Wednesday, April 17, 2013

WATENGENEZAJI WA SIMU FEKI WAKAMATWA


 



Mtu na mkewe wamekamatwa huko China kwa kutengeneza simu feki za Apple.

Watu hao ambao hawajatajwa majina wamekuwa wakitengeneza spea za bandi za simu za Apple kisha huzipeleka Apple na kudai wameletewa spea mbovu, na Apple bila ajizi huwabadilishia na kuwapa spea halisi ambazo huenda kuziunga na kupata simu orijino za apple.
Watu hao ambao wamekamatwa pamoja na wafanya kazi wao watatu walikuwa wamekabidhi spea feki za Iphone 4s pea 121 ambavyo wangeviunga na kupata Iphone mpya kabisa ambazo wangeziuza katika duka lao.
Wahalifu hao walishitukiwa na wafanyakazi wa Apple ambao waliitaarifu polisi ambao hawakusita kuwatia mbaroni, wao na wafanyakazi wao.

No comments:

Post a Comment