Saturday, April 6, 2013

MAPENZI YA SIRI
Naomba kushare hii na wadau , Kwa kifupi niko kwenye mahusiano mapya yapata miezi nane tu, na Jamaa keshanitangazia Ndoa , tatizo linakuja anataka tufunge Ndoa ya Siri ya Serikalini then baadaye ndiyo tunakuja Bariki Kanisani , Nikiuliza sababu ni kuwa anajaribu kukwepa Complications za Kanisa kwa kuwa hana Vyeti vya Ubazito na Wazazi wake woote walishafariki, Nikimshauri tukajieleze kanisani anakataa , amekazana hiyo haita kubaliwa tutapoteza muda ni heri tufunge kwanza Serikalini , then tuanze na kufuatilia ya Kanisa Taratibu
Nikimpekua pekua simkuti na chochote cha kunioneshea labda anamahusiano na kama anayo basi ni Msiri sana
Mbaya zaidi hiyo Ndoa ya Serikali hataki wapambe wala kuvaa Shela wala Picha eti tuende na nguo za kawaida tu kupunguza Bajeti !
heshima ya Ndoa ninaitaka lakini mbona hii hainiingii, kuna inayemuingia hapa ?Hivi Raha ya Ndoa ni nini si ujumuishe watu ??au nimekutana na JINI Maana hana Ndugu wengi , zaidi ya Jamaa za hapa na pale
Desperate Woman
NAOMBA MNISHAURI

No comments:

Post a Comment