Chama cha Kutetea Abiria Tanzania (CHAKUA) kimesema kinaiburuza kortini Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchikavu (SUMATRA), kwa madai kuwa hakikushirikishwa kwenye mchakato wa kuongeza nauli za abiria.
Aidha, CHAKUA kimeitaka serikali kuuwajibisha uongozi wa juu wa SUMATRA kwa kuifuta na kuunda upya kwa madai kwamba imeshindwa kusimamia maslahi ya wananchi wanyonge.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mshauri wa chama hicho, Wilson Mashaka, alisema tangazo la kupandisha nauli halikujengwa kwa dhana ya ushirikishwaji, kwani vikao vilivyofanyika kati ya Septemba na Novemba, 2012, vilifanyika kwa kuwashirikisha wamiliki wa mabasi lakini wadau muhimu kama CHAKUA hawakushirikishwa.
No comments:
Post a Comment