirikiana na wasafirishaji kujua ukweli.

No comments:

Post a Comment